Fikra Pevu: Lowassa alipwa mamilioni na Wasomali

Fikra Pevu: Lowassa alipwa mamilioni na Wasomali

Kiongozi asiyeweza kujitafutia maendeleo yake hawezi kulitafutia taifa. Viva Lowasa
 
Tamaa haimaanishi usifunguwe kampuni. Mbona Mbowe ni kiongozi aw upinzani bungeni na ana makampuni na miradi kedekede, hatujasikia hata siku mkimsema humu. Hata alipowauzia mafuso used kwa bei zaidi ya mapya mlikaa kimya.

FF,
Hapo kwenye Red ni uwongo wa Mchana, Tafuta hoja nyingine kuhusu Mbowe, ukweli ni kwamba tulimlipa Mbowe Fuso zikiwa zimechakaa na tumezichakaza sisi wenyewe. Tulipewa zikiwa mpya ila hatukuwa na fedha za kumlipa. Tulimlipa zikiwa zimechakaa. Hazikuchakazaa kwa kubebeshwa mbolea kwenye shamba la Mbowe, bali tulizitumia kuwaelimisha watz na tukapata kura. Labda ungesema Chadema tumshukuru Mbowe kwa kutodai riba japokuwa tumemcheleweshea malipo yake kwa muda mrefu sana.

Pili, nimekuona kama unachuki binafsi na Mbowe, au kwa vile uongozi wake ndio uliokifikisha chama usichokipenda hapo kilipo? Na kwa umakini huu wa Mbowe kuna dalili zote kwamba mwaka 2015 ccm na CUF watakuwa vyama vya upinzani. No way out - take it from me, na uchakachuaji utakuwa mgumu sana - wananchi wameamka
.
 
Ibara ya 17 Katiba ya CCM ya mwaka 1977 iliyochakachuliwa mwaka kwa mara ya mwisho mwaka 2007 inasema hivi kuhusu kiongozi.

Pamoja na kutimiza masharti ya uananchama kama yalivyoelezwa katika Katiba. Kiongozi sharti pia awe na sifa sifuatazo:-
  1. Awe ni mtu aliyetosheka na asiwe mtu aliyetawaliwa na tamaa
  2. .........
  3. ......
Wanachojadili watu hapa ni tamaa aliyonayo huyu waziri mkuu mjiuzulu.

Utamtambuaje kiongozi alie ridhika? Hebu nitajie mfano wa mmoja wapo katika viongozi wa nchi hii.
 
Utumiage akili, najua unazo nyingi, usitukwaze kwa maksudi, we una poa tukiibiwa na lowasa kupitia madaraka yake kwa utumishi wa uma!


Kama kunakiongozi katika siasa za CCM na serikali yake ambaye hafanyi kama haya afanyayo LOW ASSa na awe wa kwanza kumshutumu sasa. AMEN
 
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu kwa kutajwa katika kashfa ya mdadi wa umeme uliohusisha kampuni tata ya Richmond Development LLC, Edward Lowassa, amelipwa mamilioni ya fedha na wafanyabiashara wa Kisomali, Fikra Pevu imethibitisha.

Uchunguzi wa muda mrefu wa Fikra Pevu umeonyesha kwamba Wasomali hao kupitia kampuni ya Integrated Properties Investment (T) Limited walimlipa Lowassa Sh milioni 450 kupitia kampuni yake ya Barare Limited. Malipo hayo yalielezwa kuwa ni deni ambalo Lowassa kupitia Barare alikua akiidai kampuni hiyo ya Integrated ambayo kwa Tanzania imekuwa ikijihusisha na uwekezaji katika majengo.

Uchunguzi wa Fikra Pevu umethibitisha kwamba malipo hayo yalifanyika miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, na Lowassa na mkewe Regina Mumba Lowassa, walikubali malipo hayo kwa kupewa hisa 7,500 zikiwa na thamani ya Sh 60,000 kwa hisa moja.

Kwa nyaraka na habari zaidi: Wasomali wamlipa Lowassa milioni 450, wampa hisa | Fikra Pevu | Kisima cha busara!

