Fozhou China, Mkutano mkuu wa 44 wa UNESCO July 16-31: Utetetezi wetu Watanzania juu ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,682
2,000
Ni UNESCO haohao walioanza kujiridhisha kipindi cha utawala wa hayati baba wa taifa mwalimu JKN kuwa ujenzi wa bwawa la kufua umeme kamwe HALITOATHIRI mazingira ya viumbe na uoto wa asili katika pori tengefu la SELOUS!!!

HAWAKUISHIA HAPO
Miaka kadhaa baadae chini ya utawala wa kipenzi chetu hayati Magufuli wakaendelea tena kujiridhisha kuwa UJENZI wa bwawa hilo halitoathiri BAIOANUAI ya eneo lile baada ya Tanzania kujieleza bayana kuwa ni 3% tu ya eneo hilo itakayomegwa kwa ajili ya kufua nishati ya umeme wa maji ambayo Wataalamu wa dunia walijiridhisha kwalo!

KIPI TENA KIMEBADILIKA
Nchi yetu adhimu imeitwa katika mkutano utakaofanyika Fozhou nchini China kujitetea ili PORI TENGEFU la SELOUS lisiondolewe kutoka ALAMA ZA TURATHI ZA DUNIA!!!

KELELE KUTOKA NJE
Walianza wanaharakati wenye mrengo wa siasa za UPINZANI hususani CHADEMA kuukataa ujenzi wa bwawa hilo kwa sababu hizihizi tulizoitiwa huko China.

Baadaye likatokea kundi la wabunge wa CDU bungeni BUNDESTAG(ujerumani) kuupinga mpango wetu wa ujenzi huo.
Ikumbukwe chama cha CDU ndicho chama rafiki cha CHADEMA.

UMEFIKA MUDA
Kama watanzania tuna dhima kubwa ya KULINDA ukweli ulioko na kuyalinda maslahi yetu ya taifa hili adhimu ili tuendelee na ujenzi wa BWAWA LA MWALIMU NYERERE na pia Pori la SELOUS lisiondolewe kutoka TURATHI ZA DUNIA.

Ninamtakia kila la heri Dr.Allan Kijazi na wataalam wetu wengine katika ushiriki wa huo mkutano mkubwa wa 44!

Je, ni yepi mawazo yako ya KIZALENDO ?!!!

#KaziIendelee
#TaifaKwanza
#IdumuJMT
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,470
2,000
Ni UNESCO haohao walioanza kujiridhisha kipindi cha utawala wa hayati baba wa taifa mwalimu JKN kuwa ujenzi wa bwawa la kufua umeme kamwe HALITOATHIRI mazingira ya viumbe na uoto wa asili katika pori tengefu la SELOUS!!!
Watu wa mazingira ndani ya NCHI yetu walikataa..!! Hii ikikaribia kumgharimu waziri
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,470
2,000
Watu gani hao wa mazingira walikataa?

Mbona wataalam wetu waliunga mkono baada ya kufahamu kuwa ni 3% ya ardhi ya Selous ndiyo inayomegwa kwa ujenzi huo!!
Ukiweka kwa percentage, na huku hujaweka ukubwa wa solo yote hutendi haki.. Sema hekali 1000 zimechukuliwa na PROJECT hiyo kwa utafiti uliofanyika miaka ya 1970 huko... Hakukuwa na utafiti muda mfupi ULIOPITA...

HAPA WALIO WENGI WALIKUBALI PROJECT HIYO KWA KUMUHOFIA MTU MMOJA TU.. MWENDAZAKE..!!! Maana ilikuwa ukienda kinyume naye lazima uliwe kichwa.. Ilikuwa chupuchupu Makamba aliwe kichwa
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,682
2,000
Ukiweka kwa percentage, na huku hujaweka ukubwa wa solo yote hutendi haki.. Sema hekali 1000 zimechukuliwa na PROJECT hiyo kwa utafiti uliofanyika miaka ya 1970 huko... Hakukuwa na utafiti muda mfupi ULIOPITA... HAPA WALIO WENGI WALIKUBALI PROJECT HIYO KWA KUMUHOFIA MTU MMOJA TU.. MWENDAZAKE..!!! Maana ilikuwa ukienda kinyume naye lazima uliwe kichwa.. Ilikuwa chupuchupu Makamba aliwe kichwa
Sawa mkuu....

