Fisadi wa Rada, Tanil Somaiya afanya kufuru IKULU

Hii ni story ya kutungwa.
Hakikutokea kitu kama hiki, hata walinzi waliokuwa zamu siku hiyo wanashangaa mtu anaweza kuandika uongo kama huu.

hii stori itanitia hasira kweli....kwa hiyo mi nimngependa kumuunga mkono kishongo na kuomba ushahidi wa hili jambo.....unataka kusema hakuna hata mmoja kati ya hao waliokuwa wamepigwa butwaa ambaye alipiga picha?.....tuone hata picha jamani. Isije ikawa mtu anatuandikia zakufikirika hapa....sisi tukajawa na jazba za kizushi.
 
Mtu ukisema watu wa pwani hawajui ethics za uongozi unaambiwa mdini au una wivu wa kike. Kwa ufupi ni Ikulu mfukoni!

Wakati wa Mzee ruksa watu walikuwa wanaingia Ikulu na kumwita mke wake shemeji na kuuliza kama chai tayari. Enzi za mkwere ndiyo usiseme. Ukiwa na pesa ikulu ni kwako na unashiriki kupanga baraza la mawaziri na teuzi mbalimbali za kitaifa!
....lakini ustaarabu haukamiliki mpaka ufike kwa watu wa pwani, wewe uko wapi sasa na unatoka bara ya wapi?
 
Ilikuwa ni siku ya Desemba 9, 2010. Tanzania ilikuwa inasherehekea miaka 49 ya Uhuru wa taifa. Baada ya kukagua gwaride Uwanja wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete alifanya dhifa ya kitaifa Ikulu na kualika viongozi wa serikali, mabalozi, viongozi wa dini na wafanyabiashara wakuu.

Waalikwa wote, walikuwa wanaingia Ikulu kupitia mlango wa nyuma ulio karibu na bahari upande wa ferry. Lango kuu la kuingia Ikulu lilikuwa halitumiki kwa wageni siku hiyo na lilitumiwa na Rais na viongozi wengine wakuu. Magari yote, ikiwemo ya mawaziri na mabalozi yalipaki nje ya Ikulu kwenye uwanja mkubwa ulio karibu na ferry na wageni waalikwa waliingia kwa mguu kwenye viwanja vya Ikulu.

Mmoja wa wageni waalikwa mashuhuri wa Kikwete alikuwa ni Tanil Somaiya, mmiliki wa Shivacom Group of Companies.

Wakati mawaziri na mabalozi waliambiwa na maafisa usalama Ikulu watumie mlango wa nyuma wa kuingia Ikulu na kutembea mpaka kwenye gardens ambako sherehe ilifanyika, Tanil alipewa heshima ya kipekee na kuruhusiwa kutumia main entrance gate.

Tanil aliingia Ikulu na gari la kifahari jekundu (a red FERRARI) na kuipaki gari hiyo kwenye mlango mkuu wa kuingia IKULU ambako huwa gari la Rais ndipo linapaki.

Aliiacha FERRARI hiyo hapo kwenye lango la kuingia Ikulu kwa zaidi ya masaa mawili huku akijimwaga kwenye dhifa.

Mawaziri, mabalozi na vigogo wengine walibaki wamepigwa na butwaa iwaje wageni wote waambiwe waingie Ikulu kupitia mlango wa nyuma kwa mguu na kuacha magari yao nje halafu mfanyabiashara huyu apite main gate na kuweka gari lake kwenye main entrance ya lango kuu la kuingia Ikulu.

Tanil ni rafiki wa karibu na business partner wa Shailesh Vithlani, mfanyabiashara ambaye amekimbia nchi kutokana na kashfa ya rada.

Tanil, ambaye ametajwa kwenye WikiLeaks kuhusu rada, amehusishwa pamoja na Vithlani kwenye kashfa ya rada, military trucks, military choppers, Gulfstream presidential jet na scandal nyingine.