Jamani mboya haya ni mambo binafsi sana ndugu zangu?
 
Naona kama kawaida yetu naona tumeacha kujadili mada na kuanza kushambuliana. Itakuwa better tuache kumjadili Lowassa kama individual na tujadili wafanyabiashara kwa ujumla wao(Ndesa Pesa, Mbowe, Hamad Rashid etc) na uongozi wa nchi. Kuwanyima haki watu hawa ya kuongoza nchi itakuwa ni ubaguzi na kinyume na katiba. Lakini ni katiba hiyo hiyo inayotoa haki kwa mtu yeyote kuishi sehemu yeyote ndani ya nchi hii ili mradi ASIVUNJE SHERIA. Ndio maana huwezi kwenda nyumbani kwa mtu na kusema "nitakaa hapa kwa sababu katiba inasema nina haki ya kukaa sehemu yeyote ndani ya Tanzania". Kuna taratibu na sheria pamoja na taasisi ambazo zinaakikisha pamoja na mambo mengine mtu huvuki mipaka uliyowekewa.


Binafsi sina tatizo na Lowasa kuwa rais or any other businessman for that matter. Nchi za wenzetu wanafanya hivyo, na ni vigumu kwa hali iliyopo hivi sasa kupata mtu ambaye HAFANYI BIASHARA KABISA katika jamii zetu(mimi mwenyewe ni mfanybiashara pamoja na kufanya kazi). Swala la kujadili hasa ni je tuna sheria, kanuni na taasisi ambazo zina uwezo wa kuhakikisha viongozi ambao walikuwa wafanyabiashara hawatumii madaraka yao vibaya? Kwa sababu the driving force behind every businessman is GREED and PROFIT MAKING and in most cases AT ANY COST.Wenzetu wana vyombo vya kuhakikisha hao viongozi wafanya biashara hawatumii madaraka vibaya, Do we have the necessary institutions that will ensure that they dont use their power for their own benefits?


Jambo muhimu la kukumbuka ni kwamba serikali hasa kwa nchi zetu hizi ni kama "mungu mtu" na marais ndio "miungu kabisa". Mkapa alianzisha benki akiwa ikulu na akajimilikisha mgodi kwa bei ya kutupa leo hii hakuna alichofanywa na anaendelea kupeta na kutuita "wavivu wa kufikiri". Tena huyu hakuwa mfanyabiashara kabla hajaingia madarakani. Vipi hawa ambao wamezaliwa kwenye familia za wafanyabiashara wa kutupwa. Jamani "mbuzi" na "simba" wote ni wanyama lakini unapo-deal na "simba" lazima uwe makini kuliko "mbuzi" la sivyo utakufa.


Mimi nionavyo ni kwamba bado hatujafika huko kwenye uwezo wa kumdhibiti mfanyabiashara aliye ikulu, kama hii story ni kweli inamuhusu Lowasa kama wasemavyo, tujiulize mtu ambaye ni akiwa MBUNGE tu anaweza kusimamisha uchapishaji wa gazeti ambalo lina habari yake mbaya, vipi akija kuwa RAIS?? Si tutabakiwa na gazeti la UHURU na MZALENDO pekee!!


Tuwe makini tusije weka mtu akajimilikisha mlima Kilimanjaro wote, au akafanya biashara ya madisko yote kuwa yake au akajimilikisha Masaki yote iwe yake. TUSIWAZUIE ILA KAMA HATUNA MBINU ZA KUWABANA TUWAKATAE.
 
Mbowe na Ndesamburo wote wana kampuni nyingi tu hapa nchini, tukianza kutoa mikataba wanayaoingia kila siku hapa JF hapatatosha.
kwanza sioni mantiki ya hii habari kuletwa hapa JF, nilikuwa nategemea mods wangekuwa wameshaiondoa...

Wahenga walisema! nyani haoni kundule. Hili sio tusi, ni usemi wa kiswahili.

