FORBES: Rais Magufuli ni ‘Rais Mwanamageuzi’

Haina haja ya utafiti, elewa tu Mimi na familia yangu hatumtaki....wewe na wengine endeleeni kumtaka ..ni Haki yenu na hata wapinzani wasipoingia Bungeni 2020...nasisitiza Mimi na familia yangu Hatumtaki...ni hivyo tu...
Ktk familia yako si kila mmoja ananafsi yake na mawazo yake? Umepata wapi mamlaka yakuwachagulia wengine au kufikiri kwa niaba yao? Hueshimu ktk demokrasia?
 
Umechangia hoja kisomi hasa.
Safi sana
Inatia moyo sana kuona kwamba sasa na sisi tunao watu wa aina yake. Watu wasiokubali kulishwa matango tu bila ya kuhoji ni matango ya aina gani...'matango pori' au yaliyolimwa shambani.

Jambo mhimu tunalopaswa kulitambua sasa ni kwamba Kampeni za 2020 zimekwishaanza, hata kama hazijatangazwa rasmi.

CCM tayari wamekwishawapata "Cambridge Analytica" wa kwao wamo kazini tayari. Tuyategemee mengi.
 
FORBES wanasema Rais Magufuli ni ‘Rais Mwanamageuzi, mleta maendeleo’, ndani ya story hiyo wanaeleza mafanikio kedekede ya serikali yake
LOooh, angalia 'panel' ya sponsors hao!
'Penresa' ndio 'Cambridge Analytica' yetu? Kampeni zishashika moto hizo hata kabla ya kipenga?
 
Miaka mitano ya kifunga mikanda inaisha..20/25 Baba asipoonesha neema japo nami nipate mkate kwa jasho la elimu yangu japo ndogo hakika nawambia nitapata tabu sana kuelewa uhusiano wa katiba ya CCM na ilani na watu walio Serikalini.Si vyema kama tutateseka 20-25 tunahitaji kuona mavuno ya uwekezaji wa 15-20..
 
LOooh, angalia 'panel' ya sponsors hao!
'Penresa' ndio 'Cambridge Analytica' yetu?
mkuu nimependa jinsi watu walivyofunguka sana juu ya hili suala hapa, na kuwafungua macho wengine?
Naendelea kuungana na Kaka yetu Pascal Mayalla kwamba ili mtu ujue wengine wana mawazo gani juu ya kinachosemwa ni bora ukaleta hoja bila kuonesha upande ilihali unajua ukweli wa jamno, hii inasaidia kuongeza ujuzi juu ya uloleta na inaongeza maarifa kutokana na michango mbali mbali wanayoleta, na hapo hapo unapima mtazamo wao kama unaendana na wa kwako

Britanicca
 
Semeni yote, Magufuli ndie rais ambaye hata ukimuangalia usoni unaona kabisa ana uchungu na nchi hii, ndani ya miaka minne elimu bure, Atcl imefufuka, sgr, stiglers gorge, project hizi zikikamilika zitaleta uwiano mzuri kwenye kukuza uchumi.
Ni lazima watu wajifunze kukaza mkanda
 
Mkuu nimecheka sana, mtu anahonga wanawake dar alafu anamsahau bibi yake kijijini, lawama apewe magufuli... sijui wanatumia nini kufikiria
Hao bibi zenu vijijini kama huwa hamuendi kuwasaidia magufuli ndio atawasaidia kila kitu?.
1.Haujui kuwa wanatibiwa bure?
2. Huoni ulinzi wao dhidi ya wauaji kwa imani za kishirikina umepungua sana
3. Huoni kuwa ninyi mliowatelekezea bila msaada Magufuli kaamua kuwasomesheeni watoto Bure?
4. Mnajaza makalio yenu kula michips kuku ya DAR wakati Magufuli anawatengenezea mabarabara, na maji
5. umeme wanaunganishiwa kwenye nyumba zao za nyasi ambazo mmeshindwa hata kuzipaua
6. Mmekalia milupo mijini na kulalamika kwa kila hatua ya mafanikio ya Magufuli wakati bibi zenu wanaanzishiwa miradi midogo kupitia Tasaf?
Watanzania sio mabwege tena mkawalaghai na vipropaganda uchwara eti "bibi wa kijijini anafaidikaje"? Wakati wakaazi wa vijijini wanainjoi maisha kama mijini tena bila STRESS.
1.kama bia za baridi wanakunywa
2. Zahanati kila mtaa na dawa zipo
3. Watoto wanasoma bure
4. Zamani mlikuwa mnawaringishia kunywa chai siku hizi halipo hilo
5. Bodaboda, vifodi au daladala rundo tena wanashushiwa milangoninmwao
6. Wanaangalia Tv kwenye matembe yao
7. Nyumba za kisasa zinajengwa wakati mnaojidai wa mijini mnapanga room za kajamba nani
8. minara ya mawasiliano kila kijiji.
Aisee mikono imechoka kutype. Muukubali tu mziki wa uncle Magu vinginevyo mtapanuka mioyo
 
SWALI:
Hivi kwa mfano lile daraja jipya pale salenda likikamilika kama unapinga maendeleo hautapita hapo..?
 
Hili sio lile la kule ng'ambo... Hili mbona linafanana na pale mnazimmoja pale Dar
 
Amefanya mageuzi au amejikita kwenye miundombinu mbinu kwa nguvu zake zote? Mageuzi yangeanzia kwenye taratibu, sheria na katiba. Huenda hujui mageuzi yana maana gani kwa upana wake, hivyo unajikuta unachanganya kati ya mageuzi na miundombinu mbinu mingi.

Mfano mrahisi wa mageuzi tungeliona sera zingebadilika, tungeona mifumo ikibadilika kama badala ya yeye kuteua kila Mkuu wa taasisi za umma zoezi hilo lingefanywa na taasisi nyingine. Nguvu zingehama kutoka kwa mtu na kuwa na taasisi imara. Kama hayo hayajafanywa basi ujue hiyo miundo mbinu sio mageuzi bali ndio matumizi halisi ya mikopo na kodi za wananchi. Kama ili mtu kuwa kiongozi bado wizi wa kura kupitia tume isiyo huru ya uchaguzi ndio inatoa maamuzi hayo sio mageuzi.
Mageuzi yaweza kuwa na athari chanya au hasi. Jadili mageuzi kwa kutazama pande zote (chanya na hasi), siyo uelekeo mmoja tu.
 
Back
Top Bottom