Fiber ya simbanet inaonyesha jinsi Tanzania tunavyohitaji internet mbadala

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
30,745
39,849
Nimepata bahati ya wiki yote hii kutumia fiber ya simbanet (kwa ajili ya biashara), hii internet ina latency ndogo kiasi kwamba unaweza hadi kusahahu kama unatumia internet. Ni bundle ya 5mbps na unaipata speed hio hio bila kushuka kote download na upload. latency yake ni 2ms tu kitu ambacho sijawahi kiona mtandao wowote wa simu Tanzania au satelite internet yoyote niliowahi tumia.

piFRzVM.jpg

Uwe unatumia skype, unacheza games online, unaangalia tv/mpira online au kufanya kitu chochote kinachohitaji latency ndogo simbanet wanatuonesha jinsi gani internet ya kufanya mambo hayo inavyotakiwa kuwa. bahati mbaya hii ni package ya biashara hivyo ni ngumu kwa mtu wa kawaida kuweza kui afford, ila nategemea baadae waanze kuuza reja reja kwa wateja.

Kwa mnaotumia smile, 4g tigo na smart 4g kuna ambae amewahi kupata latency/ping ya single digit kama hio?

Kwa ambao hawaelewi latency/ping unaweza kujifunza zaidi hapa
https://www.jamiiforums.com/tech-ga...iwa-na-download-speed-kubwa-ndio-mzuri-2.html
 
Duuh Mm niwape tu Salute maana 2ms ni level za nje kabisa

Pili nimefurahi kuona unalipia 5Mbps then unapata same speed both Download na Upload yaani hamna kubaniana

Ukibahatika latency ya 3G ni 20-50ms and sometimes mpaka above hiyo range

Na bado speed za 4G e.g kwa Tigo maeneo mengi ni average 8Mbps+ kitu kama 3G fulani labda tuwaombee mema wanavyozidi expand network yao walau maeneo mengi yatakuja kufika atleast rate ya 30Mbps kama ilivo kwa baadhi ya maeneo
 
nimepata bahati ya wiki yote hii kutumia fiber ya simbanet (kwa ajili ya biashara), hii internet ina latency ndogo kiasi kwamba unaweza hadi kusahahu kama unatumia internet. ni bundle ya 5mbps na unaipata speed hio hio bila kushuka kote download na upload. latency yake ni 2ms tu kitu ambacho sijawahi kiona mtandao wowote wa simu tanzania au satelite internet yoyote niliowahi tumia.

piFRzVM.jpg

uwe unatumia skype, unacheza games online, unaangalia tv/mpira online au kufanya kitu chochote kinachohitaji latency ndogo simbanet wanatuonesha jinsi gani internet ya kufanya mambo hayo inavyotakiwa kuwa. bahati mbaya hii ni package ya biashara hivyo ni ngumu kwa mtu wa kawaida kuweza kui afford, ila nategemea baadae waanze kuuza reja reja kwa wateja.

kwa mnaotumia smile, 4g tigo na smart 4g kuna ambae amewahi kupata latency/ping ya single digit kama hio?

kwa ambao hawaelewi latency/ping unaweza kujifunza zaidi hapa
https://www.jamiiforums.com/tech-ga...iwa-na-download-speed-kubwa-ndio-mzuri-2.html

Simbanet ni moja kati ya ISP wakubwa , hawa huwa hawanunui B/w kutoka kampuni nyingine ya kitanzania au africa. Hawa ndio wanaowauzia ISP wengine B/w ndio maana intenet yao ni ya uhakika.
 
Tufahamishe vizuri kuhusu hii fiber ya simbanet ni kampuni gani!

Simbanet ni kampuni inayojihusisha na usambazaji wa internet lakini zaidi hawa hawategemei sana kuuza kwa watumiaji wa rejareja, zaidi wanauzia kampuni nyingine za kusambaza internet ISP, ambao hao nao wanaenda kuuza internet rejareja-RESELLERS.
 
nafikiri mtoa mada amejisahau ni kuwa fiber(mkongo) ni "media" ambayo mawasiliano hupita kufika sehemu husika.alichotakiwa kusema ni internet ya Simbanet ina kasi nzuri!
 
Everyday nikiwa natumia Internet in my pc or my smartphone huwa inaniumiza sanaaa kuona jinsi gani matumizi yangu yanakuwa limited na internet speed na ubora wa package zao...

I could av done so much more with my 4n lakin ndo ivo usipopata tatizo la speed utasikia umetumiwa msg kuwa umebakiwa na na Mb 2 za bonus (lik i could do anythin with 2mb)..

It pains me ninapowatch movie or stream video youtube na kuona how other people enjooy th Internet world..

But i am sure one day yes tutapata provider ambaye atakizi mahitaji yetu kama huyo Simbanet with reasonable Price..I hope that day will come soon..

PS. Thanks for the Post Chief...
 
nafikiri mtoa mada amejisahau ni kuwa fiber(mkongo) ni "media" ambayo mawasiliano hupita kufika sehemu husika.alichotakiwa kusema ni internet ya Simbanet ina kasi nzuri!

Hawa jamaa wana advantage sana kwasababu wao wanayo mkongo wao wenyewe kupitia baharini.
 
