Fikiria leo hii Lowassa angekuwa Rais!

Fikiria leo hii Lowassa angekuwa Rais!

Huu "mtaa" nimepita kimakosa, mambo ya utabiri ni magumu aliyaweza Marehemu Sheikh Yahya Hussein. "Ningekuwa na mbawa ningeruka", ni kama kufikirika vile!!
 
Elimu ya hapa na pale toka vyuo vya hapa na pale
 
mali ipi ya umma Lowassa aliiba ?
tusimpe mbwa jina baya kama lengo ni kumuua..
tumuue tu pasipo unafiki..
muungwana hujenga hoja hatengenezi kashfa..
mbona hao washkaji feki walimpa nafasi alietumia madaraka kujibinafsishia magorofa ya umma?
mbona maalim hana skendo pia wamegoma kumpa singapore !
hawa wabunge wabadilike
watueleza ukweli panapohitajika ukweli na sio siasa..
 
Kama tungemchagua Lowassa kuwa Raisi wa wa 5 wa JMTZ unafikiri mpaka sasa hivi ni nini kingekuwa kimetokea? Unafikri wagonjwa Muhimbili wangetoka sakafuni na kuhamia kitandani? Unafikiri Lowassa, Mbowe Lisu &Co. wangeacha kutumia milioni 250 na badala yake kuzipeleka Hospitali kusaidia Watanzania? Rejea Tundu Lissu kutetea milioni karibia 300 walizokuwa walipwe kama Wabunge, je angeziacha hizi za juzi kama angekuwa na madaraka?

Unafikiri Lowasa na Mbowe wangeahirisha kuuza sura Disemba 9 na badala yake kutumia hizo fedha kwa ajili ya maendeleo?
Unafikiri Lowassa na Mbowe wangefuta safari za nje ya nchi?

Mke wa Lowassa unafikiri leo hii angekuwa kimya kama mama Janeti au tayari angeshaanzisha NGO na sia ajabu sasa hivi angekuwa yuko safari ndefu ya Marekani na Ulaya kuuza wazo lake?

Mungu bado hajachoka na sisi Watanzania anatupenda na ndiyo maana ametuongoza na tukafanya maamuzi ya busara, leo hii ukiwauliza waliompigia kura Dr. Pombe Magufuli kama wana majuto yoyote ya kufanya jibu lake ni HAPANA kubwa!

KWA KWELI MUNGU NI MWEMA SANA. KATUEPUSHA SANA NA BALAA
 
Mbona hizo tuhuma zoooote ni kama unamsema raisi aliyekaa madarakani na kuyafanya hayo uliyasema? Kama umeamua kumdharirisha mtu mtaje tu kwa jina lake direct badala ya kunguka na kupitishia tusi kwa mtu mwingine. Sema tu hivi; "Hivi kingetokea nini kama JK angeendelea kua rais wa Tanzania kwa miaka mingine 5 au 10" Ku predict ambacho kingefanywa na mtu mwingine ambaye hajaingia Ikulu kwa madhaifu yaliofanywa na umpendaye sio vizuri.
 
Wewe ni wa kudharau kama watu wanavyidharau familia yenu!
Kama huna kitu chenye akili kuchangia, peruzi mitandao mingine inayokufaa!
Na kwa kiriba cha moyo wako kunidharau, hilo ni absolutely tatizo la orientation ya boga lilo juu ya mabega yako!
 
Kama tungemchagua Lowassa kuwa Raisi wa wa 5 wa JMTZ unafikiri mpaka sasa hivi ni nini kingekuwa kimetokea? Unafikri wagonjwa Muhimbili wangetoka sakafuni na kuhamia kitandani? Unafikiri Lowassa, Mbowe Lisu &Co. wangeacha kutumia milioni 250 na badala yake kuzipeleka Hospitali kusaidia Watanzania? Rejea Tundu Lissu kutetea milioni karibia 300 walizokuwa walipwe kama Wabunge, je angeziacha hizi za juzi kama angekuwa na madaraka?

Unafikiri Lowasa na Mbowe wangeahirisha kuuza sura Disemba 9 na badala yake kutumia hizo fedha kwa ajili ya maendeleo?
Unafikiri Lowassa na Mbowe wangefuta safari za nje ya nchi?

Mke wa Lowassa unafikiri leo hii angekuwa kimya kama mama Janeti au tayari angeshaanzisha NGO na sia ajabu sasa hivi angekuwa yuko safari ndefu ya Marekani na Ulaya kuuza wazo lake?

Mungu bado hajachoka na sisi Watanzania anatupenda na ndiyo maana ametuongoza na tukafanya maamuzi ya busara, leo hii ukiwauliza waliompigia kura Dr. Pombe Magufuli kama wana majuto yoyote ya kufanya jibu lake ni HAPANA kubwa!
Kama angelikuwa Lowassa ni Rais mkwamo wa kisiasa ZANZIBAR UINGEKUWA HISTORIA
 
Lowassa ni nabii wa watanzania, aliye Na sikio Na asikie neno hili ambalo roho wa mungu anawaambia watanzania
 
Rostam angekua anaishi ikulu.....

Kingunge angekua mganga wake wa kienyeji......

Angetangaza kua Richmond ni yake
 
Wasiwasi wangu pekee kuhusu Lowassa ilikuwa ni wale marafiki zake wasiojulikana ambao wamekuwa wakimpa mabilioni ya pesa kutoa makanisani, misikitini (hata kununulia ugombea CHADEMA) miaka nenda miaka rudi. Hawa jamaa si ajabu wangekuwa wameshaigeuza ikulu kuwa pango la walanguzi. Ni hilo tu ndo lilikuwa linanikera hata ukiniangalia usoni utaamini ni kweli lilikuwa linanikera (Nimekumbuka hotuba mashuhuri ya Baba wa Taifa)
Una ushaidi
 
Back
Top Bottom