Fozhou China, Mkutano mkuu wa 44 wa UNESCO July 16-31: Utetetezi wetu Watanzania juu ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
9,928
2,000
Exquisite πŸ‘ŠπŸ‘πŸ‘πŸ˜πŸ™πŸ™

Kama dunia inaogopa kiitwacho UHARIBIFU wa mazingira ,basi tusijenge nyumba.....kwani nao ni UHARIBIFU WA MAZINGIRA ....

Wenzetu wa ulaya ,na sisi tungeamua kuishi tu katika MAPANGO ,kuwinda na kurina asali tu..hata KILIMO ni UHARIBIFU wa BAIOANUWAI.....

βœ”βœ”βœ”βœ”πŸ’―%
 
Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
1,413
2,000
Ndivyo ilivyo, watu wengi hawajui kwamba utawala wa kikoloni wa wajerumani wao ndio waliplani kujenga hilo bwawa, utawala wa kiingereza haukuwa na nia ya kufuata hiyo plan ya mjerumani kwasababu mbili, 1--- Mjerumani alikuwa hasimu yao, 2--- Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini wa Muingereza baada ya kukabidhiwa na UNO, tulipopata uhuru Nyerere akaufufua huo mpanga wa kujenga hilo Bwawa kama wenzake akina Gamel Abdul Nasser wa Misri (Aswan dam) na Kwame Nkrumah wa Ghana (Akosambo dam ??), nadhani tulishindwa kulijenga kutokana na gharama kubwa wakati huo au mikopo kutoka Banki ya dunia na IMF ilikuwa na masharti magumu sijui!!--- Mabeberu wa zama hizo walijua na bado wanajua kwamba ukombozi wetu MKUBWA wa kiuchumi ni nguvu za umeme hivyo wakatufanyia hila ya kupeleka propasal huko UNO ili kutangaza Selous iwe ni urithi wa dunia ili katika eneo hilo pasifanyike any 'development" kwa kisingizio kwamba eneo hilo ni urithi wa dunia kwa maana hiyo hukutakiwa kujenga hilo bwawa tena!!, unaona hila na ujanja wa mabeberu??!!--- kweli yapo maeneo yanafaa kupata hadhi ya urithi wa dunia lakini sio kwa Selous, walifanya hivyo tu ili Stieglier isijengwe.

Umeme ndiyo maendeleo, wao wenyewe maendeleo waliyonayo yameletwa na umeme, Usafii wa umeme, viwanda ni umeme, mahospitali, majumbani kupikia nk, ni umeme yaani kila kitu wao ni umeme tena mwingi wa bei rahisi sana kuliko sisi, sasa iweje kwetu umeme iwe ni haramu???--- kitu gani kiko nyuma ya sisi tusipate umeme mwingi rahisi wa uhakika???--- lengo wanataka waendelee kutunyonya sikuzote, tuendelee kukodi mitambo yao ya gesi nk, hui ndio unyonyaji wao.
Utapata lila kitu lakini megawatt 2150 haziwezi kutimia. Inakadiriwa 36% ya maji yaliyokuwapo wakati wa upembuzi yakinifu wa awali yanni mwaka 1978 hayapo kutokana na sababu mbali mbali zikiwapo; miradi mbadala ya Mtera na Kihansi, shughuli za bonde la Ihefu, ongezeko la idadi na shughuli za binadamu na mabadiliko ya tabia nchi.

Hapo ni upotevu wa raslimali tu ulifanywa na Dikteta asiyeshaurika
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,682
2,000
Ni hivi watu wengi wanaandika bila kuujua ukweli.

Ukweli ni kwamba kabla ya mradi wowote mkubwa kutekelezwa lazima kifanyike kitu kinachoitwa Environment Impact Assessment.

Ukweli ni kwamba serikali iliunda team iliyojumuisha maprofesa nguli kufanya Environment Impact Assessment ambapo serikali yetu iliwalipa fedha kufanya kazi hiyo.

Ukweli ni kwamba team hiyo ilifanya kazi hiyo na kuandika ripoti yake ambayo ilieleza kwamba madhara ya kwenye mazingira kama mradi huu ukitekelezwa yatakuwa makubwa sana hivyo wakashauri mradi huu usitekelezwe na wakashauri serikali ijikite kwenye kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ambayo inapatikana mtwara kwani uzalishaji wa umeme kwa kutumia umeme hautakuwa na madhara kwenye mazingira kama mradi wa stiglers gorge.

Sasa bana ripoti hii iliwasilishwa kwanza wizara inayohusika na mazingira ya bwana January. Waziri akakubaliana na ripoti naye akaifowadi Ikulu.

Bwana kilichotokea almanusura huyu Makamba apoteze kazi. Ukweli ni kwamba jiwe alimuita akamtukana sana kwanini amekubaliana na ushauri wa hao maprofesa na kisha akamtupia ripoti yake .

