Nyuzi joto sifuri ndiyo nini?
Vipimo vya joto vipo vingi na inabidi useme ni kipi?
Kama ulimaanisha Celicius basi peleka hizo units kwenye Fahrenheit kwa mfano na hapo fanya utakavyo.
Hii unaipataje?
mmmh! Na kama baridi ya leo ni 0 f, na kesho tunatarajia itakuwa baridi mara mbili ya hii ya leo, in maana ni baridi ya fahrenheit ngapi?
Duh, mzee hapa ndo umeniacha kabisa!
SMU, tunachokifanya hapa ni Mahesabu. Sawa na kubadili Sinus kwenda Cosinus au upande mwingine.Jibu unaweza kuliweka kwenye Tan, Sin, Cos, Radian, etc. Ni kitu kilekile ili muradi urahisishe maisha. Utamu wa Mahesabu.
Kwa hiyo joto la 36°C ni mara mbili ya joto la 18°C? Kama ndiyo, kwa nini inapokuja kwenye 0°C tunabadilisha kupeleka kwenye kipimo kingine?
Itakua joto la 309°C!