Flyover ya Ubungo ya kishamba sana

Flyover ya Ubungo ya kishamba sana

Hivi ndio kusema hawa viongozi wetu wanapotembelea nchi za wenzetu huwa hawapiti barabarani na kuziona hizo flyover za wenzetu zilivyozunguka kama nyoka? Mie nilidhani daraja la Mfugale walilijenga hivyo kutokana na ufinyu wa nafasi lakini nashangaa hadi interchange ya Ubungo nayo inajengwa kishamba tena.

Waende basi hata hapo South Africa wakaone jinsi mizunguko ya flyover ilivyozungushwa.
Ni ya hovyo sana
Kuna pesa imepigwa hapo hatari
 
Kwani hili neno flyover watu wamelitoa wapi?? maana mimi nilisoma kile kibao alicho fungua magufuli kimeandikwa Daraja la mfugale au ndio tusema daraja likiwa ju ju linaitwa flyover?
 
Kwani hili neno flyover watu wamelitoa wapi?? maana mimi nilisoma kile kibao alicho fungua magufuli kimeandikwa Daraja la mfugale au ndio tusema daraja likiwa ju ju linaitwa flyover?

Ile ni flyover siyo daraja, usipende kuropoka vitu usivyokuwa na uhakika navyo

Daraja lina connect two points ambazo zimetenganishwa na natural setting ya eneo kama vile mito, bahari, bonde n.k

Flyover inaconnect two or more points ambazo zimetanganishwa na man made structures kama vile majengo barabara hasa kwenye junction ili kupunguza foleni...
 
hakuna mtu anayeponda huo ujenzi na utasaidia sana...lakini acha watu waendelee kusifia lakini moyoni wanajua kwamba design ya pale ni mbaya bora ile ya kwanza ingefanyiwa modification kidogo....kile kitu kinachojengwa pale sio arficial kwamba miaka miwili mbele unakiamisha....
 
Ikituboa tutabomoa na kujenga nyingine mpya maana Tanzania ni nchi tajiri. Hapo tupo kwenye majaribio ya kuona jinsi fly-over zinavyoonekana zikishajengwa na kukamilika!
 
Kwa kweli pale Ubungo palitakiwa kuwa na fly-over nzuri maana ndio lango la jiji kwa sasa.
 
Pale Ubungo naamini kutakuja kuwa shida kuu mbili labda kama kuna ufumbuzi tayari

1. Kituo cha BRT kilichopo upande wa Tanesco kipo karibu sana na mdomo wa daraja, mahali ambapo kutakuwa na movemwnts za watu wanaoingia na kutoka kituoni kwa kivuko cha pundamilia. Hili litaepukika kama kuna mpango wa daraja la waenda kwa miguu.

2. Kuna uwezekano kukatokezea foleni mpya kwa magari yanayotoka Kimara kwenda mjini nyakati za asubuhi, maana kutakuwa na kikwazo kipya nacho ni taa za Shekilango/UBC na hata za Urafiki. Najua wanaweza wakawekwa askari waongoza magari (suluhisho la muda mfupi)
 
Ilitakiwa mtu akiwa anatoka upande wowote aweze kupita juu kama yupo speed na aelekee uelekeo wowote anaoutaka na akijichanganya tu ajikute ametokea siko na sio tu mtu anayetoka kimara au mjini/ Buguruni au Mwenge ndio apite juu. Ilitakiwa kupita barabara ya chini iwe ni choice ya mtu na sio kulazimishwa na njia.
Huu ujinga umsomea wapi mkuu? Kwa nini uakariri ungali mtu mzima hivyo?
 
Hata mimi mpaka leo sijawaelewa kwa nini walibadilisha hii....wakati jiwe anasema fedha zipo....nasikia hata ile ya mfugale ilibadilishwa juu kwa juu ila isingekuwa vile.....Ubungo hawajengi tena Flyover bali wanajenga madaraja ya juu.Makandarasi wa ovyo kabisa hawa.
Mie ile dizaini ya kwanza naona ndo ilikuwa ya Hovyo,bora hii Sasa ipo simple less expensive,halafu effective.Kwenye dizaini ya mwanzo ile ghorofa ya kwanza gari ilibidi zisubiriane.Dizaini mpya ina round about kubwa kwa chini halafu gorofa ya kwanza na pili gari Wala hazisimani.Mie naona dizaini iko poa tu haina mbwembwe
 
Pale Ubungo naamini kutakuja kuwa shida kuu mbili labda kama kuna ufumbuzi tayari

1. Kituo cha BRT kilichopo upande wa Tanesco kipo karibu sana na mdomo wa daraja, mahali ambapo kutakuwa na movemwnts za watu wanaoingia na kutoka kituoni kwa kivuko cha pundamilia. Hili litaepukika kama kuna mpango wa daraja la waenda kwa miguu.

2. Kuna uwezekano kukatokezea foleni mpya kwa magari yanayotoka Kimara kwenda mjini nyakati za asubuhi, maana kutakuwa na kikwazo kipya nacho ni taa za Shekilango/UBC na hata za Urafiki. Najua wanaweza wakawekwa askari waongoza magari (suluhisho la muda mfupi)
Kituo cha Mwendokasi Ubungo maji sioni umuhimu wake wangekivunja tu,kitumike cha Terminal basi
 
Back
Top Bottom