Nami nitendee haki, katika hizo hekari 1000 unazosema ,Selous imebakiwa na hekari kiasi gani ?!
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,682
2,000
Kutumia 3% ya ardhi yetu na kuacha 97% ya hiyo ardhi kwa ajili ya dunia na sisi wenyewe hapo kuna kosa gani??
Hakuna kosa....

Ndipo hapo tunapoishangaa UNESCO...


Yaani inashangaza....

Katika hili HUTOIONA CHADEMA Wala mh.MBOWE kuliongelea 🤣🤣
 

DENLSON

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
648
1,000
Lakini hata ikiondolew kwenye maajabu ya dunia nini tatizo? Sisi ni dona kantri au nasema uongo ndugu zangu. Hii nchi ni tajiri kweli kweli na tunaleta ndege nyingine kwa cash pesa ipo.
 

Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
2,764
2,000
Ukiweka kwa percentage, na huku hujaweka ukubwa wa solo yote hutendi haki.. Sema hekali 1000 zimechukuliwa na PROJECT hiyo kwa utafiti uliofanyika miaka ya 1970 huko... Hakukuwa na utafiti muda mfupi ULIOPITA... HAPA WALIO WENGI WALIKUBALI PROJECT HIYO KWA KUMUHOFIA MTU MMOJA TU.. MWENDAZAKE..!!! Maana ilikuwa ukienda kinyume naye lazima uliwe kichwa.. Ilikuwa chupuchupu Makamba aliwe kichwa
Hapo umenena. Mendazake alikuwa tishio kwa kuviringisha - "rolling heads".
 

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
11,910
2,000
Mawazo ya Kizalendo?

Jesus!

Uzalendo na nani?

Uzalendo wangu mwenyewe kwangu mimi binafsi,government has no rights over the rights of individual citizens as independent peoples!

Kizalendo towards who?

Acheni bonde likae,mimea na wanyama waishi kama lilvyo..jengeni umeme wa gas ipo!

Acheni kuharibu uoto mavi nyie

Blah blah blah..uzalendo this uzalendo that,nonsense!
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,682
2,000
Mawazo ya Kizalendo?

Jesus!

Uzalendo na nani?..
Neno uzalendo linafundishwa hadi majeshini.

Hope huko Amerika uliko hakuna JESHI LA NCHI.

Ama labda mafunzo yao katika kuilinda nchi ni tofauti na kwengine.

Mkuu wewe baki na uzalendo wa NAFSI YAKO.

Uzalendo wangu unahusisha na kulipa Kodi kiwajibu nchini Tanzania ambako nchi jirani ya Kenya SIHUSIKI NA WALA SIWAJIBIKI nako.

Bwawa la umeme la MWALIMU NYERERE linahusu jasho la Kodi yangu....wewe uko huko Marekani, halikuhusu.
 

tathmini

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
311
250
Kutumia 3% ya ardhi yetu na kuacha 97% ya hiyo ardhi kwa ajili ya dunia na sisi wenyewe hapo kuna kosa gani??
Unataka tujadili huku ukiuita msimamo wako ndio wa kizalendo. Tukihitilafiana na wewe bado tutakuwa wazalendo kwako? Pili, hivi UNESCO wamekataza bwawa au wanataka tujieleze kwa nini sehemu hiyo ibaki kuitwa urathi wa Dunia? Hatutaki kuulizwa kuhusu jambo ambalo UNESCO ina usemi nalo?
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,723
2,000
Kutumia 3% ya ardhi yetu na kuacha 97% ya hiyo ardhi kwa ajili ya dunia na sisi wenyewe hapo kuna kosa gani??

Inategemea hiyo 3% ina umuhimu / unyeti gani ktk hifadhi nzima ya Selous.

Kwa mfano, moyo wa binadamu ni mdogo kuliko mguu.

Lakini sote tunaelewa kwamba pamoja na udogo wake, moyo ni muhimu kwa mwili wa binadamu kuliko mguu.

Mradi wa bwawa la umeme una ATHARI za kimazingira na itatubidi tujipange zisiwe na madhara makubwa.

Hoja yetu iwe kwamba tunao uwezo wa kupambana na athari za mradi.

Hoja nyingine iwe mradi una faida kwetu na faida hizo ni kubwa na zitatuwezesha kukabiliana na athari za kimazingira.

Lingine tunaloweza kufanya ni kueleza hatua za ziada na mbadala tutakazochukua kuendeleza uhifadhi wa mazingira ya Selous.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom