Miji 15 nchini Italia yawekwa kwenye tahadhari kutokana na wimbi la joto kali

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Hali ya joto nchini Italia inatarajiwa kuongezeka kwa nyuzijoto 12C (53.6F) zaidi ya wastani.

Utabiri wa siku ya Jumamosi kwa JIji la Roma unaonesha kuwa halo iko katika nyuzijoto 37C (98.6F), na 43C (109.4F) siku ya Jumapili.

“Italia, Uhispania, Ufaransa, Ujerumani na Poland zote zinakabiliwa na wimbi kubwa la joto huku Hali ya hewa ya joto ikitarajiwa kupanda hadi nyuzi 48C (118.4F) katika visiwa vya Sicily na Sardinia, huenda hii ni hali ya joto zaidi kuwahi kurekodiwa barani Ulaya,”

Taarifa ya Shirika la Anga za Juu la Ulaya ilieleza siku ya Alhamisi, na kuongeza kuwa zebaki inayoongezeka katika bara hilo inafuata “hali ya joto inayovunja rekodi duniani.”
 
Back
Top Bottom