First born msichana theory.........

mimi sijawahi kusikia,ila nimewahi mtoto akinyonya ziwa la mama anakua na huruma kwa mama,sasa sijui kama ni kweli siamini kiivyo,ila watu wanasema watoto wa kike wanakuwa na huruma kwa mama zao kuliko wa kiume
 
Jamani nimekutana na watu wengi sana sasa wanaoamini kuwa

familia zinazoanza na first born msichana huwa zinapata bahati au baraka zaidi hasa

kwenye kipato......

Katika mazungumzo na watu....nimekuja kugundua kuwa hii imani ipo kwenye baadhi ya

jamii hasa pwani zanzibar,pemba,na jamii za wahindi pia....

Kuna dokta mmoja aliniambia yeye alipozaliwa mtoto wake wa kwanza msichana

akapata scholarship nje.....

Halafu mkewe akajifungua watoto wakiume watatu na hakusafiri tena

mpaka mkewe alipojifungua msichana tena....

Na wengine wanasema ndoa ikianza na mtoto wa kiume ni ishara ya matatizo

kwenye familia wakati wa kike ni ishara ya neema....

Swali hapa je umewahi kukutana imani hiii???????

Unalionaje hili jambo ukilinganisha na watu unaowajua
wenye watoto wa kwanza wasichana na wenye watoto wa kwanza wavulana???????

Hii imani inatumika pia kwa wenye wake wengi au ?
Maana unaweza ukaanza na mke wa kwanza wote kazaa wanaume
Ukaja kuongezea wa pili akaanza na wakike.

Ila kwa vyovyote itakavyokuwa sijawahi hata kuisikia
Inawezekana kuna watu wamezaa midume tupu siku hizi lakin wanakula safari za nje mpaka passport inaomba msamaha so labda itakuwa imekosa nguvu sana ya ukweli siku hizi ndio maana haijaenea sana mpaka wengi wakakosa kuijua
 
Sikulijua hili; ila kwetu wa kwanza ni msichana amekuwa msaada sana ktk familia, na kwa bahati nzuri na mimi mtoto wangu amezaliwa tarehe 09/01/2011 ni wa kike.
kwa taarifa hizi zinanipa raha ukizingatia ninampango wa kuomba sponsorship ya kufanya masters naweza nikapata
 
Mh la neema na maendeleo ya familia nakukatalia kwa uzoefu wangu, ila kwa matatizo sijui sasa unaongelea matatizo yepi boss, sababu matatizo mengine ni ya kawaida kwenye ndoa na watu wengi wanayapitia.Labda kama umefanya utafiti kuhusu hili,sikuwa nalijua au kulisikia kabla
 
duh! hiyo ndio naisikia leo, ila kwa kule kwetu aisee ukipata first born men ndio unathaminika zaidi, watachinja mbusi sa kumvalisha mtoto (vichonyi) na vijisherehe visivyokuwa na kichwa wala miguu na ukifuliliza watoto wengi wa kike tu mmeo anatoka nje ya ndoa kutafuta wa kiume!
 
I mithi u
 
Mimi nawajua watanzania nawahindi wenye imani hii....
Nafikiri ni universal...........

Mkuu Boss hii na mimi pia nimeshasikia kuhusu hii kitu lakini sikuifuatilia kwa undani zaidi kuona ukweli wake. Ingawaje nilifanya utafiti wa juu juu ambao siwezi kuuita kama ni scientific research kwa ndugu, rafiki na jamaa wachache ambao walijaliwa kuwa na mtoto wa kwanza wa kike. Kwa hao wachache hili la kuwa na baraka na bahati katika maisha yao kweli lilikuwepo lakini sijui baraka hiyo inahusiana vipi na kupata mtoto wa kwanza ambaye ni Mwanamke.
 
MTOTO NI MTOTO: Ninachojua mtoto wa kike wa kwanza hua anakumbuka sana familia yake, tena anapokua ana uwezo anapenda majukumu yote ayabebe yeye kuanzia wazazi mpaka ndugu zake. Mtoto wa kiume ni kwa muda mfupi tu atasaidia au hatakumbuka hata kuwasiliana na madingi hata kwa sms, tofauti na wakike anajua habari zote za home hata kama yuko mbali. Ila hizo imani zingine za hao wapemba na waindi ni imani za kichawi tu na miungu yao wanayoabudu.
 
duh! hiyo ndio naisikia leo, ila kwa kule kwetu aisee ukipata first born men ndio unathaminika zaidi, watachinja mbusi sa kumvalisha mtoto (vichonyi) na vijisherehe visivyokuwa na kichwa wala miguu na ukifuliliza watoto wengi wa kike tu mmeo anatoka nje ya ndoa kutafuta wa kiume!

Du!, After reading your comment, i I was about to ask, wewe ni mtu wa__________and then I saw your signature nikapata jibu.
 
Ohh dear either way I'm prepared.
would love 3boys 1st then a baby girl...
I mean all 4at once ..lol
I think what you wrote up there is just a myth...
 
hmmm sijawahi sikia ila kama vile kuna ka ukweli.
all in all mafanikio yapo popote hata usipopata mtoto.
 
Imani tu hizi sidhani kama kuna uhusiano mbona mimi wa nne kuzaliwa watatu wote ni dada zangu na hakuna kitu kama hicho
 
Jamani nimekutana na watu wengi sana sasa wanaoamini kuwa

familia zinazoanza na first born msichana huwa zinapata bahati au baraka zaidi hasa

kwenye kipato......

Katika mazungumzo na watu....nimekuja kugundua kuwa hii imani ipo kwenye baadhi ya

jamii hasa pwani zanzibar,pemba,na jamii za wahindi pia....

Kuna dokta mmoja aliniambia yeye alipozaliwa mtoto wake wa kwanza msichana

akapata scholarship nje.....

Halafu mkewe akajifungua watoto wakiume watatu na hakusafiri tena

mpaka mkewe alipojifungua msichana tena....

Na wengine wanasema ndoa ikianza na mtoto wa kiume ni ishara ya matatizo

kwenye familia wakati wa kike ni ishara ya neema....

Swali hapa je umewahi kukutana imani hiii???????

Unalionaje hili jambo ukilinganisha na watu unaowajua
wenye watoto wa kwanza wasichana na wenye watoto wa kwanza wavulana???????

ni imani tuu mkuu!mwanangu wa kwanza ni wa kiume na tumebarikiwa kwa mambo makubwa sana!bado sijapata mwingine ila navyoelewa haihusiani na baraka mlizoandaliwa.watu wafanye kazi kwa bidii wakimtegemea Mungu
 
ni imani za watu na uongo tu, kwetu first borne ni wa kiume lakini baraka zimejaa tele, na tuna ndugu, marafiki na majirani kibao wenye mafirst borne wa kike wamebaki kuzishangaa baraka za nyumbani kwetu!

mtoto ni mtoto na wote ni majaliwa na zawadi za Mungu. furahini siku zote na mshukuruni Mungu kwa kila jambo na ombeni bila kukoma, maana hayo ni mapenzi yake (1 Wathesalonike 5:16-18).

Glory to God
 
Mimi naona kama kuna kauhusiano maana.........nimejipima nikagundua!! Kunamabadriko fulani!!
 
Back
Top Bottom