Fikra Pevu: Lowassa alipwa mamilioni na Wasomali

Sasa jambo hili la Mzee Lowassa na MALIPO KUTOKA 'SOMALIA' ni chagizo kubwa sana akilini ili Great Thinkers, kwa utulivu wa akili sana tu, kwa pamoja tuvuke utaratibu huu wa kufikiri tu ndani ya boksi moja tu na sasa tuanze kutafakari ki-undani zaidi kwamba URAFIKI WA HALI YA JUU kati ya Lowassa na Rostam Aziz, ni kitu gani hasa hicho kinachowaleta pamoja na kwa maslahi gani hiyo???
 
Wale waliokuwa na maswali kuhusu nguvu yake ya hela wasome hati ya malipo kwenye hiyo attachment...kweli kukosekana kwa ajira ni bomu linalotarajiwa kulipuka wakati wowote.....hivi wanajua kweli tunavyoumia kwa kukosa hata hela ya panadol wakati mwingine??

Michelle ! mimi binafsi sioni tatizo la lowasa kwani kalipwa na wasomali, nilizani apongezwe kwa kuwa kichwa na fighter wa ukweli
 
Uwezo Tunao
Ndo ujue unafiki wa habari yenyewe, kama mwandishi aliweza kuijua kampuni hiyo kwa jina, kwa nini ameshindwa kueleza inajihusisha hasa na nini, basi hata angetudanganya kwa kutuambia kuwa hadi anamaliza uchunguzi wake 'Hajajua kampuni ya Lowassa ililipwa kwa ajili ya issue gani' au 'inajishughulisha na mambo gani'
Habari hiyo ipo nusu nusu..
 
Last edited by a moderator:
Hii habari ni ya siku nyingi sana. Nyie ndio mnaishushia hadhi JF. Hebu mod ondoeni huu uzi!!!

Rejao hapa hakishushwi kitu mpaka watanzania wajue, kwani kila siku JF inapata member wapya, ningeshauri hata magazeti hii story wairudie wakati muafaka wa uchaguzi mwezi wa Oktoba
 
Kukiukwa kwa maadili ya uongozi ndio matatizo makubwa sana yanayoiangamaiza nchi yetu. Hawa mafisadi waliojivalisha ngozi ya uongozi huiuza nchi yetu taratibu kwa kupewa hisa katika makampuni mbali mbali nchini na hivyo kutojali kabisa maslahi ya nchi.

Kama hii kampuni ya wasomali ni kampuni halali kwa nini washindwe kwenda kuomba mkopo katika mabenki mbali mbali ya biashara nchini na wakaombe mkopo kwa fisadi Lowassa? Asilimia kubwa ya wafanyabiashara wa kisomali sehemu mbali mbali duniani wanahusika na biashara haramu zikiwemo uuzaji wa madawa ya kulevya, utekaji wa meli, uuzaji wa nyara za Serikali.

Huyu Lowassa ana nafasi ya juu sana Bungeni kama Mwenyekiti wa kamati ya usalama na ulinzi wa Taifa na pia mgombea mtarajiwa wa magamba pamoja na kuwa hajatangaza rasmi nia yake ya kufanya hivyo 2015. Hizi tamaa tamaa za utajiri wa haraka haraka zinaweza kabisa kumsababisha kuingia kwenye mikataba ambayo ataweka mbele maslahi yake badala ya maslahi ya nchi. Maswali niliyoyauliza katika thread hii ni lazima yajibiwe na vyombo mbali mbali husika ikiwemo hiyo kampuni ya wasomali na Lowassa mwenyewe.

Kama hakuna uchafu katika utoaji wa mkopo huo wa shilingi 450 millioni basi sioni kwa nini Lowassa ashindwe kujisafisha hasa ukitilia maanani wingu zito lililotanda kwa fisadi huyu kuhusiana na mkataba wa Richmond/Dowans na jinsi alivyoibuka katika kipindi kifupi na kuwa bilionea wakati miaka michache iliyopita hakuwa na utajiri wowote. Tusiache kuwakemea hawa mafisadi waliojivisha ngozi ya uongozi kutumia nyadhifa zao kubwa walizokabidhiwa na Watanzania kuendelea kujali maslahi yao na kujitajirisha kwa njia za haramu huku nchi ikiendelea kuangamia.



kwani wasomali wanashindwa kuwa na uwezo wa kuwa na kampuni kwa njia halali hapa nchini mkuu! mbona wapo wasomali kibao nnchi za watu huko ulaya na marekani na wanamakampuni pia! mbona hata watz wapo wengi wanaekeza huko nje na kwa hela za haramu na wengine za halali pia! yani nnchi kama somalia ikose watu wa uhalali wa kumiliki cumpini amabay ianaweza kulipa deni la mil 450 tu mkuu! skatai wapo wale wa haramu na wa halali, tuangalie pande zote mbili mkuu wangu
 
From Wikipedia

Omar Abdi Ali is a Somali entrepreneur, accountant, financial consultant, philanthropist, and a leading specialist on Islamic finance.[1] From 1986 to 1999, Omar was CEO of Dar al-Maal al-Islami Trust (DMI Trust), a Middle Eastern financial and banking group, which under his management increased it assets from $1.6 billion USD to $4.0 billion USD. He is currently the chairman and founder of the multinational real estate corporation Integrated Property Investments Limited and its sister company Quadron Investments.

