Mkuu nashukuru sana kwa ufafanuzi wako. Hata hivyo kwa kuwa umetoa nafasi ya kujazia sehemu ambayo labda inamabadiliko yafuatie,nafikiri nijikite kwenye mambo mawili
1:Mkuu kwa ufahamu wangu,hairuhusiwi tena mtu kuendelea na 4m 5 na wakati huohuo akiwa anarisit. Hii ni kwasababu ili ufanye mtihani wa kidato cha sita lazima uwe umekaa darasani miaka miwili toka umalize kidato cha nne,hivyo basi ukijiunga na 4m 5 huku unarisit hiyo miaka miwili haitatimia.
2:Hairuhusiwi tena kuunga unga vyeti,mfano mtu alikuwa na c mbili then arisit ili apate moja aunganishe na zile mbili za mwanzo,swala hilo haliwezekani tena. Hii ni kwa sababu ili mtahiniwa aruhusiwe kufanya mtihani kidato cha sita lazima awe amepata angalau crediti 3 O-level kutoka kwenye kikao kimoja ( ie 3 credits in o-level at the same sitting). Hii inamaanisha mtu akiamua kurisit anayakana matokeo yake na anatafuta mengine,na kwa mfano kama mtu alikuwa na c mbili na zilizobaki ni D halafu akarist assume akapata tena C mbili na D nne labda na F moja,hawezi kuanga hayo matokea akadai eti ana C nne kwasababu zimepatikana kwenye vikao tofauti(miaka tofauti). Hata hivyo lazima nikiri kwamba taratibu za kuunga vyeti zilikuwa zinatumika hapo nyuma lakini kwa ufahamu wangu ni kwamba kwa sasa zimefutwa. Kwahiyo kama mtu ana C mbli hawezi kwenda form 5, na akiamua kurisit ajue ni kama anaanza kazi upia. So kama kuna mtu hali hii inamgusa aangalie hayo mambo.