Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.
tapatalk_1498207593799.png

WAKUU VP APO NAONA KAMA DEMO NAIPATIA
 
Pigeni shule mazee telegram mambo yanakwenda atari watu zaidi ya 5 wameshaanza na live account.

Akili ni kitu cha ajabu sana ukitaka kufika mbali usisikilize kelele za wapita njia Be focused. Wanaokatisha tamaa ni kuwaacha bila ya kuwajibu kwakuwa kuwajibu ni kupotezeana muda na hawako kuelewa Bali kulazimisha kueleweka.

Vitabu ni muhimu sana na ukiijua forex vizuri hutojutia. Hii ni darasa huru kuingia na kutoka ni uamuzi wako, hii biashara haina uchawi faida yako inatokana na maarifa uliyonayo ukiwa shallow utaambulia hasara na kuishia kulalama.
 
L
Ivi kumbe unaweza kutrade pair hiyo hiyo moja kwa position nyingi?

Halafu bado ishu ya volume ni mtihan kwangu

Mkuu@bavaria msaada pls

Kabisa Mkuu inategemea na deposit yako....nilipoanza demo nilikuwa natrade kama anonymous kwa hyo ile 100,000 nikawa naweka mpaka position mia kwa pair moja...siku ya kwanza tu nikapiga USD 34,000...nikaclose halafu nikaingia tena kwa pair ya XAUUSD...hyo ilikuwa usiku sikuweka ST wala TP...nikapitiwa na usingizi...kuja kustuka nikakuta nina profit ya usd 6k+....Sijui nyingine ziliyeyukia Wapi...
 
Wakuu leo nimekutana na hii challenge!!

Palikua na event moja huko ujerumani... Na katika forecast zao...na hasa katika actual result wali comment kwamba EURO itapanda (bullish)...embu soma hii picha...
a37314ec609419befc1eca7296ac31e9.jpg

Cheki na hii...
f0d6a7249696bbc39ef2e43c2155ffd7.jpg

Lakini katika actual market EURO imeshuka sana...yaani EURUSD imekua so bearish!!

Maana kwenye hiyo pic actual value ni kubwa kuliko expected/forecast, ilitakiwa iwe bullish sasa nashangaa imekua bearish!!

Je ni mimi niliielewa vibaya hii "news"???

ONTARIO Bavaria na traders wengine wote!!!

Mkuu katika kusoma kwangu hicho ni kitu cha kawaida.. Iko hivi hapo hiyo news ni FUNDAMENTAL ANALYSIS na kuna wakati market inarespond vile event inataka lkn pia kuna wakati market inaweza ignore hiyo event. So wanasema kabla ya kufanya maamuzi ni vizuri pia ukaangalia TECHNICAL ANALYSIS ambazo nadhani unajua jinsi ya kuzicheki.

Hayo ni maoni yangu sijui kama nimeelewa sawa.
 
Habari.

Wakati mwingine News zinaweza zisilete impact kiasi kile ambacho watu wanafikiria.
Inategemea na jinsi Institutional Investors wanavyodigest hiyo news na kwamba wanaipa kipaumbele au la.
Binafsi, sijaona kama hiyo news ina uzito sana kiasi cha kuipa attention. Kwahiyo, nimeona bora ibaki na trend kama ilivyo.
Kingine, Euro ni official currency ya nchi nyingi za Ulaya. Kwahiyo, news ya Germany inaweza isilete uzito kama dola inavyokuwa.
Collective decisions mfano, interest rate anazotoa Draghi ndo huwa zinatikisa Euro. Ila kwa Germany bado sana.
Sababu kubwa inaweza kuwa;
-Institutional Investors hawajaona umuhimu wa hiyo news.
-Germany ni single entity kwenye matumizi ya Euro. So haiwezi kupush price juu wala chini..
 
Ivi kumbe unaweza kutrade pair hiyo hiyo moja kwa position nyingi?

Halafu bado ishu ya volume ni mtihan kwangu

Mkuu@bavaria msaada pls
Inawezekana. Ni strategy tu ya kumaximize profit kwenye trade zako.
Ukiwa na position moja inayokuletea profit ya 90$ itakufanya ufungue position zaidi hata ya 10 ili uweze kupata faida zaidi ya hiyo.
Pia, kuna kiasi fulani cha capital hakikuruhusu kuwa na lot kubwa. Wengi wanachofanya, wanafungua position nyingi kwa lot ndogondogo kumaximize faida.
 
Mkuu katika kusoma kwangu hicho ni kitu cha kawaida.. Iko hivi hapo hiyo news ni FUNDAMENTAL ANALYSIS na kuna wakati market inarespond vile event inataka lkn pia kuna wakati market inaweza ignore hiyo event. So wanasema kabla ya kufanya maamuzi ni vizuri pia ukaangalia TECHNICAL ANALYSIS ambazo nadhani unajua jinsi ya kuzicheki.

Hayo ni maoni yangu sijui kama nimeelewa sawa.
Uko sahihi kabisa mkuu, ila hata wao wana classify kama medium, low, high!! event yoyote yenye high influence mara nyingi lazima itokee!!! Ila niekubaliana na wewe yoyte kwa yote inategemea na soko!!

Kama nusu saa iliyopita kulikua na event huko marekani naona dola ya USA imechezea za kichwa kweli kweli!!!
 
Duuu...hapo labda wakongwe watusaidie Mkuu.

Ila kama una trade live hii pair ya EUR/GBP naona imekaa poa sana....naona double bottoms na double tops zinapigana vikumbo.

Ukiwa mtu wa kuingia na kutoka unaweza piga mkwanja mrefu sana...mm nimekomaa nayo kwenye demo mpaka sasa Nina mshahara kama wa wabunge wawili wa TZ..

Sijui kama nipo sahihi lakn...mm bado mchanga...wakuu ONTARIO au Bavaria wanaweza kutia neno
Kuna pairs zina liquidity nzuri tu. Ukizikomalia zinakupeleka mbali.
Kuna traders duniani nawafahamu, wanatrade pair moja au mbili tu. Hawajishughulishi na pair nyingine yeyote.
Nna rafiki yangu anatrade EURUSD na GBPJPY.
Toka mwaka huu uanze hajawahi kugusa pair zaidi ya hizo mbili. Na hana mpango wa kuhangaika nazo na anazifahamu haswa hizo pairs.
Anaweza fungua position zaidi ya 200 kwa lot ya 0.10 kwa pair hizo mbili na akatoka na mpunga wake wa kutosha.
 
Habari.

Wakati mwingine News zinaweza zisilete impact kiasi kile ambacho watu wanafikiria.
Inategemea na jinsi Institutional Investors wanavyodigest hiyo news na kwamba wanaipa kipaumbele au la.
Binafsi, sijaona kama hiyo news ina uzito sana kiasi cha kuipa attention. Kwahiyo, nimeona bora ibaki na trend kama ilivyo.
Kingine, Euro ni official currency ya nchi nyingi za Ulaya. Kwahiyo, news ya Germany inaweza isilete uzito kama dola inavyokuwa.
Collective decisions mfano, interest rate anazotoa Draghi ndo huwa zinatikisa Euro. Ila kwa Germany bado sana.
Sababu kubwa inaweza kuwa;
-Institutional Investors hawajaona umuhimu wa hiyo news.
-Germany ni single entity kwenye matumizi ya Euro. So haiwezi kupush price juu wala chini..
Nashukuru sana mkuu!!! Uko sahihi!!

Niko nangoja hii event ya EUR ECB Youth Dialogue With Mario Draghi in Lisbon. After an hour nadhani itakua hewani!!
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Wazo la nne
Si hata wazo la msingi sana, hahaa. Sijui niandike nini, lkn nachotaka kumaanisha ni usiwe mchoyo, kama kuna rafiki yako wa faida unahisi inabidi aone huu uzi usisite kumtag.

Ni bora tukaepuka kuQuote huu uzi, ni mrefu sana sana, yani ukiquote unatusumbua sana ambao tunatumia simu na gadgets zingine ndogo ndogo.

Karibuni kwaaliji ya ku discuss.

Updates

Moja ya ombi la msingi ambalo nimeona watu wengi wanaulizia ni - "Ontario ni kitabu gani naweza kuanza nacho?"

Kila mtu ambae yupo interested atafute kitabu kinaitwa Currency trading for Dummies: Kimeandikwa na Brian Dolan 2nd Ed ndio poa zaidi. Cover yake ni kama changano then kuna dunia hivi inaramani za nchi mbali mbali.

shukurani sana kaka kwa elimu hii pana umenifungua
 
Uko sahihi kabisa mkuu, ila hata wao wana classify kama medium, low, high!! event yoyote yenye high influence mara nyingi lazima itokee!!! Ila niekubaliana na wewe yoyte kwa yote inategemea na soko!!

Kama nusu saa iliyopita kulikua na event huko marekani naona dola ya USA imechezea za kichwa kweli kweli!!!
Sawa kabisa mkuu Loddy.
 
Kuna pairs zina liquidity nzuri tu. Ukizikomalia zinakupeleka mbali.
Kuna traders duniani nawafahamu, wanatrade pair moja au mbili tu. Hawajishughulishi na pair nyingine yeyote.
Nna rafiki yangu anatrade EURUSD na GBPJPY.
Toka mwaka huu uanze hajawahi kugusa pair zaidi ya hizo mbili. Na hana mpango wa kuhangaika nazo.
Anaweza fungua position zaidi ya 200 kwa lot ya 0.10 kwa pair hizo mbili na akatoka na mpunga wake wa kutosha.
tena inakuwa very simple kufanya analysis zako ukispecialise kwa pair mbili au tatu kinyume na trader anaye trade pair nyingi hivyo kuongeza chances zako za kupata positive results
 
KK VP, NAJARIBU KUSET IZ ORDER HASA IZI OCO, IF/THEN, STOP LOOSE, TP LAKINI BADO NI CHANGAMOTO. NAOMBA SUPPORT TAFADHAL, [HASHTAG]#ontario[/HASHTAG]
 
Ushauri kwa ambao tunatumia demo accounts na ambao tunataka kuanza kutumia real/live account lakini tunakwama kwa kukosa uwezo!!

Habari wadau!!!

Leo nimeona si mbaya kama tukapeana hints ambazo kwa namna moja au nyingine zitatusaidia kutujenga hasa katika nyanja ya forex kwa ujumla wake!!

Kwanza ni lazima tufahamu demo account zina umuhimu mkubwa sana katika ku-implement kile ambacho tumejifunza kwa nadharia! Pia demo account ni kama test ya kutupima yale tuliyojifunza katika vitabu na videos!!

Lakini kwa mtazamo wangu (narudia tena, mtazamo wangu) demo account hazitupi uhalisia wa soko lilivyo, mind you sisemi kwamba ni mbaya la hasha ni nzuri tena sana tu!! Ila ni vyema tunapoanza kutumia demo account kuhakikisha kiasi tunacho-set kama capital kiwe kidogo chini na kiwe kina akisi uhalisia!!

Kufanya mazoezi kwa ktumia account yenye 1,000,000 USD si kwamba ni vibaya, ila haikupi uhalisia wa mambo yalivyo katika live account hasa kwa sisi tunaoanza (labda kama unataka kuanza kutrade kwa kutumia 1million dollas)!!!

Now what to do??

Hapa nna mawazo mawili ambayo nna uhakika unaweza yatumia yote au moja wapo!!

1. Wakati wa kufungua demo account ni vyema kuhakikisha tunaset amount iwe chini sio kuanza na demo yenye 1mil dola!!

2.Kufungua real account!!

Sasa hapa kwenye real account naomba nifafanue zaidi!!!

Kama tunavyojua kuna brokers wengi na kila broker ana sifa zake!! Naamini kama unapitia vitabu utakua ushaona au umejifunza aina ya brokers!!

Ni vyema pia ukajua kwamba ku trade na real account kwa baadhi ya brokers sio lazima uwe na cash, yaani sio lazima u-deposit pesa ndio uanze ku trade!!! Kuna brokers ambao wanatoa kitu kama bonus ambayo inakuwezesha wewe kama trader kuitumia katika ku trade (live na sio demo)!!

Mfano kulingana na ushindani wa soko, kuna brokers wanatoa bonus ya dola 30 wengine mpaka dola 100 (huwezi withdraw hii bonus)!! sasa unaweza tumia hii bonus katika ku trade nayo kabla hujaweka pesa (hasa kwa wale wenzangu ambao kiasi flani tunakwama kufungua live account kwa kukosa uwezo)!!! Trust me, hii itakupa nguvu sana hasa pale utapotaka kuweka pesa yako na kuanza ku trade!!!

Uzuri wa bonus ni kwamba unapewa free (kwa baadhi ya brokers) ukifungua live account na unaweza trade nayo ukapata faida pia ambayo utaku-boost ukija kuweka cash!!

My advice to you guys!!!

1. Anza na demo account ukiiweza hamia kwenye live account yenye bonus!! Sio lazima utumie bonus, pia unaweza kuweka kiasi kidogo cha pesa ukaanza nacho maana kuna brokers wana kubali kudeposit minimum amount kuanzia dola 5 wengine mpaka dola moja!

2. Na kama unataka kuanza kutrade live account, may be kidogo mambo hayako sawa au umetumia demo account mda mrefu na unataka challenges za live trading bila risk kubwa...to me, this is the best way!! Fungua live account then apply bonus then anza kutrade, sio ungoje uanze ku-trade ukipata pesa!!!

Belive me, ukiweza kuizungusha bonus account bila kuichoma (and even if ikitokea umeichoma maana sometimes inatokea), utakua umepiga bonge la hatuaaa!! na zaidi ya yote utakua umepata experience/uzoefu wa utamu na uchungu wa forex ambao kwenye demo pekee huwezi kuupata!!

Tutumie demo accounts, ikiwezekana tuset amount ndogo, ukiizoea demo na kama huna uwezo kifedha kutrade kwenye live, usisubiri mpaka uwe na uwezo! unaweza fungua live account kwa broker yeyote anayetoa bonus, then ukaitumia hiyo bonus kutrade mpaka hapo utapokua na uwezo au utapoona umeridhika kuweka pesa yako!!!

Tuendelee kujifunza, NAIMANI tutajifunza mengi zaidi ONTARIO akiweka mambo yake sawa!!

Wako katika kujifunza,

Lodrick Thomas (Eng.)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom