Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,833
- 2,790
Toa pole kwanza, ndio uulize. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali panapostahili. Amen
Unilever ni Kampuni gani hiyo?
Nawapa pole wafiwa
Kianachonisikisha zaidi ni huu utambaji wa viongozi wa Polisi hasa wanaokuja Mkoa wa Dar es Salaam, utadhani wao ndio muarobaini wa jinai zote jijini. Huyu wa sasa anatamba mpaka leo kuwa majambazi, vibaka na wapiga debe wakae mkao wa kula. leo ni siku mia moja tangu afike lakini majambazi wapo, vibaka kibao na wapiga debe wamejazana vituoni. Polisi wenye pikipiki wapo lakini kazi ni kufukuzia maroli yaliyopakia mizigo barabarani.
Ndo maana mi Bongo nshaamua ntakuja kutembea tu lakini siwezi rudi kuishi, yani watu wanakuwa victims of their own success, haka ka gari kangu ninakoendesha huku mamtoni ndio kanaweza kakawa msiba wangu huko, hiki ki selula changu kitakuwa ndio chanzo cha mauti yangu, nikiwa na drive kurudi home litakuja jitu na mgari wake lina leseni ya kununua halafu limelewa bwii na kuniparamia, nikienda hospital hata kama nina hela zangu naambiwa dawa hakuna na kama zipo kuna uwezekanio zikawa fake! no! no! no! sirudi ng'oooooo!
Pole sana wafiwa, Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
Nawapa pole wafiwa
Kianachonisikisha zaidi ni huu utambaji wa viongozi wa Polisi hasa wanaokuja Mkoa wa Dar es Salaam, utadhani wao ndio muarobaini wa jinai zote jijini. Huyu wa sasa anatamba mpaka leo kuwa majambazi, vibaka na wapiga debe wakae mkao wa kula. leo ni siku mia moja tangu afike lakini majambazi wapo, vibaka kibao na wapiga debe wamejazana vituoni. Polisi wenye pikipiki wapo lakini kazi ni kufukuzia maroli yaliyopakia mizigo barabarani.
Bongo longolongo nyingi, polisi wanajisifu badala ya kusifiwa na wananchi wanaowatumikia!.
Nimeambiwa hao majambazi walitumia pistol kutoa roho ya Ndg Lugano, na hawakuchukua chochote!
Inawezekana ni chuki binafsi, au kweli walikuwa na nia ya kuiba ila hawakufanikiwa, maana naambiwa wamempiga risasi mbele za watu wengi! Kazi kwenu Polisi, tunataka muwakamate hao wauwaji hatutaki yaani yaani!
Mungu amrehemu Lugano na awape subira ndugu na jamaa wote waliokuwa karibu siku za uhai wake! Amen