Ama kweli watanzania wengi sasa akili zao zinazeeka kabla ya mwili. Hivi kuna kosa gani kwa mtu kuwa na kampuni iliyosajiliwa kihalali? kuna kosa gani kwa mtu kulipwa deni halali? Ni upuuzi kuweka post hapa kwa lengo la kumshutumu mtu ikiwa haina ushahidi wa ubatili wake. Tangu siasa ya ujamaa na kujitegemea kufa, na kuja kwa soko huria. Biashara imekuwa haina mipaka tena. Mradi iwe halali tu, bila kujali nani anafanya biashara hiyo.

Nilitegemea utatuwekea nyaraka zinazoonyesha uharamu wa biashara za EL matokeo yake kumbe ni biashara halali, kosa liko wapi? Hivi vitega uchumi vya hao viongozi wa upinzani na makampuni yao hamviaoni? Wanasiasa wengine wengi tu wenye makampuni hamuwaoni? Acheni wivu wa kijinga. Nchi huru hii, soko huru pia. Hakuna anayekuzuia kuwa na kampuni, hakuna anayekuzuia kuwa na nyumba wala shamba. Ilimradi umevipata kwa njia halali. Wapo wanaosema tunachukua bahasha, upuuzi huo.
 
nimesikia mtunzi mmoja wa vitabu akieleza misaada ya wazungu kwa nchi masikini kuwa ni "kunyanganya masikini wa nchi zilizoendelea na kuwagawia matajia wa nchi masikini".
Ndicho ninachothibitisha hapa, ni unabii unatimia mkuu ..."mwenye nacho anaongezewa na asiye nacho....". Alafu uje useme Osama, Joseph Kony nk hawajui wanachopigania!
Tina na Wana JF,

Duh kwa mwendo huu, tunatakiwa kusema, Mimi sina hela, pesa, mapene na sio Sisi, Watanzania hatuna pesa, hela, mapene.

Nawasilisha
 
FF,
Hapo kwenye Red ni uwongo wa Mchana, Tafuta hoja nyingine kuhusu Mbowe, ukweli ni kwamba tulimlipa Mbowe Fuso zikiwa zimechakaa na tumezichakaza sisi wenyewe. Tulipewa zikiwa mpya ila hatukuwa na fedha za kumlipa. Tulimlipa zikiwa zimechakaa. Hazikuchakazaa kwa kubebeshwa mbolea kwenye shamba la Mbowe, bali tulizitumia kuwaelimisha watz na tukapata kura. Labda ungesema Chadema tumshukuru Mbowe kwa kutodai riba japokuwa tumemcheleweshea malipo yake kwa muda mrefu sana.

Pili, nimekuona kama unachuki binafsi na Mbowe, au kwa vile uongozi wake ndio uliokifikisha chama usichokipenda hapo kilipo? Na kwa umakini huu wa Mbowe kuna dalili zote kwamba mwaka 2015 ccm na CUF watakuwa vyama vya upinzani. No way out - take it from me, na uchakachuaji utakuwa mgumu sana - wananchi wameamka
.

Mbowe anafanya biashara na makampuni yake. Hamsemi, mnatetea kwa nguvu zote. Wengine wakifanya biashara zao, kosa kubwa. Mnalalamika, huu ni ujinga kwa kweli. Ya nini kuingilia mambo binafsi ya mtu. Kama Lowasa anafanya biashara halali, mwacheni. Acheni wivu wa kijinga.
 
FF,
Hapo kwenye Red ni uwongo wa Mchana, Tafuta hoja nyingine kuhusu Mbowe, ukweli ni kwamba tulimlipa Mbowe Fuso zikiwa zimechakaa na tumezichakaza sisi wenyewe. Tulipewa zikiwa mpya ila hatukuwa na fedha za kumlipa. Tulimlipa zikiwa zimechakaa. Hazikuchakazaa kwa kubebeshwa mbolea kwenye shamba la Mbowe, bali tulizitumia kuwaelimisha watz na tukapata kura. Labda ungesema Chadema tumshukuru Mbowe kwa kutodai riba japokuwa tumemcheleweshea malipo yake kwa muda mrefu sana.

