Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 5,255
- 7,920
Utapata lila kitu lakini megawatt 2150 haziwezi kutimia. Inakadiriwa 36% ya maji yaliyokuwapo wakati wa upembuzi yakinifu wa awali yanni mwaka 1978 hayapo kutokana na sababu mbali mbali zikiwapo; miradi mbadala ya Mtera na Kihansi, shughuli za bonde la Ihefu, ongezeko la idadi na shughuli za binadamu na mabadiliko ya tabia nchi.Ndivyo ilivyo, watu wengi hawajui kwamba utawala wa kikoloni wa wajerumani wao ndio waliplani kujenga hilo bwawa, utawala wa kiingereza haukuwa na nia ya kufuata hiyo plan ya mjerumani kwasababu mbili, 1--- Mjerumani alikuwa hasimu yao, 2--- Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini wa Muingereza baada ya kukabidhiwa na UNO, tulipopata uhuru Nyerere akaufufua huo mpanga wa kujenga hilo Bwawa kama wenzake akina Gamel Abdul Nasser wa Misri (Aswan dam) na Kwame Nkrumah wa Ghana (Akosambo dam ??), nadhani tulishindwa kulijenga kutokana na gharama kubwa wakati huo au mikopo kutoka Banki ya dunia na IMF ilikuwa na masharti magumu sijui!!--- Mabeberu wa zama hizo walijua na bado wanajua kwamba ukombozi wetu MKUBWA wa kiuchumi ni nguvu za umeme hivyo wakatufanyia hila ya kupeleka propasal huko UNO ili kutangaza Selous iwe ni urithi wa dunia ili katika eneo hilo pasifanyike any 'development" kwa kisingizio kwamba eneo hilo ni urithi wa dunia kwa maana hiyo hukutakiwa kujenga hilo bwawa tena!!, unaona hila na ujanja wa mabeberu??!!--- kweli yapo maeneo yanafaa kupata hadhi ya urithi wa dunia lakini sio kwa Selous, walifanya hivyo tu ili Stieglier isijengwe.
Umeme ndiyo maendeleo, wao wenyewe maendeleo waliyonayo yameletwa na umeme, Usafii wa umeme, viwanda ni umeme, mahospitali, majumbani kupikia nk, ni umeme yaani kila kitu wao ni umeme tena mwingi wa bei rahisi sana kuliko sisi, sasa iweje kwetu umeme iwe ni haramu???--- kitu gani kiko nyuma ya sisi tusipate umeme mwingi rahisi wa uhakika???--- lengo wanataka waendelee kutunyonya sikuzote, tuendelee kukodi mitambo yao ya gesi nk, hui ndio unyonyaji wao.
Hapo ni upotevu wa raslimali tu ulifanywa na Dikteta asiyeshaurika