Isingekuwa aibu ya jiwe akifahamu jinsi January alivyomfanyia figisufigisu ya kutengeneza matokeo yaliyomsaidia kumuweka madarakani pale kituo cha Masaki huyu Januari alikuwa afukuziwe mbali.

Sasa twende kwenye hoja, kwa nini serikali yetu inakataa repoti ya timu ya iliyoiunda na kuilipa ifanye kazi na wao wakafanya na wakashauri.

Mbona Serikali hiii hii haitoi vibali vya kuendeleza miradi ambayo environment impact assessment zimeshauri kwamba arhari za mradi ni hasi.? Kuna msemo wa kiingereza unaoheshimika sana unaosema "no research no right to speak" Research imefanyika imeeleza mradi ni mbaya kwenye mazingira watu bila hata kufanya research nyingine wanakurupuka kuukataa ushauri wa wataalamu.

Tusiwalaumu sijui bunge la Ujerumani , mimi binafsi siungi mkono kupangiwa mambo yetu na hao Wajerunani. Ukweli ni kwamba mradi huu ulikataliwa kwanza na timu yetu sisi wenyewe watanzania iliyohusisha maprofesa wataalamu ambao mwisho wa siku kama kawaida ya jiwe ukitoa mapendekezo tofauti na mtazamo wake unaitwa siyo mzalendo au sijui umetumwa na mabepari.

Aina hii ya uongozi ya kukataa mapendekezo ya wataalamu ni mojawapo ya element za utawala wa KIDIKTETA
Mkuu pamoja na kuwaheshimu mno....mno wataalamu,madaktari na maprofesa wetu.....

ILA......

Unalikumbuka sakata la GMO's?!!

GENETICALLY MODIFIED SPECIES(GMO's)ilizua majambo hapa nchini.....

Wako waliosema kuwa ,baadhi ya WAPIGA UPATU NA NZUMARI ya kutumia utaalamu/mbegu hizo za maabara "waliwezeshwa"....waliwezeshwa kutoka nje(hayo makampuni) "fluus,mikabala,faranga,dinari" 🀣🀣

Sisemi WATAALAM wetu wanaweza kupotosha ukweli kutokana na msukumo wa "umatemate",ila kule MAREKANI imeshawahi kutokea PROFESA NGULI WA UCHUMI aliyeaminiwa na nchi KUTOA MAPENDEKEZO/NJIA za kufuata baada ya ule mdororo wa uchumi(economic recession) wa 2008....ikaja kubainika kuwa MAKAMPUNI makubwa "yalimkamata kimshiko" AKASALITI KAMBI" na kutoa MWELEKEO aliyekuwa "ANAJUA VYEMA" kuwa UNAWANUFAISHA makampuni makubwa YALIYOCHANGIA yale matatizo....kwa hiyo AKALIINGIZA taifa lake "CHAKA" ......

#KaziIendelee
#JMTKwanza
 
Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
9,928
2,000
Utapata lila kitu lakini megawatt 2150 haziwezi kutimia. Inakadiriwa 36% ya maji yaliyokuwapo wakati wa upembuzi yakinifu wa awali yanni mwaka 1978 hayapo kutokana na sababu mbali mbali zikiwapo; miradi mbadala ya Mtera na Kihansi, shughuli za bonde la Ihefu, ongezeko la idadi na shughuli za binadamu na mabadiliko ya tabia nchi.

Hapo ni upotevu wa raslimali tu ulifanywa na Dikteta asiyeshaurika

64% ya 2150MW ni MW ngapi??

Better have something than nothing balonga bazungu.

Kumbuka wale wanasiasa wote waliosimama kidete kupinga huu mradi wanayo maslahi ya moja kwa moja auvya mbali kwenye visima vya gesi.--- walipinga kwa ajili ya matumbo yao.
 
rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,253
2,000
Ni UNESCO haohao walioanza kujiridhisha kipindi cha utawala wa hayati baba wa taifa mwalimu JKN kuwa ujenzi wa bwawa la kufua umeme kamwe HALITOATHIRI mazingira ya viumbe na uoto wa asili katika pori tengefu la SELOUS!!!

HAWAKUISHIA HAPO
*********************

Miaka kadhaa baadae chini ya utawala wa kipenzi chetu hayati Magufuli wakaendelea tena kujiridhisha kuwa UJENZI wa bwawa hilo halitoathiri BAIOANUAI ya eneo lile baada ya Tanzania kujieleza bayana kuwa ni 3% tu ya eneo hilo itakayomegwa kwa ajili ya kufua nishati ya umeme wa maji ambayo Wataalamu wa dunia walijiridhisha kwalo!