Inaeleweka kuwa Tanil alimchangia pesa nyingi sana Kikwete kwenye uchaguzi wa Rais uliopita na pia alitoa helikopta zake zitumike kwenye kampeni ya CCM, lakini hii ndivyo Ikulu ya Mwalimu Julius Nyerere inavyodharauliwa siku hizi?

Kwa kutumia main entrance na kupaki gari lake mbele ya lango kuu la Ikulu, Tanil alikuwa anataka kuwaonesha wageni wote kuwa yeye yuko karibu sana na Rais wa nchi na Ikulu ni kama nyumbani kwake.

Mbaya zaidi, kufuru hii ilifanywa siku ambayo Tanzania inaadhimisha uhuru wake. Kuna uhuru kamili kweli kama watuhumiwa wakubwa wa ufisadi wanafanya kufuru namna hii mpaka IKULU?

Unatarajia kweli Edward Hoseah wa PCCB anaweza kuondokana na uoga wa kumkamata Tanil kwa ufisadi wa rada wakati Rais wa nchi ni besti wake na Ikulu ni kama playground yake?

Mbona mimi pia nilipita lango kuu na kupaki gari ndani? mimi nadhani hii sio ishu labda kwa washamba tu.Na unajua wengi hum jf ni watu wakuja kila kitu wanakishangaa.Ikulu mtaisikia tu,miaka yote tutakuwa na Rais mmoja at a time na huyo sio lazima awe yule unayemtaka wewe atakuwa ni yule ambae ni chaguo la Mungu kama jk
 
Wadau,
Ferrari yenyewe hii hapa na registration no. yake,hapa ikiwa imepakiwa kwenye parking lot yake ikiwa na mwenzi wake Ferrari orange,
This thing must stop now,enzi za Babu kweli mwanadamu kama huyu tena wa kiasia angeweza enda na kagari haka kakununua kwa hela zetu tulizoibiwa na kukapaki ndani tena ikulu???
umefika wakati serikali yabidi iogope nafasi za kiongozi walizopewa na angalau kuonyesha uoga sio kutuibia,kisha kutuonyesha ufahari usio na msingi unaotuongezea machungu ya makali ya maisha.
 
Attachments

  • TANIL's.jpg
    TANIL's.jpg
    38.4 KB · Views: 174
Tunawacheka kenya kwa Lois Mareno OCAMPO KUPELEKA MAWAZIRI WA SERIKALI THE HEGUE

ILA 2016 JK AND HIS ASSOCIATES WILL GO TO THE HEGUE.. FOR SURE

SIPATI PICHA AKIFUNGWA NA NORTH KOREA WAKASEMA WANAMPA JELA YA KUMFUNGIA...
 
Ndoto za alinacha. If all wishes were.....
 
Issue ni nini? Kupaki Ferrali nyekundu mbele ya lango kuu au kuingia na hiyo gari?
 
hii stori itanitia hasira kweli....kwa hiyo mi nimngependa kumuunga mkono kishongo na kuomba ushahidi wa hili jambo.....unataka kusema hakuna hata mmoja kati ya hao waliokuwa wamepigwa butwaa ambaye alipiga picha?.....tuone hata picha jamani. Isije ikawa mtu anatuandikia zakufikirika hapa....sisi tukajawa na jazba za kizushi.

Ikulu unaacha camera mlangoni. Japokua siku hiyo hakukua na ukaguzi getini lakini bado kwa anayefaham taratibu za pale ni risk kupiga picha hata kwa simu ya mkononi. Hata hivyo mimi nlibahatika kuwepo siku hiyo, sikuona gari hilo japokua haimaanishi kuwa kitendo hicho hakikutokea kwani mimi nlipitia geti la baharini na sikujali sana nini kinaendelea huko mbele

Hata hivyo inasikitisha sana!
 
Mimi nina Rais wangu moyoni, Kiongozi wangu,namuheshimu na kusikiliza maelekezo yake.

Halafu kuna Rais Mwingine ana Dola,ananitawala kwa unyonge wangu, simkubali na sikumpa kura yangu.
 
Wadau,
Ferrari yenyewe hii hapa na registration no. yake,hapa ikiwa imepakiwa kwenye parking lot yake ikiwa na mwenzi wake Ferrari orange,
This thing must stop now,enzi za Babu kweli mwanadamu kama huyu tena wa kiasia angeweza enda na kagari haka kakununua kwa hela zetu tulizoibiwa na kukapaki ndani tena ikulu???
umefika wakati serikali yabidi iogope nafasi za kiongozi walizopewa na angalau kuonyesha uoga sio kutuibia,kisha kutuonyesha ufahari usio na msingi unaotuongezea machungu ya makali ya maisha.

Heshima yako JF Senior Exper Member Iteitei Lya Kitee, Ferrari ya Tanil niliyo iona kwa macho yangu mbele ya lango la Ikulu ni hiyo nyekundu. Ni ushenzi sana huu
 
Mbona mimi pia nilipita lango kuu na kupaki gari ndani? mimi nadhani hii sio ishu labda kwa washamba tu.Na unajua wengi hum jf ni watu wakuja kila kitu wanakishangaa.Ikulu mtaisikia tu,miaka yote tutakuwa na Rais mmoja at a time na huyo sio lazima awe yule unayemtaka wewe atakuwa ni yule ambae ni chaguo la Mungu kama jk

Usitake kudanganya watu hapa. Siku hizi utaratibu Ikulu tangu kuapishwa kwa mawaziri na shuhuli zote zile zenye watu wengi utaratibu ni kuacha magari kwenye uwanja mkubwa uliopo geti la nyuma na watu wanaingia Ikulu kwa mguu. Wanaoruhusiwa kuingia Ikulu kwa magari yao ni Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na manaibu wake, na Tanil Somaiya. Au wewe ni mmoja wapo wa watajwa hawa?
 
....lakini ustaarabu haukamiliki mpaka ufike kwa watu wa pwani, wewe uko wapi sasa na unatoka bara ya wapi?

Ustaarabu wa mijitu ya Bara nikutumia makarasi chooni..utaliona jitu limevaa suti ya bei mbaya huku anatembea na haja kubwa....kazzi kweli kweli. Pwani ndio ustaarabu ulikoanzania bwana.
 
Mbona tittle na habari haviendani? Nini maana ya kufuru? Au wewe hujui kiswahili? Kweli wewe ni zezeta.

Ni wewe peke yako tu ambaye unaona title (sio tittle) haiendani na habari. Kwa hiyo wewe ndio mwenye matatizo na huenda ni 'zezeta' wewe!
 
eti Ikulu ya Nyerere!!!!

Love him or hate him, katika marais wote wanne ambao Tanzania imepata, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ndiye kiongozi pekee aliyesimamia maadili ya kiongozi wa umma ipasavyo na alikuwa hawachekei mafisadi. Ilikuwa ni ndoto kuona mafisadi wa aina ya Tanil Somaiya, Yusuf Manji, Subhash Patel na baba yao Rostam Aziz wakienda Ikulu. Hivi sasa kwenye dhifa yoyote ya kitaifa, majina ya mafisadi hawa ndio top on the list kwa VIP guests.

Enzi za Mwalimu hata wana familia yake wakitaka kumuona marufuku kwenda Ikulu. Anakutana nao Msasaaniiii!
 
Somaiya amenunua kampuni ya ulinzi ya Ultimate Security, nadhani anafanya warm up ya kuinunua Jeshi la wanachi wa Tanzania pamoja na Polisi.
By few years to come, huyu mtu atakuwa hakamatiki.
Sio "By few years to come", hivi sasa tayari hakamatiki. Masikini Watanzania sie.
 
Back
Top Bottom