WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu kwa kutajwa katika kashfa ya mdadi wa umeme uliohusisha kampuni tata ya Richmond Development LLC, Edward Lowassa, amelipwa mamilioni ya fedha na wafanyabiashara wa Kisomali,
Fikra Pevu imethibitisha. Uchunguzi wa muda mrefu wa
Fikra Pevu umeonyesha kwamba Wasomali hao kupitia kampuni ya Integrated Properties Investment (T) Limited walimlipa Lowassa Sh milioni 450 kupitia kampuni yake ya Barare Limited.
Malipo hayo yalielezwa kuwa ni deni ambalo Lowassa kupitia Barare alikua akiidai kampuni hiyo ya Integrated ambayo kwa Tanzania imekuwa ikijihusisha na uwekezaji katika majengo. Uchunguzi wa
Fikra Pevu umethibitisha kwamba malipo hayo yalifanyika miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, na Lowassa na mkewe Regina Mumba Lowassa, walikubali malipo hayo kwa kupewa hisa 7,500 zikiwa na thamani ya Sh 60,000 kwa hisa moja.
Uchunguzi wa muda mrefu wa
Fikra Pevu umeonyesha kwamba Wasomali hao kupitia kampuni ya Integrated Properties Investment (T) Limited walimlipa Lowassa Sh milioni 450 kupitia kampuni yake ya Barare Limited. Malipo hayo yalielezwa kuwa ni deni ambalo Lowassa kupitia Barare alikua akiidai kampuni hiyo ya Integrated ambayo kwa Tanzania imekuwa ikijihusisha na uwekezaji katika majengo.
Waraka wa Bodi ya Integrated iliyoidhinisha malipo kwa LowassaWaanzilishi wa Barare Limited
Sehemu ya nyaraka zinazohusiana na Barare Limited
Kampuni ya Barare Limited inamilikiwa na Lowassa na Regina kwa wanaoishi Mtaa wa Mahando namba 407, Masaki, Dar es Salaam, wakati Integrated ikiwa inamilikiwa na kundi la Wasomali, akiwamo
Omar Abdi Ali, ambaye ni mfanyabishara na mchumi wa Kimataifa.