Optic fiber, twisted pair cable na coaxial cable ni transmission media za internet.....hila optic Fiber ni latest media inayowezesha kupata internet ya kasi zaidi
 
Mimi binafsi ningekuwa Tayari kuhustle nipay even 100-150 a month kama ningepata proof kabisaa kuwa certain provider angenipa tru unlimited package with good Download,uploaf speed na Latency nzuri regardless of the place i am and the time of day meaning regardless ni mchana au usiku maaana izi internet zetu za Bongo zinafikia hatua zinatuharibia Hadi Sleeping Patterns...
 
nafikiri mtoa mada amejisahau ni kuwa fiber(mkongo) ni "media" ambayo mawasiliano hupita kufika sehemu husika.alichotakiwa kusema ni internet ya Simbanet ina kasi nzuri!

Yap nafahamu na ningeweza kusema hivyo lakini wana internet za aina tatu tofauti.
-fiber internet
-3g internet
-satelite internet

Kila moja ina speed yake na latency yake. Hivyo ningesema tu internet ya simbanet ni nzuri then mtu akatumia 3g yao au satelite internet yao na kuona ni mbaya ingekuwa haipendezi.

Ukumbuke hizo media za usafirishaji pia huathiri speed na latency
 
Hawa jamaa wana advantage sana kwasababu wao wanayo mkongo wao wenyewe kupitia baharini.

hii si kweli hapa tanzania kuna mikongo miwili kupitia baharini nayo ni Seacom na Eassy. Simbanet na operator wengine wanatumia hiyo mikongo kwa huduma za internet toka ulaya.
 
Yap nafahamu na ningeweza kusema hivyo lakini wana internet za aina tatu tofauti.
-fiber internet
-3g internet
-satelite internet

Kila moja ina speed yake na latency yake. Hivyo ningesema tu internet ya simbanet ni nzuri then mtu akatumia 3g yao au satelite internet yao na kuona ni mbaya ingekuwa haipendezi.

Ukumbuke hizo media za usafirishaji pia huathiri speed na latency

Nimekupata ndugu! ila hii inaonekana kama aina za huduma ama Vifurushi,kwa maana unaposema Fiber na 3g internet inachanganya kwa maana tunaangalia Equipment ya mwisho itakayorusha hayo mawimbi kwa mteja kwasababu Fiber ni kipitisho cha mawasiliano kufikia chombo kitakachorusha hayo mawimbi unaweza kurusha pia hayo mawimbi kupitia hewani hasa kwa kutumia Radio nakutoa huduma husika yaani "Wireless".Ningependa kujua huduma hiyo ya internet unaipataje ?je wameleta Fiber mpaka hapo ulipo ama unapokea kupitia "wireless"?
 
Jamani ule mkongo wa mawasialo wa prof mbarawa na makamba junior umefikia wapi?
 
Nimekupata ndugu! ila hii inaonekana kama aina za huduma ama Vifurushi,kwa maana unaposema Fiber na 3g internet inachanganya kwa maana tunaangalia Equipment ya mwisho itakayorusha hayo mawimbi kwa mteja kwasababu Fiber ni kipitisho cha mawasiliano kufikia chombo kitakachorusha hayo mawimbi unaweza kurusha pia hayo mawimbi kupitia hewani hasa kwa kutumia Radio nakutoa huduma husika yaani "Wireless".Ningependa kujua huduma hiyo ya internet unaipataje ?je wameleta Fiber mpaka hapo ulipo ama unapokea kupitia "wireless"?

Hapa nilipo imeletwa na fiber ila hapa ni kitawi tu na sio head office, so sijajua head office imekuja kama fiber ama la, itabidi uniachie homework.

Kucompare na mobile data, hii fiber kila mtu ndani ya kampuni anapata same speed bila kudrop kwenye kifurushi kimoja, hata mkiwa wengi haiathiri matumizi.
 
Yaan ikatokea kampuni ikatoa 3g unlimited speed unlimited bandwith hata kwa elfu 50 mpaka kilo minajipinda maaa sasa hiv dstv kilo 2 parefu nikilipia internet nauhakika wa kucheki mpira movies na series na download
 
hii si kweli hapa tanzania kuna mikongo miwili kupitia baharini nayo ni Seacom na Eassy. Simbanet na operator wengine wanatumia hiyo mikongo kwa huduma za internet toka ulaya.

Ipo hivi inawezekana kabisa wasitumie jina la seacom wala eassy lakini ikawa ni part ya ya mmojawapo, hizi ni mbinu za kuteka soko katika eneo husika.
 
Yaan ikatokea kampuni ikatoa 3g unlimited speed unlimited bandwith hata kwa elfu 50 mpaka kilo minajipinda maaa sasa hiv dstv kilo 2 parefu nikilipia internet nauhakika wa kucheki mpira movies na series na download

Smart 20,000 unlimited bandwitch nje ya dar
 
Chief nipo dar mkuu smart nimewajaribu speed ya kobe balaa zantel wapo fast ila unlimited laki 3 parefu hapo voda unlimied yao ya hovyo .airtel hawana na tigo
 
Back
Top Bottom