William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
- Thread starter
-
- #61
Mkuu FMES
Katika picha hizi sioni sura ya Mzee Issa Matona, inawezekana huyo ni mtoto wake lakini siyo yule wa KIMASOMASO ninayemfahamu,.
Huu wimbo umefanana sana yaani kasoro maneno tu na lugha na wimbo wa Caiphus Semenya & Letta Mbulu uitwao everybody sing along. Huu unaweza kuusikiliza hapa: http://www.amazon.fr/Thalassa-collection-Afrique-Sud-Cap/dp/B00005UV78
Kuna wimbo ambao nimegundua juzijuzi kuwa Marijan Shaaban alichukua beats zake ni huu hapa chini. Huu unafanana sana na wimbo wa Mayasa unavyoanza.
http://www.youtube.com/watch?v=MSrklNeDwNM
Kichuguu,
Ndiyo maana nikauliza kwa sababu moja kubwa sana. Nilikuwa sifahamu/sikumbuki ni mwaka gani hizo nyimbo zimepigwa. Inawezekana kabisa jamaa wakawa wameiga wao kama walichukua baada ya miziki ya Tanzania au hata wote wakawa waliiga kutoka kibendi fulani kidogo sana.
Ule wimbo wa Mayasa vs Byron nilisema ni kile KIPANDE CHA MWANZO tu kama 20 seconds za mwanzo. Kule mbele hazifanani kabisa kabisa.
Wimbo ambao hadi leo nina uhakika Koffi Olomide ali-copy ni huu aliimba Max Bushoke sina uhakika na bendi gani ila anaimba "Kiu ya jibu mamaa, ndiyo inisumbuaayo. Natafuta jibu litakalonirushia? furaha, nimechoka kulala macho na kuota ndoto za alinacha...." Huu pekee nina uhakika kuwa ulipigwa kwanza Tanzania na baadaye Koffi akaja akapiga.
http://www.youtube.com/watch?v=jfoxX7jZwtc&feature=related
(Anzia 0:20. Beats zake ni sawa kabisa na huo wa Chidumule. Labda ni bahati mbaya).
Kwa Koffi Olomide, hii album yenye wimbo huu (Noblesse Oblige) kwangu inbaki milele kuwa THE BEST OF KOFFI OLOMIDE. Ila kila album kulikuwa na wimbo wa kukata na shoka. Kama Civilise, Coucou, Loi, etc////
Vijana Jazz Band
Nilitaka Iwe Siri: Vijana Jazz Band. <noscript>
</noscript> <script language="Javascript"> var imageViewerTagDiv = '
'; document.write(imageViewerTagDiv); </script>
- Hii ni bendi ya Vijana Jazz, iliyokuwa bendi ya umoja wa vijana wa Tanu na baadaye CCM, ilianzishwa na Mzee John Ondolo, baadaye ikaja kuwika sana na kiongozi wake Hemedi Maneti "Chiriku", pamoja na mpiga solo wake maarufu sana Hamza Kalala "Komandoo".
- Vijana Jazz waliwahi kupiga vibao maarufu sana enzi hizo kama "Kuruka Ukuta", "Zuhura", "Salima", "Chiku", "Operation Maduka" na zinginezo kama "Amba Baharia". Mungu amuweke pahali pema peponi marehemu Maneti.
Respect.
FMEs!