Omar graduated in 1964 as a certified accountant from the Leeds College of Commerce in the United Kingdom. He returned to Somalia, where he joined the Ministry of Finance and became a Deputy Accountant General. He also assumed the role of Director of Finance in the African Development Bank Group, where he took part in transforming the pilot project into a multi-regional project.

From 1974 to 1983, Omar would take up positions in the Gulf States and Europe as a financial consultant. In 1983, he became CEO of the Islamic financial institution the DMI Trust based in Geneva, Switzerland. Under his tenure, DMI became a leading Islamic Financial Institution and its assets increased from $1.6 billion USD to $4 billion USD, with Omar managing a worldwide staff of 1,400 employees in three continents.[2] He became Vice-President of the Bahraini Faisal Private Bank,[3] and established their most profitable branches in Pakistan, Switzerland and New Jersey in the United States.

In 2009, Omar together with his business partner Suleiman A. Dualeh entered an agreement with Shelter Afrique that will see their corporation Integrated Property Investments Ltd take on an ambitious housing project worth $624 million USD in Dar es Salaam, Tanzania known as the Bahari Beach satellite town.[4]
 
Kama ni biashara halali.....analipa kodi kwa stahili.....anaweka katika mabenki yetu mie sina tatizo na hili....mbona kuna wanasiasa wengi tu wana utajiri wa kutisha....palipo na ukweli tubaki wakweli...tusiwe na wivu kwani tuliliuwa wenyewe Azimio la Arusha
 
Hii ni network ya Bwn Lowasa kuibia taifa maskini la Watanzania!!!!!!!!!!!!!!!!


Kweli Njaa mbaya. Haya ni maeneno ya kijinga. Yamejaa wivu na chuki. Fanyeni kazi. Wenzeni wanazitafuta. Nyinyi mnatunga hadithi za uzushi. Loooo wajinga ndiyo waliwao.
 
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu kwa kutajwa katika kashfa ya mdadi wa umeme uliohusisha kampuni tata ya Richmond Development LLC, Edward Lowassa, amelipwa mamilioni ya fedha na wafanyabiashara wa Kisomali, Fikra Pevu imethibitisha.

Uchunguzi wa muda mrefu wa Fikra Pevu umeonyesha kwamba Wasomali hao kupitia kampuni ya Integrated Properties Investment (T) Limited walimlipa Lowassa Sh milioni 450 kupitia kampuni yake ya Barare Limited. Malipo hayo yalielezwa kuwa ni deni ambalo Lowassa kupitia Barare alikua akiidai kampuni hiyo ya Integrated ambayo kwa Tanzania imekuwa ikijihusisha na uwekezaji katika majengo.

Uchunguzi wa Fikra Pevu umethibitisha kwamba malipo hayo yalifanyika miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, na Lowassa na mkewe Regina Mumba Lowassa, walikubali malipo hayo kwa kupewa hisa 7,500 zikiwa na thamani ya Sh 60,000 kwa hisa moja.

Kwa nyaraka na habari zaidi: Wasomali wamlipa Lowassa milioni 450, wampa hisa | Fikra Pevu | Kisima cha busara!

SO WHAT IS THE PROBLEM WITH THIS?MLITAKA IWEJE YAANI?MWACHENI JAMANI ALIYE WAHI KAWAHI NANYI TENGENEZENI BOMU LENU MLIPUE MTOKELEZEE KAMA RAISI AJAYE lowassa NGOYAYE EDWARD
 
Hapo pana dalili zote za money laundry,

Nafikiri ndio maana hio kampuni yake Barare limited imeandika principle activities brela kuwa ni "Laundry and Dry Cleaning Services"! Hahahah!

Principal Activities za Barare Limited: "Laundry and Dry Cleaning Services" kwa mujibu wa nyaraka zake za BRELA, sasa wamefua nguo ngapi na kunyoosha za Integrated hadi wadai 450,000,000/-? tujiulize na hawa jamaa waliingia lini nchini? jamani hii ni zaidi ya RichmondView attachment 45389
 
Hivi IPTL ndo wale jamaa wanaotuzalishia umeme kwa kutumia mafuta mazito na kuifanya TANESCO kibogoyo?
 
Common sense somitimes matters...now days unaweza kusajili biashara kama stationery but ukafanya zaidi ya kazi hamsini za ziada .., na usidhani kwa uwezo wa Lowasa akafungua biashara inayoingiza laki mbili... acheni uvivu wa kifikiri
 
Acha unafiki mda wote ulikuwa wp umesubiri ameenda cdm ndo unaleta ujinga wako tangu 2o10 hadi leo umekumbuka nn na ccm harud ng'o na hata angelipwa na nani cc hatujui kura tunampa upende ucpende tena naona kama masanduku yanachelewa vile
 
2015 he was in CCM,you never dared to spell that out. #mnatapata
Ya kae hayanuki ndiomaana CHADEMA wanajisahaulisha
lakini wapo Makamanda km
banner-4.gif
http://mnyika.blogspot.com/2008/09/serikali-iache-kumlinda-lowassa.html

TAARIFA KWA UMMA

SERIKALI IACHE KUMLINDA LOWASSA

  • Ni mmoja wa mizizi ya ufisadi wa Richmond
  • Akamatwe, ahojiwiwe na achukuliwe hatua za kisheria.
Tarehe 25 Februari, 2008 Vijana wa CHADEMA tulitoa taarifa kwa u..............................................
 
Back
Top Bottom