Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo ambaye aliwasili Nchini kwa ziara ya Kitaifa ya siku mbili Tarehe 21 - 22 Agosti, 2023.
View: https://www.youtube.com/watch?v=fD3KSwiNGxI
View: https://www.youtube.com/watch?v=klwwBqPsRtU
Dondoo kadhaa
Ziara ya Rais Joko Widodo ni ziara ya pili ya kiongozi wa Taifa la Indonesia aliyopo madarakani kutembelea nchini.
Tanzania na Indonesia zina uhusiano wa muda mrefu na wa kihistoria ulioasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Indonesia, Soekarno.
Tanzania na Indonesia zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1964, ambapo Indonesia ilifungua Ubalozi wake nchini Tanzania na kuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa kufungua Ubalozi wake nchini, miaka michache baada ya uhuru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo wakati alipowasili katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuanza Ziara ya Kikazi hapa nchini tarehe 22 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo wakati wakielekea kwenye Viwanja vya mapokezi ya Viongozi Ikulu Jijini Dar es salaam wakati wa Ziara ya Kikazi ya Rais huyo hapa nchini tarehe 22 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania na Indonesia ukipigwa katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam kwenye mapokezi rasmi kwenye Ziara ya Kikazi ya Rais huyo hapa nchini tarehe 22 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo wakati alipokuwa akitia saini kitabu cha Wageni alipowasili Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 22 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 22 Agosti, 2023.
Rais Samia Suluhu Hassan
Ni moja kati ya Nchi za kwanza kufungua Ubalozi Nchini Mwaka 1964, tumekubaliana kuimarisha uhusiano baina ya Nchi zetu, kuna mengi zaidi yanaweza kufanyika na kuibua ushirikiano upande wa uchumi.
Kuimarisha uhusiano katika sekta ya viwanda na Kilimo pamoja na maendeleo ya Teknolojia.
Nchi zetu mbili zimeshirikiana katika sekta ya Kilimo, Mwaka 1996 Serikali ya Indonesia ilianzisha Kituo cha Kilimo Mkoani Morogoro na kuna mpango wa kufufua kituo hicho.
Tumekubaliana mambo mengi, lakini nimemweleza Jamhuri ya Muungano kuna pande mbili.

Attachments
-
9534e731-2001-4018-95d1-f5224d661526.jpg155.3 KB · Views: 4
-
082dafa9-6df5-49cc-bf5f-e2f2b8e982a4.jpg111.9 KB · Views: 4
-
9d5981b2-0840-4b24-9f70-a5bf0c3570b6.jpg152.9 KB · Views: 4
-
bed99d70-31ab-486e-bddc-8ececd48f2d1.jpg90.4 KB · Views: 5
-
642e6bf2-7614-4291-ab39-4582eb8312ec.jpg110.8 KB · Views: 8
-
2d7fdefc-dc28-4af2-9298-023e3f2419fe.jpg98.4 KB · Views: 5
-
Jokowi Tanzania 1.jpeg532 KB · Views: 1