First Lady anapoingia Ikulu ni kuwa anaacha kazi kama ni mwajiriwa?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
43,044
2,000
Tuna bahati kubwa sana ya kupata ma First Lady kutoka taaluma ya ualimu. Kutoka mama Maria Nyerere, mama Salma Kikwete na sasa mama Janet Magufuli.

Wanapoingia Ikulu ni wazi kuwa wanakuwa na majukumu mapya. Sasa zile ajira zao huwa wanachukua early retirement?
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,637

Sky, hii role ya first lady haikuelezwa vema katika taratibu za nchi. Ni siku za karibuni imekuwa kama sehemu ya shughuli tu

Mama Maria alikuwa na jukumu la mama wa Taifa akimsaidia mzee nyumbani, ofisini n.k.
Hakuonekana kama 'first lady' wa siku hizi kwasababu alifanya majukumu yake bila taasisi rasmi na wala hakutaka media ziwe sehemu ya majukumu yake

Baada ya Mwalimu, Mzee Mwinyi naye alifuata nyayo kwa namna fulani, wakeze wakiwa na majukumu ya nyumbani na kimataifa kimya kimya bila taasisi au media

Baada ya hapo ndipo tukaanza kuona first lady wakiwa na taasisi. Kazi zao hazikuainishwa kikatiba lakini wana majukumu 'ya kitaifa'.
Ni kama utamaduni tumeiga lakini hatujautengenezea taratibu zitakazo fit na jamii yetu.
Ndiyo maana kila mmoja anakuja na taasisi yake na akiondoka anaondoka nayo

Sasa unapouliza ajira zao, sky, ajira ni ili ikupe mkate wa siku. Labda nikuulize wewe Sky Eclat , ikiwa unafanya kazi sasa hivi na unapewa milioni 2 kwa mwezi, halafu kukawa na majukumu mengine yanayokuhakikishia milioni 10 kwa mwezi, utaitizama ajira yako kwa masikitiko?
 
Asante kwa ufafanuzi huu mkuu Nguruvi3. Swali ni kuwa mfano mimi mpika chapati nilieajiriwa na DDC, 2020 Asprin ameibuka mshindisasa ule mkataba wangu na DDC unavunjwa na kuingia mkataba mpya maana Nani atakuwa na guts za kuuliza kama ule mshahara wa DDC bado unaingia kwenye account yangu?
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,637
2,000
Asante kwa ufafanuzi huu mkuu Nguruvi3. Swali ni kuwa mfano mimi mpika chapati nilieajiriwa na DDC, 2020 Asprin ameibuka mshindisasa ule mkataba wangu na DDC unavunjwa na kuingia mkataba mpya maana Nani atakuwa na guts za kuuliza kama ule mshahara wa DDC bado unaingia kwenye account yangu?
Kuna ajira za umma, na ajira za mkataba. Ukiwa katika ajira za umma kama Mwalim, Daktari nikimaanisha mwajiriwa unaweza ku-resign tu hakuna tatizo. Utafanya hivyo ukijua kwa namna fulani umevunja mkataba mwenyewe na hakuna malipo ya ziada

Ukiajiriwa na DDC na Mzee akaulamba, itategemea mkataba na DDC kuhusu chapati ukoje
Katika mkataba kuna pande mbili, ya mwajiri na mwajiriwa na mkataba lazima useme ikitokea kuuvunja nani anawajibika na kwa eneo gani.

Kama DDC hawataridhika uhamie jumba kubwa kwa kuchelea hasara utawajibika kuwalipa kulingana na mkataba

Nani ana guts za kuuliza hilo ni tatizo la mwajiri,akiridhia hewala, akiona mawaa ana haki ya kisheria kuuliza. Hapa guts zipo kwa mwajiri na si mwajiriwa
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
15,222
2,000
...kuingia mkataba mpya maana Nani atakuwa na guts za kuuliza kama ule mshahara wa DDC bado unaingia kwenye account yangu?
Sasa nimeelewa lengo la uzi wako. Kwa maelezo ya mwalimu wangu juu ya hoja yako, nadhani ingekuwa vyema Waziri wa masuala ya utumishi aandae muswada na kuupeleka bungeni unaolega kutambua cheo hiki rasmi na majukumu yake yaanishwe kiutumishi. Kama waziri wa mambo ya Utumishi hawezi basi waziri wa katiba na sheria apeleke mapendekezo ya kuboresha katiba ili kichomekwe kifungu cha kutambua majukumu ya 'First Lady' wa taifa.
 
Last edited:
Top Bottom