FIFA kufungua mashitaka ya kinidhamu kwa timu ya Argentina

Raphael Thedomiri

JF-Expert Member
Sep 1, 2019
442
728
Shirikisho la soka ulimwenguni, FIFA limetangaza kufungua kesi za kinidhamu dhidi ya timu ya Argentina kutokana na kile ilichokitaja kama tabia zisizo za kiungwana ilizoonyesha baada ya kuchukua ubingwa wa kombe la Dunia mwezi uliopita.

Mlinda mlango wa Argentina Emiliano Martinez alionyesha kitendo hicho baada ya kutunukiwa tuzo ya mlinda mlango bora wa michuano na baadaye kurekodiwa akitoa matamshi ya kumbeza nyota wa Ufaransa, Kylian Mbappe wakati akiwa kwenye chumba cha kubadilisha nguo.

FIFA imesema kulikuwa na uwezekano kwamba Argentina ilikiuka sheria kuhusu tabia za kuudhi na kanuni za ushindani wa haki lakini pia utovu wa nidhamu wa wachezaji na maafisa.

DW
 
Emiliano Martinez akishangilia tuzo ya golikipa bora wa michuano ya Copa America, ndio style yake ya kushangilia


5DFBB043-8B7C-4054-BC25-57C74CA74509.jpeg
 
Back
Top Bottom