nakusaidia kumuita CC:
Pascal Mayalla
Asante kuniita, nimeitika,
Haya ndio majarida ya kizalendo na kiukweli kwa ajili ya kuleta maendeleo ya Africa, sio the Economist, kila siku wao ni kukandia.
Ni ukweli uliowazi, rais Magufuli amefanya mageuzi makubwa ambayo by 2025, yatakuwa yameibadili Tanzania kuwa ni nchi ya viwanda, nchi ya uchumi wa gesi na nchi ya uchumi wa kati kupitia :
Shirika kubwa la ndege la ATC, litakalo kuwa la 3 baada ya Ethiopia na SAA,
Tutakuwa na SGR ambapo bandari za Tanzania ndizo zita handle cargo ya Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi na DRC.
Umeme wa Stigler sio tuu tuta export electricity, tunaweza ku electrify DART, magari yakatumia umeme.
Uchumi wa gesi kwa industrial power, na domestic use, hadi gesi ya majumbani, na magari kutumia gesi badala ya mafuta, India, hadi bajaj, zinatumia gesi!.
Maeneo yote yatakuwa accessible kupitia miondombinu ya mabarabara, reli, ndege, ma flyovers na ma interchanges kama ya Ubungo yatashehenezwa kote hivyo kurahisisha movement of people, goods and services.
Tutaboresha kilimo chetu kuwa ni kilimo cha kisasa kwa kutumia mechanized agriculture, na kutumia kilimo biashara kuzalisha malighafi ya viwanda.
Kupitia elimu bure, tutatengeneza taifa la kisomi lenye nguvu kazi ya kutosha na teknolojia ya kisasa kuendesha Tanzania ya viwanda.
Tanzania, itakuwa ni nchi ya viwanda, everything we producer kinakuwa processed humu humu nchini to add value, badala ya kuuza korosho ghafi, ambayo ina short life span, tutabangua korosho yote na ku export. Badala ya kuuza mahindi, tutauza unga, etc. Tutatengeneza almost everything, hivyo Tanzania kuwa an industrial power.
Yote haya hayawezi kufanikiwa bila a price to pay kwa mageuzi ya kisiasa kwenye democracy na human rights. 2020 yanakuja mageuzi makubwa ya Tanzanian democracy, uchaguzi wa 2020 utairudisha CCM in full control of this country, hivyo kufuatia hii kazi nzuri ya kuleta maendeleo anayoifanya rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5, kutakako ifanya CCM, ikubalike sana na Watanzania, uchaguzi wa 2020 kwa huku bara, Watanzania wote wataichagua CCM tuu, hivyo Bunge lijalo ni Bunge la chama kimoja, na kukitokea mpinzani kurudi bungeni, ni mpinzani mmoja tuu, Zitto, kama asipogombea urais kwa tiketi ya upinzani, tena huyu atarejea kwa sababu yeye ni Mwami.
Haya pia ni mageuzi.
Magufuli atainyoosha nchi, hakutakuwa na rushwa na ufisadi, uzembe, uvivu kwa kusingizia mikutano ya kisiasa, na uzururaji kusingizia kufanya maandamano, kila mtu sio anaombwa kufanya kazi, au anabembelezwa kufanya kazi, bali kila mtu ni lazima afanye kazj, na asiye fanya kazi na asile, afe, hapa kazi tuu hata ikibidi kwa mijeledi. Ndivyo walivyofanya kina Seretse Khama wa Botswana, Tito wa Yugoslavia, Lee Kuan Yew wa Singapore, Mustafa Kemal wa Uturuki, hawa wote walitawala kwa mkono wa chuma kuzikomboa nchi zao toka umasikini na kuzigeuza tajiri, hivyo Magufuli ataigeuza Tanzania kuwa a Donor Country.
Pia tutakuwa na mageuzi kwenye media, right of information, access to information, na mambo ya human rights, ikiwemo freedom of expression, nchi yetu itakuwa iko vitani kwenye vita vya kiuchumi, mtu yoyote atakaye turudisha nyuma kwa mawazo, maneno na matendo, hawezi kuachwa hivi hivi akasurvive. Atafanywa nini, hili sio langu ni la vyombo husika, wakiwemo wale waodhaniwa ni wasiojulikana.
No gain without pain, hivi ndivyo the tiger walivyo pata maendeleo, anachikifanya Magufuli sasa, wengi mtakielewa 2025, na ikifika hayo hayakamilika, aendelee, akamilishe ndipo apumzike.
P