Inauma sana kuo watu waliotuaminisha kua watatuletea mabadiliko ya kweli kuliko yale yaliyohubiriwa na kina Lowassa wa UKAWA, badala yake wanatuletea viongizi wanaotumia vyeti vya watu na kuwalinda kwa kuwapa ulinzi. Hili halikubaliki na hatutakubali kamwe na watanzania hatutadanganyika.
Mtu anasimama bila kuficha aibu anatumbia vyeti vya wateule wa mukulu vinakaguliwa na TAMISEMI badala ya NECTA?NECTA kazi yao nini?TAMISEMI tangu lini wafanye kazi za NECTA? Tusidanganyane hapa! Huu ni usaliti wa ajabu sana. Watanzania sasa wameshajua waliahidiwa nini,wamevuna nini na sasa hawatakua tayari tena.
Yaani inatengwa bajeti ya maendeleo trillion 11 zinatolewa trillion 3.9? Kwanin tusiseme ni bora ya Lowassa Mara 1000 na zaidi kuliko walioshindwa kutekeleza ahadi zao?Mini maaana ya TRA kukusanya trillion 1.3 kwa mwezi? Makusanyo hayo yanakwenda wapi?
Kwenye serikali ya Lowassa sitegemei kama wangeweza kufanya vioja vya kuajiri na kumlinda mtu aliyefeli akatumia vyeti vya mtu, Sidhani kama serikali ya kina LISSU wangelea mtu anayevamia ofisi za watu.
Nasema hivi watumishi wa serikali wanafanya kazi ilimradi tu liende,hawana morali ya kazi yaani wapo wapo tu. Hawapandishwi madaraja,hakuna anual increments huku gharama za maisha zikipaa.
Mpaka sasa hakuna sababu ya kutompa nchi Lowassa,hakuna anayejutia kumpa Lowassa kura yake zaidi ya wale walioipigia kura CCM 2015. Ninaomba tena na tena Lowassa akamatie kijiti kupitia UKAWA kwa maisha haya tuone kweli watanzania wanaweza kufanya kitu gani.