Fisadi ni kama samaki - Tafakari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fisadi ni kama samaki - Tafakari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 29, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kama vile samaki anavyohitaji maji ili aishi vivyo hivyo fisadi huitaji
  ufisadi ili aishi na kufanikiwa. Kumtoa fisadi kutoka ufisadi ni sawa na
  kumtoa samaki kwenye maji ukidhania unamuokoa. Lakini samaki huvuliwa ili kugeuzwa mlo na siyo mapambo!  Wapo wengine hufanya uvuvi kama mchezo; wenyewe wanaita sport fishing ambapo samaki hutolewa kwenye maji, anaachwa anatapatapa halafu anarudishwa majini kuendelea kuishi. Ukiniuliza mimi hivi ndivyo ninavyoona mchezo wa CCM na ufisadi - Sport Corruption.. ambapo mafisadi huchezewa chezewa, hupewa chambo, hunaswa na kutolewa majini na watu wanashangilia. Lakini kabla hawajafa kwa kukosa oksijeni hurudishwa majini ambapo huruka ruka kwa furaha huku wananchi wakisubiri waone nani mwingine atavuliwa.

  Kumbe hatuhitaji wavuvi wa michezo tunataka wale wenye kuvua samaki ili kuwageuza kitoweo. Hawa wanafuata kanuni asili ya mababu kuwa "usivue samaki ambaye hutaki kumla" (msiniulize mababu walisema lini hilo).

  Tunahitaji viongozi wapya ambao hawatakuwa na muda wa mchezo na mafisadi bali watawakaanga na kuwageuza geuza katika jungu kuu la sheria huku mafuta ya ushahidi yakizidi kumiminwa juu yao.
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  One of the best analogies I have ever come across!! Luv it!!
   
 3. M

  MC JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kuna watu wakisoma hii .... machozi yanawalengalenga

  Pamoja na mambo mengine, Juhudi sasa zielekezwe kwenye ulinzi wa KURA !!! Baada ya hali ya hewa kubadilika, huko CCM hawana amani tena, wana wasiwasi na mgombea Uraisi wao, kuna watu watapelekwa MASTERS course ya jinsi ya kuiba Kura....
   
 4. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mkiji, I salute you! kweli we ni kichwa mkuu.. tafadhali malizia hii kitu uirushe kwenye magazeti ya bongo,
  bytheway, japo najua is below your standard but kuna magazeti ya udaku yanauzwa kama njugu huko bongo.. kwa makala nzuri zenye kuinua ari na mori wa kulikomboa taifa letu, unaonaje hata ukawa unazirusha huko mara moja moja ili ziwafikie wengi zaidi? hata yale magazeti ya alasiri huwa yanasomwa sana kwa vile ni bei chee.., na ili kufanya muendelezo waweza kuwa unatoa hizi makala kama hadithi fulani yenye muendelezo.. kwa njia hiyo utakuwa umetoa mchango mkubwa sana kuelekea ukombozi II wa bongo yetu!
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu hii ya samaki ina mantiki kali sana na nadhani unahitaji kuipa sura zaidi maanake kila napotazama TV kipindi cha sports fishing hucheka sana wanapoibua bonge la samaki wakapiga picha nalo, wakaonyesha meno yake na rangi zake kisha jinsi ndoana ilivyoweza kushika (TAKUKURU) na kadhalika. Lakini maajabu ya Mungu samaki huyo hurudishwa majini! halafu wao wakapongezana sana kwa jinsi kazi ilivyokuwa kubwa kumvua samaki huyo!.

  Hapo hapo majuzi tu nimeona kisha cha Nyangumi mmoja akirukia mashua na kuipindua majini, ikawa habari kubwa na kkutangaza jinsi samaki huyo anavyoweza kuwa hatari. Na hakika sijawahi kuona wavuvi wa sports fishing wakivua Nyangumi kwa mchezo huo huo maanake ni hatari kwa usalama wao... ooooh! nimekosea sio usalama wao ila ni Usalama wa mashua (Taifa).
   
 6. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ubarikiwe MM kwa makala makini kama hii. Ni mfano hai na halisi unaoendana na hali ndani ya nchi yetu. Tunahitaji kuwafikishia wananchi wote wa Tanzania makala kama hizi ili kuwaamsha akili zao.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Aisee nimecheka saaana hujui tu.. yaani na hilo ulilolisema itabidi niiendeleze kidogo sikuwa nimeifikiria sana lakini mawazo yenu hapa yamenipa mwanga zaidi.. thanks!

  NImechekaaaaa


  I like this!! LMAO!
   
 8. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Tungo kabambe hii. Tuangalie jinsi ya vitu kama hivi kuwafikia watz wengi zaidi, maana tumepumbazwa miaka mingi inahitajika nguvu ya ziada kutuzindua.
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni mfumo wenyewe wa kuwapata wavuvi. Mvuvi unampa maagizo kwamba no sports fishing lakini anaweka mashkio kwene pamba (sic). Mzizi wa fitna unapotakiwa kukatwa ni sisi wenyewe wadau kujifunza uvuvi na kuvua wenyewe! Hatuhitaji dalali kwene tenda muhimu kama hii.
   
 10. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mkuu hii threads, imesimama.keep up the good work.
   
 11. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Wetu mtiifu MM,
  Nami naungana kukupongeza kwa hii thread. Naomba kuuliza kuna wakati ulikuwa unatoa kile kijarida cha kila wiki, hata jina lake nimelisahau. Unaonaje wakati huu tunapoelekea uchaguzi mkuu ukakiendeleza ili watu waone njia ya ukombozi, na sisi hapa JF tu print na kuwasambazia wananchi nchi nzima? Hii itasaidia sana dhidi ya kampeni chafu za ccm za kofia, kanga na t-shirts.
   
 12. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 803
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Moto mpya, kiberiti kipya, na petroli mpya. Mpaka mafisadi waishe.
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Enzi za Mwalimu... kulikuwa na kipindi RTD cha MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI. Kisa hiki kimenikumbusha enzi zileee...
   
 14. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  CCM tatizo ni kwamba kilikuwa ni chama cha ukombozi na sasa zama zake zimekwisha,
  kilichobaki sasa ni kuwa chama cha majangili wa haki za wanyonge, na chama cha
  kuweka tofauti baina ya jamii na jamii
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Jul 31, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tunakushukuru wewe kwani pasipo mawazo ya mtazamo wa samaki sisi wengine tungeelea kununua sokoni na vijiweni wale waliokwisha kaangwa na kutiwa chunvi na ndimu. Nafikiri hapo pia umenipata..
   
Loading...