KIPI TENA KIMEBADILIKA
************************

Nchi yetu adhimu imeitwa katika mkutano utakaofanyika Fozhou nchini China kujitetea ili PORI TENGEFU la SELOUS lisiondolewe kutoka ALAMA ZA TURATHI ZA DUNIA!!!

KELELE KUTOKA NJE
*********************
Walianza wanaharakati wenye mrengo wa siasa za UPINZANI hususani CHADEMA kuukataa ujenzi wa bwawa hilo kwa sababu hizihizi tulizoitiwa huko China.

Baadaye likatokea kundi la wabunge wa CDU bungeni BUNDESTAG(ujerumani) kuupinga mpango wetu wa ujenzi huo.
Ikumbukwe chama cha CDU ndicho chama rafiki cha CHADEMA.

UMEFIKA MUDA
****************
Kama watanzania tuna dhima kubwa ya KULINDA ukweli ulioko na kuyalinda maslahi yetu ya taifa hili adhimu ili tuendelee na ujenzi wa BWAWA LA MWALIMU NYERERE na pia Pori la SELOUS lisiondolewe kutoka TURATHI ZA DUNIA.

Ninamtakia kila la heri Dr.Allan Kijazi na wataalam wetu wengine katika ushiriki wa huo mkutano mkubwa wa 44!

Je ni yepi mawazo yako ya KIZALENDO ?!!!

#KaziIendelee
#TaifaKwanza
#IdumuJMT
kama uzalendo ni kukatwa tozo za simu hakuna uzalendo
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,682
2,000
64% ya 2150MW ni MW ngapi??

Better have something than nothing balonga bazungu.

Kumbuka wale wanasiasa wote waliosimama kidete kupinga huu mradi wanayo maslahi ya moja kwa moja auvya mbali kwenye visima vya gesi.--- walipinga kwa ajili ya matumbo yao.
Sahihi kabisa.....

Maslahi maslahi maslahi ya baadhi ya wanasiasa Kaka ha ha ha 🀣
 
Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
7,182
2,000
Ndivyo ilivyo, watu wengi hawajui kwamba utawala wa kikoloni wa wajerumani wao ndio waliplani kujenga hilo bwawa, utawala wa kiingereza haukuwa na nia ya kufuata hiyo plan ya mjerumani kwasababu mbili, 1--- Mjerumani alikuwa hasimu yao, 2--- Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini wa Muingereza baada ya kukabidhiwa na UNO, tulipopata uhuru Nyerere akaufufua huo mpanga wa kujenga hilo Bwawa kama wenzake akina Gamel Abdul Nasser wa Misri (Aswan dam) na Kwame Nkrumah wa Ghana (Akosambo dam ??), nadhani tulishindwa kulijenga kutokana na gharama kubwa wakati huo au mikopo kutoka Banki ya dunia na IMF ilikuwa na masharti magumu sijui!!--- Mabeberu wa zama hizo walijua na bado wanajua kwamba ukombozi wetu MKUBWA wa kiuchumi ni nguvu za umeme hivyo wakatufanyia hila ya kupeleka propasal huko UNO ili kutangaza Selous iwe ni urithi wa dunia ili katika eneo hilo pasifanyike any 'development" kwa kisingizio kwamba eneo hilo ni urithi wa dunia kwa maana hiyo hukutakiwa kujenga hilo bwawa tena!!, unaona hila na ujanja wa mabeberu??!!--- kweli yapo maeneo yanafaa kupata hadhi ya urithi wa dunia lakini sio kwa Selous, walifanya hivyo tu ili Stieglier isijengwe.

Umeme ndiyo maendeleo, wao wenyewe maendeleo waliyonayo yameletwa na umeme, Usafii wa umeme, viwanda ni umeme, mahospitali, majumbani kupikia nk, ni umeme yaani kila kitu wao ni umeme tena mwingi wa bei rahisi sana kuliko sisi, sasa iweje kwetu umeme iwe ni haramu???--- kitu gani kiko nyuma ya sisi tusipate umeme mwingi rahisi wa uhakika???--- lengo wanataka waendelee kutunyonya sikuzote, tuendelee kukodi mitambo yao ya gesi nk, hui ndio unyonyaji wao.
Huu ujinga ndio watanzania wenye akili fupi mnapenda kulishwa.
Nani alikwambia mzungu anaumia sisi kuwa na bwawa kubwa la umeme?

Hadithi kama hizo tulizisikia pia wakati ule tunajenga bomba la gesi la Mtwara. Watawala hawa hawa wanaojenga sasa bwawa la umeme huko selous walituambia kupitia gesi ya Mtwara kuwa tungekuwa na utoshelevu wa umeme, tutanunua kwa bei nafuu (sawa na bure), tutauza umeme nje ya nchi, tutauziwa gesi ya majimbani kwa bei sawa na bure nk. Bomba la gesi kwa nguvu zote likajengwa, kiko wapi mpaka leo hii?
 
Ujinga wa muafrika ndio huo, akili yako inafikiri mambo ya siku moja ijayo wakati wenzako wanafikiri yajayo miaka 10--20!!.

Ulipoambiwa umeme ungekuwa sawa na bure ukadhani ni jambo la kufumba na kufumbua macho??--- maendeleo ni process na ukidanganywa leo usifikiri kesho utadanganywa, ya leo ni leo ya kesho ni kesho.
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,682
2,000
Ndivyo ilivyo, watu wengi hawajui kwamba utawala wa kikoloni wa wajerumani wao ndio waliplani kujenga hilo bwawa, utawala wa kiingereza haukuwa na nia ya kufuata hiyo plan ya mjerumani kwasababu mbili, 1--- Mjerumani alikuwa hasimu yao, 2--- Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini wa Muingereza baada ya kukabidhiwa na UNO, tulipopata uhuru Nyerere akaufufua huo mpanga wa kujenga hilo Bwawa kama wenzake akina Gamel Abdul Nasser wa Misri (Aswan dam) na Kwame Nkrumah wa Ghana (Akosambo dam ??), nadhani tulishindwa kulijenga kutokana na gharama kubwa wakati huo au mikopo kutoka Banki ya dunia na IMF ilikuwa na masharti magumu sijui!!--- Mabeberu wa zama hizo walijua na bado wanajua kwamba ukombozi wetu MKUBWA wa kiuchumi ni nguvu za umeme hivyo wakatufanyia hila ya kupeleka propasal huko UNO ili kutangaza Selous iwe ni urithi wa dunia ili katika eneo hilo pasifanyike any 'development" kwa kisingizio kwamba eneo hilo ni urithi wa dunia kwa maana hiyo hukutakiwa kujenga hilo bwawa tena!!, unaona hila na ujanja wa mabeberu??!!--- kweli yapo maeneo yanafaa kupata hadhi ya urithi wa dunia lakini sio kwa Selous, walifanya hivyo tu ili Stieglier isijengwe.

Umeme ndiyo maendeleo, wao wenyewe maendeleo waliyonayo yameletwa na umeme, Usafii wa umeme, viwanda ni umeme, mahospitali, majumbani kupikia nk, ni umeme yaani kila kitu wao ni umeme tena mwingi wa bei rahisi sana kuliko sisi, sasa iweje kwetu umeme iwe ni haramu???--- kitu gani kiko nyuma ya sisi tusipate umeme mwingi rahisi wa uhakika???--- lengo wanataka waendelee kutunyonya sikuzote, tuendelee kukodi mitambo yao ya gesi nk, hui ndio unyonyaji wao.
Daaah....

".....siku zote tuendelee kukodi mitambo yao ya gesi...."!!

#KaziIendelee
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
13,502
2,000
Umeandika vizuri ila umekosea huo mstari ulioandika "kipenzi chetu hayati Magufuli"

Naomba mtoa mada usituhusishe sote, aweza kuwa kipenzi chako lakini siyo kipenzi changu.

🀣🀣Ok mkuu wangu ha ha ha ila "CHETU" huanzia na "mbili"....katika hilo tuko:

1)Jumbe Brown
2)JohntheBaptist
3)Idugunde
4)Mkaruka et al🀣

Niongeze na mimi pamoja na mama D

Mmeamkaje watoto wa kipenzi cha Watanzania shujaa mbeba maono John Pombe Magufuli
πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
3,434
2,000
Mmeamkaje watoto wa kipenzi cha Watanzania shujaa mbeba maono John Pombe Magufuli
πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Wakati mwingine sisi Watanzania ni wapuuzi. JPM aliamua kuhakikisha anarudisha hela zilizokuwa zimechukuliwa na mafisadi na kuacha wanyonge wabaki na kidogo walichonacho. Miradi ikaenda kwa spidi ila Watu wakamlalamikia na kumuita majina ya ajabu. Sasa Samia kaingia na gia ya kutowabughudhi mafisadi, watu wakamshangilia, imagine!!!! Leo hii hakuna hela ya kuendesha serikali, akaona wanyonge wajipapase; kilio kama chote. JPM bwana, Mwenyezi Mungu amrehemu huko alipo. Inauma
 
kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
3,434
2,000
Kumekucha komrediπŸ’ͺ

Mbeba maono ametuachia mradi ADHIMU wa BWAWA LA MWALIMU NYERERE,cha ajabu UNESCO "wametubadilikia" 🀣🀣
Kwa siasa za sasa ambazo JK ndiye dereva, inawezekana wakausimamisha ili kutafuta sifa! Lakini 2025 sijui
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom