Forbes yatangaza watu 10 wenye ushawishi zaidi Duniani

Mark Zuckerberg yupo kwenye the most influential Business People in the World tokea mwaka 2015, humu tunaangalia watu ambao kauli zao moja kwa moja na matendo yao yanaweza kuathiri mwelekeo wa maisha yetu. Hivi leo Zuckerberg akisumbua na Facebook yake ndiyo tutaikumbuka lakini siyo FATAL sana, lakini Mfalme Salman akisumbua na mafuta yake hadi wewe na mimi tunaweza tusiende kazini kwasababu ya uhaba wa mafuta na mfumuko wa bei.
If that's the case imekuaje Amazon imeingia kwenye top 10 ina maana amazon ina nguvu kuliko facebook !! Why bezos na sio zuckeberg
 
Unajua sio kila wanachosema hawa jamaa kina ukweli. Inategemea wanalengo gani na huo utafiti wao umejikita kwa watu gani.

Huwezi kusema ushawishi duniani wakati kuna watu hata hawamfahamu huyo rais wa China au US. Inamaana Burundi au Rwanda na Uganda napo wana ushawishi? Ushawishi wa nchi moja au kundi la watu unafanya uwakilishe dunia nzima?

Ndio haya mambo Nyerere alisema jambo la kijinga likisemwa kiingereza au na mzungu linaonekana la maana.
unaposema watu kibao hawamfahamu xi unamaanisha nn? maana wachina ndo wapo kibao duniani kuliko taifa lolote lile
 
Mrusi ndiyo nchi ya kwanza kuwa na rasilimali nyingi duniani ambazo zina thamani ya Dola za Kimarekani Trillioni 75.
Marekani akiwa nchi ya pili kwa wingi wa rasilimali duniani ambazo zina thamani ya Dola za Kimarekani Trillioni 45.
Nadhani kwenye uchumi utakuwa ushajua kwamba nini hutokea kwa nchi yenye rasilimali nyingi pamoja na idadi kubwa ya watu wenye ujuzi wa kuzalisha.

Mwaka jana Umoja wa Ulaya umeitaja Urusi kama moja ya mshirika wao mkubwa biashara, takwimu zinaonyesha ni wa nne baada ya Marekani, Uchina na Uswisi. Jinsi umoja wa Ulaya ulivyo mkubwa nadhani utakuwa ushafahamu hapa kuna ushawishi mkubwa sana kimasoko.

Uchumi wa dunia unaendeshwa na viwanda na viwanda vinahitaji nishati kubwa, nchi za Ulaya na Mashariki ya mbali zina tatizo la nishati. Hasa hasa nchi kama India na Uchina, bahati mbaya sana wanahitaji gesi na mikataba hiyo ya kupeleka gesi amesaini Bwana Vladmir Putin. Unapoongelea GIANT ENERGY CORPORATIONS hapa duniani utataja Exxon Mobil, BP, Chevron, Royal Dutch Shell bila kusahau makampuni makubwa ya Urusi kama Gazprom, Rosneft na Lukoil. Sasa wote tunajua kamba jinsi ambavyo nishati inaweza kutumika kama rungu la kidiplomasia hata na nchi ndogo. Ushahidi wa hili Juzi Uchina kalalamika kwamba Saudi Arabia anapandisha bei za mafuta bila mpangilio. Upande wa pili kinachoendelea Mashariki ya kati sasa hivi baina ya Israel na Iran yote ni kwasababu ya mafuta na inakuwa ngumu sana kumsumbua Iran kwasababu anatumia vizuri sana rungu lake la kidiplomasia la Mafuta.

Kama wewe umefuatilia vizuri kuhusu Historia ya Marekani, utakumbuka Oil Crisis ya mwaka 1973 baada ya Yom Kippur War. Ambapo Marekani na Ujanja wake wote ule aliwekewa vikwazo na nchi za Uarabuni kwa kunyimwa mafuta kwasababu aliwaunga mkono Waisraeli dhidi ya waarabu. Matokeo yalikuwa mabaya sana kwasababu bei za mafuta zilipanda na Wamerekani walikuwa wanapanga foleni kama Nigeria kwenye kununua mafuta. Bahati mbaya sana alikuwa anapigana vita kule nchini Vietnman hivyo alichanganyikiwa: Henry Kissinger alikuwa hadi anafikiria kuvamia mashariki ya kati lakini, wakatoa vitisho lakini Waarabu hawakujali kwasababu walijua kabisa ikianza vita Makampuni ya Marekani na Muingereza yangeumia zaidi na lingekuwa bonge la dili kwa Warusi.

Sasa hawa Waarabu walikuwa wanauza tu mafuta bila kuwa na Makampuni makubwa, jiulize ushawishi wa Vladmir Putin mwenye gesi nyingi na mafuta pamoja na makampuni makubwa kama Gazprom, Lukoil, Rosneft na Tafneft atakuwa na ushawishi mkubwa kiasi gani ??? Waziri Mkuu wa Ujerumani tokea mwaka 1998-2005 Bwana Gerhard Schroeder ameajiriwa na Bwana Vladmir Vladmirovich Putin kuwa mwenyekiti wa kampuni la nishati la Urusi (Government Corporation) liitwalo Rosneft: Huu ndiyo ushawishi wa gesi na mafuta bwana, Ulaya na kiburi cha watakimbia lakini mwishoni watarudi tu.

Marekani na Umoja wa Ulaya wanashindwa kufanya chochote kule nchini Ukraine, wewe unahisi kwanini ???
GESI YA MRUSI, GESI YA MRUSI !!! Ukraine na ujehuri wake wote ule anategemea gesi asilia kutoka Urusi na bila gesi asilia hawezi kuishi. Hivyo mwaka huu ikabidi tu aende akasaini mkataba na Gazprom na Urusi akasema kuna majimbo atayapa gesi bure kama msaada wa kibinadamu.

NB: Hapa hatujaongelea Uuzaji wa teknolojia ya silaha ambazo nchi nyingi hupenda kununua kwasababu ya bei ndogo.
Haya ni machache kwenye ushawishi wa Bwana Vladmir Putin, anacheza karata zake vizuri sana hadi Ulaya, Uchina na India hawawezi kuishi kirahisi bila kutegemea mikataba ya nishati kutoka kwake.
Duh hii nondo ni hatari.
 
Kiongozi wa China Xi Jinping ndiye mtu mwenye ushawishi Zaidi duniani, kwa mujibu wa jarida la Forbes. Amechukua nafasi hiyo baada ya bunge China kumpa mamlaka zaidi na kuondoa kikomo cha muhula wa rais.

Jingping amechukua nafasi hiyo kutoka kwa Rais Vladimir Putin wa Urusi ambaye kwa sasa anashika nafasi ya pili.

World Most [HASHTAG]#PowerfulPeople[/HASHTAG] List of forbes [HASHTAG]#forbes[/HASHTAG]

1. Xi Jinping
2. Vladimir Putin
3. @realDonaldTrump
4. Angela Merkel
5 @JeffBezos amazon
6. Pope Francis
7. @BillGates
8. Mohammed bin Salman Al Saud
9. @narendramodi
10. Larry Page GOOGLE
Hawa jamaa wanazingua, kiduku anakosaje ??
 
Rais Wetu hajachaguliwa?
 
Ushaanza kuzingua.....
Hahahaa!! mkuu ni kweli umemamaliza kwenye hoja zako. ila kwa kuongezea naona Merkel yupo hapo sababu ya Umoja wa Ulaya maana Ukiongea EU kwa sehemu kubwa unaongelea Germany. Ila naona Trump kuwa nafasi ya tatu kunatokana sana na jinsi bunge linavyowabana marais wa Marekani. China na Urusi kikwazo kama hicho kwa Rais ni kidogo.
 
Hivi Putin huwa ana shawishi nini na anawasahawishi kina nan?
Ana ushawishi hata kwa Marekani pia na ndio maana Wamarekani waligawanyika kumjadili kipindi cha uchaguzi lakini pia kunapotokea sintofahamu kuhusu amani ya dunia, Putin kama kiongozi wa Russia anakuwa sehemu muhimu ya kushirikishwa pamoja na kwamba ni mara chache wakakubaliana na Marekani
 
asilimia 70 ya waliopo kwenye list hii wanaweza kuwepo kwe list ya miaka mitano ijayo
 
If that's the case imekuaje Amazon imeingia kwenye top 10 ina maana amazon ina nguvu kuliko facebook !! Why bezos na sio zuckeberg

Mkuu mpaka sasa hivi,
Amazon ndiyo The Second Most Valuable Brand in the world only next to Apple.
Tukija kwenye Networth zao binafsi Bezos ni two folds ile ya Zuckerberg ambapo ana 132 Billions USD wakati Zuckerberg ana 70 Billions USD. Hawa watu watalinganaje mkuu wangu ???
 
Unajua sio kila wanachosema hawa jamaa kina ukweli. Inategemea wanalengo gani na huo utafiti wao umejikita kwa watu gani.

Huwezi kusema ushawishi duniani wakati kuna watu hata hawamfahamu huyo rais wa China au US. Inamaana Burundi au Rwanda na Uganda napo wana ushawishi? Ushawishi wa nchi moja au kundi la watu unafanya uwakilishe dunia nzima?

Ndio haya mambo Nyerere alisema jambo la kijinga likisemwa kiingereza au na mzungu linaonekana la maana.
Nimependa hapo bold ...by the way nimeangalia hiyo namba 1 mpaka 4 nimeona wameingia kwa sababu ya mambo yao mbofumbofu ya vita na amani ya dunia sidhani kama kuna kingine maana wote hao wanne ni wajumbe wa kudumu wa UN Security Council
 
unaposema watu kibao hawamfahamu xi unamaanisha nn? maana wachina ndo wapo kibao duniani kuliko taifa lolote lile

Mkuu unaelewa nini unapoambiwa ushawishi duniani? Kiongozi au mtu anaweza kuwa na ushawishi au uungwaji mkono kwenye eneo flan, haimaanishi ana ushawishi duniani.
 
Mkuu mpaka sasa hivi,
Amazon ndiyo The Second Most Valuable Brand in the world only next to Apple.
Tukija kwenye Networth zao binafsi Bezos ni two folds ile ya Zuckerberg ambapo ana 132 Billions USD wakati Zuckerberg ana 70 Billions USD. Hawa watu watalinganaje mkuu wangu ???
Kwa takwimu hizo sina kipingamizi tena..... Dah nlikuwa naichukulia Amazon poa sana kumbe iko mbali hivo statistically

Thanks mkuu kwa clarification zako
 
Back
Top Bottom