Ila baba nae anakaa mbali sana na mama yetu, mbona ma first lady huwa wanakuwa close!?

Status
Not open for further replies.

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,032
2,769
Mama yetu Yuko poa sana Kwa Sasa . Mcheshi ,mpole na ana chapa kazi kweli kweli. ila Sasa baba yetu haijulikani kapotelea wapi. . Misafara kama hii ya ziara za mikoani ilitakiwa baba anakuwa closed na mama! Si mnaijua baridi ya njombe? au ni namna gani wajameni .! Mama anakwenda , congo , marekani, ubelgiji, Kenya.

Kwanini aende peke yake? Au sheria inambeba first lady pekee? Maana ma first lady wanafanya mpaka ziara, wanatambulishwa Kila Mahali, mbona kama sisi wanaume tunaonewa ikifika zamu yetu? Au ndio ubaguzi .kumbuka mama Salma na mama janeth walivyokuwa wanaupiga mwingi. .Kwanini first gentleman mfumo haumbebi?

Naona sisi wanaume tunabaguliwa haiwezekani . Mama yetu bado mdogo na pia hata angekuwa Mzee hawezi kujitenga na baba Kwa sababu ya madaraka!!!! Ndoa lazima iheshimiwe . ,watu wa protocol, mkalisheni chini mama yetu msimuogope ,.Katiba yetu inataka Rais wa kiume awe na mke !

Na vivyo hivyo akitokea Rais mwanamke awe na mume. .mwambieni mara Moja Moja basi awe anasafiri nae .au anabana matumizi? Mh Sasa mbona anasafiri na mawaziri ? Hapana bwana kuna jambo haliko sawa .watafutwe wazee wa hekima wamuweke chini huyu mama yetu tunapenda couple iwe still alive! Nb,,hapa nazungumzia mama yetu malkia Elizabeth wa uingeleza msije mkaninukuu vibaya
 
Naongezea hapo. Hata Namba 3 naye nasikia eti alishikishwa pingu (kwa lazima?) alipoutwaa ufalme wa Uingereza.
 
kwel. wanawake wa Africa wakifanikiwa tu bas anaona ameshamaliza kilakitu, hataki mume anatakaga aishi peke yake. na ingekuwa wanapata mimba bila mwanaume bas wanaume tusingekuwa na chetu.
Umenifurahisha sana hapo!
Maana kwa wenye maish yao, hilo tu ndio la muhimu
 
Mkuu Mganguzi, hakuna ibara yoyote ya Katiba yetu inayomtaka Rais/mgombea wa Urais awe na mke/mume. Maoni yangu juu ya hoja yako ni inawezekana kuna masuala ya kiimani au kifamilia katika jambo hilo. Tuheshimu mambo yalivyo. Ni hayo tu mkuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom