FORBES: Rais Magufuli ni ‘Rais Mwanamageuzi’

FORBES: Rais Magufuli ni ‘Rais Mwanamageuzi’

Habari hii inamsaidia vipi bibi yangu kule kijijini ambaye anatumia maji yasiyo safi na salama
Kwani bibi yako anaetumia maji yasiyo safi akianza kutumia yalio safi anasaidia nini kwa yule kijana alieko dar kwenye ujenzi wa SGR?
 
Isijekuwa hilo jarida forbes limechapishiwa lumumba!!
 
Baraza la vijana la demacha njoni mpinge na hii ya wazungu
 
Asante kuniita, nimeitika,
Haya ndio majarida ya kizalendo na kiukweli kwa ajili ya kuleta maendeleo ya Africa, sio the Economist, kila siku wao ni kukandia.

Ni ukweli uliowazi, rais Magufuli amefanya mageuzi makubwa ambayo by 2025, yatakuwa yameibadili Tanzania kuwa ni nchi ya viwanda, nchi ya uchumi wa gesi na nchi ya uchumi wa kati kupitia :

Shirika kubwa la ndege la ATC, litakalo kuwa la 3 baada ya Ethiopia na SAA,
Tutakuwa na SGR ambapo bandari za Tanzania ndizo zita handle cargo ya Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi na DRC.

Umeme wa Stigler sio tuu tuta export electricity, tunaweza ku electrify DART, magari yakatumia umeme.

Uchumi wa gesi kwa industrial power, na domestic use, hadi gesi ya majumbani, na magari kutumia gesi badala ya mafuta, India, hadi bajaj, zinatumia gesi!.

Maeneo yote yatakuwa accessible kupitia miondombinu ya mabarabara, reli, ndege, ma flyovers na ma interchanges kama ya Ubungo yatashehenezwa kote hivyo kurahisisha movement of people, goods and services.

Tutaboresha kilimo chetu kuwa ni kilimo cha kisasa kwa kutumia mechanized agriculture, na kutumia kilimo biashara kuzalisha malighafi ya viwanda.

Kupitia elimu bure, tutatengeneza taifa la kisomi lenye nguvu kazi ya kutosha na teknolojia ya kisasa kuendesha Tanzania ya viwanda.

Tanzania, itakuwa ni nchi ya viwanda, everything we producer kinakuwa processed humu humu nchini to add value, badala ya kuuza korosho ghafi, ambayo ina short life span, tutabangua korosho yote na ku export. Badala ya kuuza mahindi, tutauza unga, etc. Tutatengeneza almost everything, hivyo Tanzania kuwa an industrial power.

Yote haya hayawezi kufanikiwa bila a price to pay kwa mageuzi ya kisiasa kwenye democracy na human rights. 2020 yanakuja mageuzi makubwa ya Tanzanian democracy, uchaguzi wa 2020 utairudisha CCM in full control of this country, hivyo kufuatia hii kazi nzuri ya kuleta maendeleo anayoifanya rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5, kutakako ifanya CCM, ikubalike sana na Watanzania, uchaguzi wa 2020 kwa huku bara, Watanzania wote wataichagua CCM tuu, hivyo Bunge lijalo ni Bunge la chama kimoja, na kukitokea mpinzani kurudi bungeni, ni mpinzani mmoja tuu, Zitto, kama asipogombea urais kwa tiketi ya upinzani, tena huyu atarejea kwa sababu yeye ni Mwami.
Haya pia ni mageuzi.

Magufuli atainyoosha nchi, hakutakuwa na rushwa na ufisadi, uzembe, uvivu kwa kusingizia mikutano ya kisiasa, na uzururaji kusingizia kufanya maandamano, kila mtu sio anaombwa kufanya kazi, au anabembelezwa kufanya kazi, bali kila mtu ni lazima afanye kazj, na asiye fanya kazi na asile, afe, hapa kazi tuu hata ikibidi kwa mijeledi. Ndivyo walivyofanya kina Seretse Khama wa Botswana, Tito wa Yugoslavia, Lee Kuan Yew wa Singapore, Mustafa Kemal wa Uturuki, hawa wote walitawala kwa mkono wa chuma kuzikomboa nchi zao toka umasikini na kuzigeuza tajiri, hivyo Magufuli ataigeuza Tanzania kuwa a Donor Country.