Pili, nimekuona kama unachuki binafsi na Mbowe, au kwa vile uongozi wake ndio uliokifikisha chama usichokipenda hapo kilipo? Na kwa umakini huu wa Mbowe kuna dalili zote kwamba mwaka 2015 ccm na CUF watakuwa vyama vya upinzani. No way out - take it from me, na uchakachuaji utakuwa mgumu sana - wananchi wameamka.

Huyu chuki yake kwa Mbowe ni dini ya Mbowe, FF ni adui wa Ukristo na Wakristo.
 
Mbowe na Ndesamburo wote wana kampuni nyingi tu hapa nchini, tukianza kutoa mikataba wanayaoingia kila siku hapa JF hapatatosha.
kwanza sioni mantiki ya hii habari kuletwa hapa JF, nilikuwa nategemea mods wangekuwa wameshaiondoa...
Mbowe na Ndesa wameanza BIASHARA kisha wakaingia SIASA; Lowasa kaanza SIASA kisha kaingia BIASHARA. Siasa inakupaje mtaji wa biashara kubwakubwa hivi?
 
Watu wengi wamefanya business transactions na wamelipwa. Kwa nini umtaje Lowassa?
 
Jamani mimi sioni tatizo hapo kama ni biashara viongozi wote wanaruhusiwa kufanya na wanafanya, na kama ni ukubwa gani wa biashara hakuna kikomo kilichowekwa. Sasa lowassa anawatisha nini na vibiashara vyake vya millions na sio trillions. Kama amehujumu toeni ushahidi na mumpeleke mahakamani. Kama amumtaki akigombea msimpe kura muone kama atashinda. Poleni sana kwa hofu zenu. Mimi nitamchagua yule ninayemtaka hata kama kuna majungu vipi sibadilishi maamuzi.
 
Jamani i don't see any problem there, kama kuna mtu kaona anionyeshe nini tatizo.
Ta

tizo ninaloliona mimi ni je hii biashara ni halali?.Taifa linanufaika vipi na biashara hizi?.Was this income declared by Lowasa to Tra for taxation?.
 
bila shaka hii pesa itatumika kuwapa watu bahasha za kaki..watu gani? kuna uzi umeanzishwa na Lunyungu unaeleza kuhusu hawa wapokea bahasha za kaki..
Ebu acheni kutangaza u-kihiyo wenu. Lowassa hajapewa hizo fedha. Kilichofanyika ni kufutwa kwa deni ambalo kampuni yake (Barare) ilikuwa inadai kampuni ya Integrated na badala yake Barare (na kwa hiyo wanahisa - Lowassa na Regina) kupewa hisa 7,500 katika kampuni ya Integrated zenye thamani ya Shs.450m/= basi. Hili kitaalamu linaitwa Debt Conversion. Hizo hisa zinaweza kuwa pesa taslimu kama Lowassa na Regina wataamua kuziuza kwa mtu mwingine. Vinginevyo ni makaratasi tu.
 
Wale waliokuwa na maswali kuhusu nguvu yake ya hela wasome hati ya malipo kwenye hiyo attachment...kweli kukosekana kwa ajira ni bomu linalotarajiwa kulipuka wakati wowote.....hivi wanajua kweli tunavyoumia kwa kukosa hata hela ya panadol wakati mwingine??

Ni panadol tu au mpaka mambo mengine ya lazima hela haionekani? we acha tu
 
Hivi kuna biashara gani ambayo mnadhani Lowassa hafanyi?kwa taarifa yenu mpaka hizi issue za uharamia kwenye pwani ya somalia jamaa ana mkono kwa kushirikiana na hao hao maswahiba wake wa kisomali,nyie hii ndio mnaijua leo,mbona hii cha mtoto..

toa evidence> usirukie tu. mi sioni shida ya hiyo. iyo kampuni yake, kwani haruhusiwi? bora ana kampuni halali na inajulikanika kuliko wale wanaoweka majina feki
 
Back
Top Bottom