For matured only: Tuongelee home budget na financial responsibilities kwa familia kati ya mume na mke. Kwako ikoje?

Busara Kali

Member
Jan 7, 2021
59
77
Nini mtazamo wako juu ya mpangilio wa majukumu yahusuyo fedha kwa familia yenye mume, mke watoto na hawajajenga. Ishu za matumizi ya nyumbani, ada, malengo ya ujenzi n.k

1642489661367.png

 
Mtazamo wako juu ya financial responsibilities za nyumbani ikiwa wote wa2 wanavipato
Responsibilities Kwa silimia kubwa over 80% inaenda Kwa mwanaume labda kama mkeo Hana kipato Cha kuingiza, kwangu Mimi Masuala ya kula (msosi wa familia) ni jukumu langu mwenyewe, shule wife anachangia 25% ya ada za watoto, maendeleo tunachangia wote tukiamua kufanya jambo Fulani tunajadiliana na Kila Mmoja anachangia
 
Alafu pesa zake zinaenda wapi huyo mwanamke dada?
Huwa tunapendeza ili msichepuke pia tunaweka akiba. Kuna wakati unasikia mama mkwe ameanguka huko kijijini, unawahi kumpeleka hospitali. Unamnunualia na nightu dress, khanga, vitenge, mswaki, lotion sabuni na kataulo kidogo. Haya mambo wanaume hawaya kumbuki.

Pia baba akikwambia hali yake ni ngumu unaweza kumsaidia na milioni 2-5.
 
Traditionally ni jukumu la mume, ila mambo mengi yamebadilika kwa hiyo kwa mtazamo wangu kama umemzidi mke kipato wewe deal na fees na bills zingine kama maji umeme na yeye mwachie vya jikoni.
Na ikiwa mna kipato sawa na mnaishi kwa maelewano wekeni bills mezani na vipato vyenu mezani mpangilie kwa makubaliano.

👀Hili litawezekana tu kama mke atajiridhisha huna bills nyingine nyumba za kando.
 
Sasa hapa tujadili nini mkuu? Unajua kuna unavyotaka hali iwe na vile hali ilivyo.

Yote kwa yote, majukumu ya kutunza familia ni ya mwanaume, hapo haijalishi mke ana kipato au hana kipato. Akiamua kusaidia sawa au kama kuna wakati mambo ya mme hayajakaa sawa asaidie lakini kamwe haiwezi kuwa jukumu lake.

Hata kama kuna kitu cha ziada kimetatiza naweza kutafuta pesa nje kutokumsumbua wife ili niirudishe kuliko wife akikupa kama anakukopesha unaweza kuchelewa akaanza dharau za rejareja.
 
Tukubaliane kuwa kama mwanaume unaweza fanya yote mwenyewe. Mke yeye akiamua kuchangia ni sawa ila mwanaume usikae ukiwa na matarajio ya kupata chochote kutoka kwa mkeo.

Wanawake mara nyingi ni wabinafsi sana. Anaweza kuwa anafanya kazi na ana mshahara mzuri ila anakuomba jero ya vocha.
 
inafika hatua hata mwanamke anaona aibu au huruma
Mimi ninafikiri wanaume tubebe tu majukumu yetu yote kama vichwa vya hizi familia zetu.

Mke akiwa na kazi, wewe chukulia ni mama tu wa nyumbani ili uweze kupambana vyema.

Ukisema unapambana mpaka mke aone huruma kama alivyoshari mdau...aisee utakufa ukisubiri hiyo huruma bila kuiona. Wanawake wa hivyo waliishia kwenye vita kuu ya dunia.

Hawa wanawake wa siku hizi sio kabisa.
 
Huwa tunapendeza ili msichepuke pia tunaweka akiba. Kuna wakati unasikia mama mkwe ameanguka huko kijijini, unawahi kumpeleka hospitali. Unamnunualia na nightu dress, khanga, vitenge, mswaki, lotion sabuni na kataulo kidogo. Haya mambo wanaume hawaya kumbuki.

Pia baba akikwambia hali yake ni ngumu unaweza kumsaidia na milioni 2-5.
Kwani mwanamke anakuwa anaendeleza familia ya nani?yake au Yao?Mama yake angeendeleza yao angekuwa wapi?
 
Back
Top Bottom