Fisadi wa Rada, Tanil Somaiya afanya kufuru IKULU

Fareed

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
328
0
Ilikuwa ni siku ya Desemba 9, 2010. Tanzania ilikuwa inasherehekea miaka 49 ya Uhuru wa taifa. Baada ya kukagua gwaride Uwanja wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete alifanya dhifa ya kitaifa Ikulu na kualika viongozi wa serikali, mabalozi, viongozi wa dini na wafanyabiashara wakuu.

Waalikwa wote, walikuwa wanaingia Ikulu kupitia mlango wa nyuma ulio karibu na bahari upande wa ferry. Lango kuu la kuingia Ikulu lilikuwa halitumiki kwa wageni siku hiyo na lilitumiwa na Rais na viongozi wengine wakuu. Magari yote, ikiwemo ya mawaziri na mabalozi yalipaki nje ya Ikulu kwenye uwanja mkubwa ulio karibu na ferry na wageni waalikwa waliingia kwa mguu kwenye viwanja vya Ikulu.

Mmoja wa wageni waalikwa mashuhuri wa Kikwete alikuwa ni Tanil Somaiya, mmiliki wa Shivacom Group of Companies.

Wakati mawaziri na mabalozi waliambiwa na maafisa usalama Ikulu watumie mlango wa nyuma wa kuingia Ikulu na kutembea mpaka kwenye gardens ambako sherehe ilifanyika, Tanil alipewa heshima ya kipekee na kuruhusiwa kutumia main entrance gate.

Tanil aliingia Ikulu na gari la kifahari jekundu (a red FERRARI) na kuipaki gari hiyo kwenye mlango mkuu wa kuingia IKULU ambako huwa gari la Rais ndipo linapaki.

Aliiacha FERRARI hiyo hapo kwenye lango la kuingia Ikulu kwa zaidi ya masaa mawili huku akijimwaga kwenye dhifa.

Mawaziri, mabalozi na vigogo wengine walibaki wamepigwa na butwaa iwaje wageni wote waambiwe waingie Ikulu kupitia mlango wa nyuma kwa mguu na kuacha magari yao nje halafu mfanyabiashara huyu apite main gate na kuweka gari lake kwenye main entrance ya lango kuu la kuingia Ikulu.

Tanil ni rafiki wa karibu na business partner wa Shailesh Vithlani, mfanyabiashara ambaye amekimbia nchi kutokana na kashfa ya rada.

Tanil, ambaye ametajwa kwenye WikiLeaks kuhusu rada, amehusishwa pamoja na Vithlani kwenye kashfa ya rada, military trucks, military choppers, Gulfstream presidential jet na scandal nyingine.

Inaeleweka kuwa Tanil alimchangia pesa nyingi sana Kikwete kwenye uchaguzi wa Rais uliopita na pia alitoa helikopta zake zitumike kwenye kampeni ya CCM, lakini hii ndivyo Ikulu ya Mwalimu Julius Nyerere inavyodharauliwa siku hizi?

Kwa kutumia main entrance na kupaki gari lake mbele ya lango kuu la Ikulu, Tanil alikuwa anataka kuwaonesha wageni wote kuwa yeye yuko karibu sana na Rais wa nchi na Ikulu ni kama nyumbani kwake.

Mbaya zaidi, kufuru hii ilifanywa siku ambayo Tanzania inaadhimisha uhuru wake. Kuna uhuru kamili kweli kama watuhumiwa wakubwa wa ufisadi wanafanya kufuru namna hii mpaka IKULU?

Unatarajia kweli Edward Hoseah wa PCCB anaweza kuondokana na uoga wa kumkamata Tanil kwa ufisadi wa rada wakati Rais wa nchi ni besti wake na Ikulu ni kama playground yake?
 
The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
13,513
2,000
Hata wakati wa Mwinyi mambo yalikuwa similar na tunavyoona sasa.................... Nchi hii inawataka watu kama Slaa na Pombe Magufuri then heshima ya serikali itarudi.
 
Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
44,066
2,000
heheh nathani kazi ya Hoseah ni kitanzi jamani tumuache baba wa watu ana watoto nae... ngoma nzito wajameni! khaa
 
Mbaha

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
697
225
Hakuna ikulu nchii hii!!!!... kuna pango la wanyang'anyi tu hapo karibu na feri!!!!! Ndege wa unyoya mmoja wanaruka pamoja!! Rafiki wa mwizi ni mwizi!! .....&*%$£?@'^£@# .... I feel like bursting!!!!!....
 
The Dreamer

JF-Expert Member
Feb 2, 2009
1,282
0
Mtu ukisema watu wa pwani hawajui ethics za uongozi unaambiwa mdini au una wivu wa kike. Kwa ufupi ni Ikulu mfukoni!

Wakati wa Mzee ruksa watu walikuwa wanaingia Ikulu na kumwita mke wake shemeji na kuuliza kama chai tayari. Enzi za mkwere ndiyo usiseme. Ukiwa na pesa ikulu ni kwako na unashiriki kupanga baraza la mawaziri na teuzi mbalimbali za kitaifa!
 
Fanfa

JF-Expert Member
Sep 25, 2009
564
250
Kwa mtindo huu, hata akitaka ma-ketio ya wa na-Ikulu atapewa. Pesa anayo, nchi ni yake na sirikali ameiteka
 
Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,703
0
Ilikuwa ni siku ya Desemba 9, 2010. Tanzania ilikuwa inasherekea miaka 49 ya Uhuru wa taifa. Baada ya kukagua gwaride Uwanja wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete alifanya dhifa ya kitaifa Ikulu na kualika viongozi wa serikali, mabalozi, viongozi wa dini na wafanyabiashara wakuu.

Waalikwa wote, walikuwa wanaingia Ikulu kupitia mlango wa nyuma ulio karibu na bahari upande wa ferry. Lango kuu la kuingia Ikulu lilikuwa halitumiki kwa wageni siku hiyo na lilitumiwa na Rais na viongozi wengine wakuu. Magari yote, ikiwemo ya mawaziri na mabalozi yalipaki nje ya Ikulu kwenye uwanja mkubwa ulio karibu na ferry na wageni waalikwa waliingia kwa mguu kwenye viwanja vya Ikulu.

Mmoja wa wageni waalikwa mashuhuri wa Kikwete alikuwa ni Tanil Somaiya, mmiliki wa Shivacom Group of Companies.

Wakati mawaziri na mabalozi waliambiwa na maafisa usalama Ikulu watumie mlango wa nyuma wa kuingia Ikulu na kutembea mpaka kwenye gardens ambako sherehe ilifanyika, Tanil alipewa heshima ya kipekee na kuruhusiwa kutumia main entrance gate.

Tanil aliingia Ikulu na gari la kifahari jekundu (a red FERRARI) na kuipaki gari hiyo kwenye mlango mkuu wa kuingia IKULU ampako huwa gari la Rais ndipo linapaki.

Aliiacha FERRARI hiyo hapo kwenye lango la kuingia Ikulu kwa zaidi ya masaa mawili huku akijimwaga kwenye dhifa.

Mawaziri, mabalozi na vigogo wengine walibaki wamepigwa na butwaa iwaje wageni wote waambiwe waingie Ikulu kupitia mlango wa nyuma kwa mguu na kuacha magari yao nje halafu mfanyabiashara huyu apite main gate na kuweka gari lake kwenye main entrance ya lango kuu la kuingia Ikulu.

Tanil ni rafiki wa karibu na business partner wa Shailesh Vithlani, mfanyabiashara ambaye amekimbia nchi kutokana na kashfa ya rada.

Tanil, ambaye ametajwa kwenye WikiLeaks kuhusu rada, amehusishwa pamoja na Vithlani kwenye kashfa ya rada, military trucks, military choppers, Gulfstream presidential jet na scandal nyingine.

Inaeleweka kuwa Tanil alimchangia pesa nyingi sana Kikwete kwenye uchaguzi wa Rais uliopita na pia alitoa helikopta zake zitumike kwenye kampeni ya CCM, lakini hii ndivyo Ikulu ya Mwalimu Julius Nyerere inavyodharauliwa siku hizi?

Kwa kutumia main entrance na kupaki gari lake mbele ya lango kuu la Ikulu, Tanil alikuwa anataka kuwaonesha wageni wote kuwa yeye yuko karibu sana na Rais wa nchi na Ikulu ni kama nyumbani kwake.

Mbaya zaidi, kufuru hii ilifanywa siku ambayo Tanzania inaadhimisha uhuru wake. Kuna uhuru kamili kweli kama watuhumiwa wakubwa wa ufisadi wanafanya kufuru namna hii mpaka IKULU?

Unatarajia kweli Edward Hoseah wa PCCB anaweza kuondokana na uoga wa kumkamata Tanil kwa ufisadi wa rada wakati Rais wa nchi ni besti wake na Ikulu ni kama playground yake?

Tuseme nini sasa.Ni kama kupigia mbuzi gitaa.
 
collezione

JF-Expert Member
Oct 22, 2010
352
250
jakaya kikwete uku kwetu wanamwita kubwa jinga...
kifupi kapoteza heshima yake, hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba 10
 
Joyum

Senior Member
Oct 30, 2007
153
0
Hii inaonyesha ni jinsi gani hamna uhuru na katiba inavyokanyagwa na kutemewa mate na hawa mafisadi!!! Sasa hapo kama kulikuwa na mabalozi na wanapiga jeki bajeti yetu alafu wanaona watuhumiwa wa ufisadi wanakulashavu namna hii kwanini wasibane hiyo misaada? yani ni sawa na mtu anakuja kuomba hela ya kula familia yake alafu unampa kisha unamkuta baa anamwaga mipesa na mi-ofa kwa walevi wenzake na kutaka sifa. Yani unamnyang'anya kilichobaki.
 
Fareed

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
328
0
Ferrari ya Tanil iliyopaki mbele ya man entrance ya Ikulu ni kama hii hapa:

Google Image Result for http://www.madwhips.com/upload/images/my_friends_red_ferrari_f430_5-568-426.jpg FERRARI.jpg
 
eliakeem

JF-Expert Member
May 29, 2009
12,633
2,000
Nafuu Baba wa taifa JK Nyerere alijifia, sijui angefanyeje kuona sehemu takatifu kama ile ikichezewa na MAFISADI KAMA SOMAIYA. ........ NADHANI HATA SASA ANGEPEWA NAFASI YA KUFUFUKA NA KUSHUHUDIA MAMBO YANAYO FANYIKA, ANGESEMA BORA AENDELEE KUPUMZIKA KUZIMU.

HALAFU MOD KUFUTA POSTI ZA WENZAKO BILA KUTOA SABABU SI UUNGWANA. UMEZOEA SANA KUFUTA MICHANGO YANGU BILA KUTAJA SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA HIVYO.
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
2,000
Somaiya amenunua kampuni ya ulinzi ya Ultimate Security, nadhani anafanya warm up ya kuinunua Jeshi la wanachi wa Tanzania pamoja na Polisi.
By few years to come, huyu mtu atakuwa hakamatiki.
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,613
2,000
Wakati mwingine huwa nahisi hata kuwalaumu hawa 'waasia' pengine tunawaonea tu....zaidi ni udhaifu wa viongozi wetu na hasa Rais wetu. Mambo yote haya yanayotokea yanategemea sana 'tone at the top'! Ameshindwa kabsa kuwaambia "Ikulu ni mahali patakatifu".

Sitta aliwahi kumshauri awe mkali kidogo lakini nina mashaka makubwa kwamba alielewa alichoshauriwa! Kwa kweli tunastahili kuwa masikini.
 
Kishongo

JF-Expert Member
May 4, 2010
932
0
Ilikuwa ni siku ya Desemba 9, 2010. Tanzania ilikuwa inasherekea miaka 49 ya Uhuru wa taifa. Baada ya kukagua gwaride Uwanja wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete alifanya dhifa ya kitaifa Ikulu na kualika viongozi wa serikali, mabalozi, viongozi wa dini na wafanyabiashara wakuu.

Waalikwa wote, walikuwa wanaingia Ikulu kupitia mlango wa nyuma ulio karibu na bahari upande wa ferry. Lango kuu la kuingia Ikulu lilikuwa halitumiki kwa wageni siku hiyo na lilitumiwa na Rais na viongozi wengine wakuu. Magari yote, ikiwemo ya mawaziri na mabalozi yalipaki nje ya Ikulu kwenye uwanja mkubwa ulio karibu na ferry na wageni waalikwa waliingia kwa mguu kwenye viwanja vya Ikulu.

Mmoja wa wageni waalikwa mashuhuri wa Kikwete alikuwa ni Tanil Somaiya, mmiliki wa Shivacom Group of Companies.

Wakati mawaziri na mabalozi waliambiwa na maafisa usalama Ikulu watumie mlango wa nyuma wa kuingia Ikulu na kutembea mpaka kwenye gardens ambako sherehe ilifanyika, Tanil alipewa heshima ya kipekee na kuruhusiwa kutumia main entrance gate.

Tanil aliingia Ikulu na gari la kifahari jekundu (a red FERRARI) na kuipaki gari hiyo kwenye mlango mkuu wa kuingia IKULU ampako huwa gari la Rais ndipo linapaki.

Aliiacha FERRARI hiyo hapo kwenye lango la kuingia Ikulu kwa zaidi ya masaa mawili huku akijimwaga kwenye dhifa.

Mawaziri, mabalozi na vigogo wengine walibaki wamepigwa na butwaa iwaje wageni wote waambiwe waingie Ikulu kupitia mlango wa nyuma kwa mguu na kuacha magari yao nje halafu mfanyabiashara huyu apite main gate na kuweka gari lake kwenye main entrance ya lango kuu la kuingia Ikulu.

Tanil ni rafiki wa karibu na business partner wa Shailesh Vithlani, mfanyabiashara ambaye amekimbia nchi kutokana na kashfa ya rada.

Tanil, ambaye ametajwa kwenye WikiLeaks kuhusu rada, amehusishwa pamoja na Vithlani kwenye kashfa ya rada, military trucks, military choppers, Gulfstream presidential jet na scandal nyingine.

Inaeleweka kuwa Tanil alimchangia pesa nyingi sana Kikwete kwenye uchaguzi wa Rais uliopita na pia alitoa helikopta zake zitumike kwenye kampeni ya CCM, lakini hii ndivyo Ikulu ya Mwalimu Julius Nyerere inavyodharauliwa siku hizi?

Kwa kutumia main entrance na kupaki gari lake mbele ya lango kuu la Ikulu, Tanil alikuwa anataka kuwaonesha wageni wote kuwa yeye yuko karibu sana na Rais wa nchi na Ikulu ni kama nyumbani kwake.

Mbaya zaidi, kufuru hii ilifanywa siku ambayo Tanzania inaadhimisha uhuru wake. Kuna uhuru kamili kweli kama watuhumiwa wakubwa wa ufisadi wanafanya kufuru namna hii mpaka IKULU?

Unatarajia kweli Edward Hoseah wa PCCB anaweza kuondokana na uoga wa kumkamata Tanil kwa ufisadi wa rada wakati Rais wa nchi ni besti wake na Ikulu ni kama playground yake?

Hii ni story ya kutungwa.
Hakikutokea kitu kama hiki, hata walinzi waliokuwa zamu siku hiyo wanashangaa mtu anaweza kuandika uongo kama huu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom