Kuna tofauti kubwa kati ya kutafuta mke/mume na kutafuta mpenzi

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,270
40,085
Kuna njia au namna za kutafuta mke/mume na kutafuta mpenzi. Ni vizuri ukajua kuzitofautisha. Njia utakazotumia kutafuta mke/mume ni tofauti na njia utakazotumia kutafuta mpenzi.

Ukijichanganya kwenye hizo njia, mwisho wake huwa ni kilio; mfano ulitumia njia za kutafuta mpenzi ili upate mke/mume, hapo lazima changamoto za ndoa zitokee tu.

Na kama ulitumia njia za kutafuta mke/mume ili upate mpenzi, hapo lazima upande mwingine uumie, kwa sababu kutakuwa na upande utakaopenda zaidi na kujipa mamlaka ya kukumiliki.

Vitu vya kuangalia katika kutafuta mke/mume:
  • Utu
  • Kujali
  • Mwenye imani ya kidini
  • Mnyenyekevu
  • Mvumilivu
  • Mwenye mtazamo wa kifamilia
  • Mwenye uchungu na familia
  • Mwenye mawazo ya kuboresha mapato ya familia
Vitu vya kuangalia katika kutafuta mpenzi:
  • Awe ana chura
  • Awe mtanashati
  • Awe ana hela
  • Awe ana umbo zuri
  • Awe na mali
  • Awe na mwanya
  • Awe na kazi nzuri/ ya maana
  • Atoke kwenye familia yenye kipato
  • Awe mrefu
  • Awe mnene
  • Awe na biashara n.k
Tumieni njia sahihi, ili msiwatese watoto wa wenzenu.
 
Imani inampa hofu ya Mungu, hasa pale utakapopata ulemavu, au uchumi kwenda hovyo n.k
Kuna komandoo nipo naye huwaga hana habari na kanisa.Akijiamulia huwa anaenda misa ya jioni/watoto.Ila kwa kuongoza sala wakati wa kula na tunapotaka kulala hajambo.

Hata anapotaka kunywa bia huwa anatulia kidogo.Ni imani yangu huwa anaziombea bia tunazogonga.She is so sweet!
 
Hapo kwenye "utu na kujali"..mke akiwa mtu mwenye utu na kujali sana huoni kwamba atakua mtu wa kukubali kila OMBI la mwanaume atakaye mtongoza kutokana na tabia yake ya utu na kujali sana shida za wengine??

Yaani kwa kifupi atakua "mama huruma" na wahuni watamgonga sana tu.


#kuchapiwahakuepukiki.
 
Hapo kwenye "utu na kujali"..mke akiwa mtu mwenye utu na kujali sana huoni kwamba atakua mtu wa kukubali kila OMBI la mwanaume atakaye mtongoza kutokana na tabia yake ya utu na kujali sana shida za wengine??

Yaani kwa kifupi atakua "mama huruma" na wahuni watamgonga sana tu.


#kuchapiwahakuepukiki.
Anayekuthamini wewe tu
 
Back
Top Bottom