Pia tutakuwa na mageuzi kwenye media, right of information, access to information, na mambo ya human rights, ikiwemo freedom of expression, nchi yetu itakuwa iko vitani kwenye vita vya kiuchumi, mtu yoyote atakaye turudisha nyuma kwa mawazo, maneno na matendo, hawezi kuachwa hivi hivi akasurvive. Atafanywa nini, hili sio langu ni la vyombo husika, wakiwemo wale waodhaniwa ni wasiojulikana.

No gain without pain, hivi ndivyo the tiger walivyo pata maendeleo, anachikifanya Magufuli sasa, wengi mtakielewa 2025, na ikifika hayo hayakamilika, aendelee, akamilishe ndipo apumzike.
P
Umemsifia sana mkulu hata kwa yale ambayo ni dhahiri haoneshi kufanikiwa kama sekta ya kilimo.

Huko sijamuelewa kabisa.
 
We bhana mi nina kesi na wewe manake tangia utoe simulizi yako kuhusu Mshua wako, mke wangu Khantwe hataki kabisa kuongea na mimi, na mara zote anakesha kwenye uzi wako, na labda kuna mengine zaidi ya hayo! Mkuu wangu Relief Mirzska, nitakuja huko kuripua bomu lakini nimegundua mbaya wangu ni huyu Analyse; manake baada ya ku-analyse maisha ya mshua ake, inaelekea hivi sasa ameanza kum-analyse my wife wangu! Na nasema hivi, mwambie Swahiba ako Khantwe, am watching her closely, ngoja nimalize mishe zangu mitaa ya kati 🙄😀!
Hadi huku [emoji134][emoji134][emoji134]
 
Hakuna, lakini tatizo ni pale unapojaribu kuaminisha umma kwamba "napendwa" wakati umelipia tangazo itangazwe kwamba "unapendwa!" Tatizo ni pale unapojaribu kuutangazia umma kwamba unafanya mambo mazuri kweli kweli kumbe umelipia tangazo liuambie umma usiokufahamu vizuri kwamba unafanya mambo mazuri kweli kweli!!

Kwenye siasa ukifikia hatua hiyo, moja ya tafsiri zake ni kwamba, kile ambacho ulitarajia kionekane, basi hakionekani sawasawa au hakionekani kabisa, na kama kinaonekana sawasawa basi kuna kingine kinachoonekana sawasawa zaidi!!

Kama ni Investor, kinachoonekana sawasawa zaidi ni urasimu uliokithiri na mrundikano wa mikodi kila pahala! Kinachoonekana sawasawa zaidi, ni mtikisiko mkubwa wa sekta binafsi huku kukiwa na tuhuma za serikali kufanya ndivyo sivyo kwa wawekezaji; iwe wazawa au wageni; na mengine sawa na hayo, ambayo endapo yasingekuwepo au yasingekuwa ndiyo yanayoonekana zaidi, basi hilo la kwenda Pernas huenda wala lisingekuwapo!
Yaani jamaa ana Honga kabisa ili aweze kupikiwa takwimu pumbavu sana
 
Huyu mzee ana haha ana puyanga kutaka kuiaminisha ' ' jamii kuwa ana kubalika kumbe hamna kitu. .....Sijui ana matatizo gani
Kumbe ni sponsored article iliyoandaliwa na Penresa na kuwekwa Forbes Africa! Siyo article ya Forbes, na wala haipo ndani ya Jarida la Forbes.

Forbes hawawezi kuandika kitu kisichofanyiwa utafiti. Penresa ni marketing company, wamefanya hii marketing kwa gharama gani? Na nani amelipia hiyo gharama? Walioamua kwenda Penresa kuomba kufanyiwa hiyo marketing, wamefanya hivyo kwa lengo gani?

Ama kweli, kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza. Hatuwezi kujiuza mpaka tukafanye kazi ya kuomba kupambwa?
 
Forbes hela yako tu hata wewe utaandikwa
 
Back
Top Bottom