FRANCIS GODWIN aenda Mafichoni akihofia kifo kabla ya kujojiwa juu ya kifo cha Daudi Mwangosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

FRANCIS GODWIN aenda Mafichoni akihofia kifo kabla ya kujojiwa juu ya kifo cha Daudi Mwangosi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Sep 7, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=3]HOT NUUZ: FRANCIS GODWIN :NIMECHAGUA KUWA MKIMBIZI KATIKA KTK MKOA WANGU. AENDA MAFICHONI AKIHOFIA KIFO KABLA HAJATOA USHAHIDI NA KUSEMA UKWELI WA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI![/h]  [h=3][/h]

  [​IMG]Mmiliki wa mtandao huu http://www.francisgodwin.blogspot.comBw.Francis Godwin (kushoto) akitoka kujisalimisha polisi akiwa na mkewe Vumilia Mwangosi (kulia) ambaye ni dadake na marehemu Daudi Mwangosi
  [​IMG]Hapa mzee wa matukio daima akiwa na mkewe katika basi
  [​IMG]Maisha ni safari ndefu yenye misukosuko mingi ila katika maisha ukichagua kuwa mkweli kifo kwako ni rafiki wa karibu sana.

  Daudi Mwangosi ameuwawa kwa kusimamia ukweli na kutimiza wajibu wake kama mwanahabari ,leo mimi nalazimika kukimbia mkoa wangu wa Iringa ambao nilitokea kuupenda zaidi kutokana na kusimamia ukweli juu ya kifo cha mwenyekiti wangu katika klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa ,pia kama shemeji yangu na tatu kama mwanaharakati wa kweli katika kutetea wanyonge .

  Ila cha kushangaza mbali ya kuwa mimi si muuaji wa Daudi Mwangosi jeshi la polisi wameanza kuniwinda mimi kama shuhuda wa tukio badala ya kuwasaka wauwaji kweli inanishangaza sana ila ndio Tanzania yetu .

  Hivyo kutokana na kuendelea kufuatwa fuatwa usiku na mchana binafsi nimechangua kuwa mkimbizi katika mkoa wangu huku nikisimamia ukweli ule ambao ninao na kamwe sitakubali kusema uongo kwa kile nilichokiona nawapenda sana wana Iringa na kuamua kuukimbia mkoa si kwa ajili ya kuwakimbia wakazi wa mkoa wangu nimeamua kwenda mafichoni kwa muda ili kupisha wenye roho mbaya kutaka kunitoa uhai wangu kabla ya kutoa ushahidi wangu.

  Iwapo nitapata nafasi zaidi nitaanika kila kitu hapa ili kukuwezesha wewe mdau kujua kilichotokea hadi leo kukimbia mkoa.
   
 2. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  khaaaaaa MUNGU AMLINDE na mkono wa dhuluma na mauaji wa kikwete! amen!
   
 3. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,334
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  aende moja ya balozi wampe hifadhi
   
 4. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Pole sana Francis Godwin kwa kumpoteza mwenzako na huku ushahidi ukiwa nao! hakika kama kweli ukweli uongo hujitenga!
   
 5. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  pole sana kaka godwin, pengine tanzania is the most dangerous place to live kwa sasa, jihadhari na mtu anayeitwa ramadhan ighondu moja ya evils people aliyewahi ku exist kwenye hii nchi
   
 6. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Bro umefanya vema kwani waliomtesa Ulimboka walikuwa wanakuotea. Ila sema mapema usije kuwa unakufa na siri moyoni. Recodi kwenye CD wape ndugu na marafiki ili leo na kesho wakikukamata hiyo kumbukumbu ibaki. Usikubali kupewa hela kama akina Ulimboka la sivyo utakuwa umemsaliti mkewo na shemeji yako Mwangosi na mama mkwe na damu yake itakuwa juu yako na vizazi vyako. Fanya kiume usimame kama mwanaume useme yooote tunakutakia ushupavu mwema.
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  .. itakua ni vigumu zaidi jamii yetu hii kukubali kupokea damu zaidi ya kisiasa popote pale nchini tena; na hili watawala ni vema wakalitilia mkazo kidogo vile.
   
 8. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,494
  Trophy Points: 280
  ... Baada ya kusikiliza ushahidi wa Francis Godwin-mtu pekee aliyelishuhudia tukio lote la mauaji, nashawishika kuamini kwamba askari aliyeua akipelekwa mahakamani atashinda kama hakutakuwapo ushahidi mwingine wa askari aliyekuwapo ktk tukio lile. Ktk maelezo yake (sikiliza channel 10 jmosi au kupitia youtube) ameacha mianya mingi ktk maelezo yake kiasi kwamba ushahidi wake hauwezi kukubaliwa. Mfano, anakiri alileweshwa na moshi wa mabomu. Kukiri kulewa tayari ni loophole. Pili, anakiri kwamba hakuona kilichotokea-alikuwa amegeuka, kurudisha macho tena baada ya mlipuko akaona mwili wa marehem.

  Ndugu watanzania, tujiandae kwa yasiyotarajiwa kama ilivyokuwa ktk suala la Zombe. Yaani, mahakama itakiri polisi waliua, isipokuwa haitajulikana ni polisi gani-kumbuka hata yule anayeonekana anamuelekezea bunduki marehem, sura yake haionekani vizuri.
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  pole sana ndugu yangu..

  mungu akuongoze...!

  taifa linatambua sana michango yenu
   
 10. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole sana Godwin ndio maisha ya utetezi wahaki iwe isiwe haki itapatikana hata kama sio leo basi sio muda mrefu haki itapatiakana
   
 11. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Haya mambo ya kusema utaanika kila kitu hadharani tushayachoka hata dr.Uli alikuja na kauli kama hizo matokeo yake washamtuliza hata haijulikani yuko wapi pamoja na mbwembwe nyingi kuwa atasema kila kitu lakini hakuna kitu.
   
 12. frema120

  frema120 JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 5,103
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  inauma sana
  tunaelekea wapi?
  hivi kwanini tusishawishi
  watanzania wenye kupenda haki
  tufanye kama misri
  tuwatoe hawa magamba......

  "akili ndogo kutawala akili kubwa"
  by mch msigwa
  hii ndio tabu ya miccm

  tupia hapa ukweli usiofu bhana...

  V
  SENGEREMA
   
 13. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa nini unatangaza kuwa unaenda kujificha?!! Just disappear!
   
 14. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Anatafuta umaarufu tu. Yuko kama kunguru anayekimbia bawa lake.
   
 15. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  sura yake haionekani vizuri kivipiwakati wale askari wote wa liokuwa wamzunguka pamoja na wengine walioonekana kwenye picha mbalimbali wameshatambuliwa kwa majina hata mikoa wali
  toka? kwa sababu wewe umeona sura ya muuaji kwa upande unafikiri wanaomjua hawawezi kumtambua?
   
 16. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  watu wengine mnaendeshwa na majini...
   
 17. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmh napata harufu ya TEMBO hivi upepo unaelekea wapi, anywayz Upepo unapita tu huu, Salamu zao kaka ila usiitelekeze Familia kumbuka kuwatumia hela ya Matumizi au unaondoka nao?
  Ukirudi tafadhari weka mambo mezani usitufanyie kama Dr.Uli, Puliiiiiz!!
   
 18. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,033
  Likes Received: 8,520
  Trophy Points: 280
  hivi wewe hujui mitego ya fedha ya zama hizi.?jamaa ndo anaianza safari ya kutoka,unaeza stukia baada ya mda unamuona kitaa,anatembelea masaburi na akiitwa mheshmiwa mbunge kamanda francis..
   
 19. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Wajinga ndio waliwao.
   
 20. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,494
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu, siongei haya kwa nia mbaya. Ni ukweli mchungu. Hao wanaomfahamu watakuwepo mahakamani? Serikali ina nia ya dhati ya kumfikisha mahakamani aliyeua? Jeshi la polisi liko tayari kumtoa kafara Kamhanda? Maana askari wakifikishwa mahakamani, itakuwa lazima kwa Kamhanda kuwajibishwa. I understand many people are looking at this emotionally, but with courts, there has to be no reasonable doubt. If you ask me, partial disclosure of face is a reasonable doubt, especially when there is no credible witness to collaborate the story. Otherwise, tuko pamoja-wote tunapenda waliohusika directly and indirectly wawajibishwe na kushtakiwa. Labda nikuulize ni nan alimuua Mwangosi? Nipe jina moja tu.
   
Loading...