Ferooz awaanika Prof Jay na Chege

Ferooz awaanika Prof Jay na Chege

kwelo unga sio kabisa, mbona hajamtaja swaiba wake daz baba? kuna kipindi flan alisaliti kundi lake,
 
Nymbo kama hiz huwa ata wik hazimaliza ishafichwa kapuni...
Na kinachofata n kunyosheana vidole kwa makosa alieyafanya yeye mwenyew...
 
Muziki wa Bongo kuna kitu kimoja bado ni challenge sana.

Arrangement.

Wimbo unaweza kuwa na lyrics nzuri. Production nzuri. Sauti nzuri. Vionjo vizuri. Lakini ukikosa arrangement tu, unakosa mvuto.

Nilikuwa nasikiliza Michael Jackson's "Wanna Be Startin' Something", wimbo ulio katika album yenye mauzo mengi kuliko zote duniani nafikiri, Thriller (Thriller imefikisha "Diamond", which is better than "Platnum" in sales, yes, diamond and platinum are sales threshold). Nilipousikiliza wimbo ule, nikajiuliza, ni kwa nini umenikaa kichwani miaka 35 sasa tangu utoke, na ukipigwa unakufanya usisimke na utake kucheza. Nikagundua production ni nzuri, uimbaji ni mzuri, lyrics ni nzuri lakini vyote ni kawaida. Ila arrangement, kuanzia drums za kwanza mpaka mwisho Michael anavyowaimbisha watu "Mama se, Ma Mako Ma makosa", Michael alielewa anataka kufanya nini na kafanya arrangement ya wimbo kama ana chireograph dance move. Chombo gani kitaanza, kipi kitafuatia, chorus itakaa wapi, itajirudia mara ngapi, bassline litaendaje, litakata wapi kuachia vyombo vingine, hirns zitaenda wapi, zitakaa vipi zisiingilie vyombo vingine, Michael atapagawisha vipi, atashirikisha wengine vipi, atamalizia vipi wimbo.

Kila kitu kimepangwa kwa detail sana. Na unaweza kuona watu wamepangua vingi mpaka kufikia hapo.

Sisi tunaenda studio huku tunaangalia muda wa studio kwa bajeti, producer akikupigua beat ya kwanza ndiyo hiyo hiyo. Hakuna hata muda wa kujadili.

Hata kama kila instrument imepigwa vizuri, lyrics nzuri, uimbaji mzuri, bila arrangement wimbo unaboa.
 
ferooz angejiingiza kwenye kitengo cha wapambanaji wa ukimwi, Pengine saivi angekua balozi wa kupambana na ukimwi Africa. mziki umebadilika sasa, watu hawahitaji mafunzo, wanataka mziki mnene tu
 
Mziki wa bongo watu hawana talent...
Bila kiki mtu hatoki....
Ni tofauti na njee...
Talent kwanza...kiki utaleta kwenye kutoa album tu na si katika nyimbo mpya
 
Muziki wa Bongo kuna kitu kimoja bado ni challenge sana.

Arrangement.

Wimbo unaweza kuwa na lyrics nzuri. Production nzuri. Sauti nzuri. Vionjo vizuri. Lakini ukikosa arrangement tu, unakisa mvuto.

Nilikuwa nasikiliza Michael Jackson's "Wanna Be Startin' Something", wimbo ulio katika album yenye mauzo mengi kuliko zote duniani nafikiri, Thriller (Thriller imefikisha "Diamond", which is better than "Platnum" in sales, yes, diamond and platinum are sales threshold). Nilipousikiliza wimbo ule, nikajiuliza, ni kwa nini umenikaa kichwani miaka 35 sasa tangu utoke, na ukipigwa unakufanya usisimke na utake kucheza. Nikagundua production ni nzuri, uimbaji ni mzuri, lyrics ni nzuri lakini vyote ni kawaida. Ila arrangement, kuanzia drums za kwanza mpaka mwisho Michael anavyowaimbisha watu "Mama se, Ma Mako Ma makosa", Michael alielewa anataka kufanya nini na kafanya arrangement ya wimbo kama ana chireograph dance move. Chombo gani kitaanza, kipi kitafuatia, chorus itakaa wapi, itajirudia mara ngapi, bassline litaendaje, litakata wapi kuachia vyombo vingine, hirns zitaenda wapi, zitakaa vipi zisiingilie vyombo vingine, Michael atapagawisha vipi, atashirikisha wengine vipi, atamalizia vipi wimbo.

Kila kitu kimepangwa kwa detail sana. Na unaweza kuona watu wamepangua vingi mpaka kufikia hapo.

Sisi tunaenda studio huku tunaangalia muda wa studio kwa bajeti, producer akikupigua beat ya kwanza ndiyo hiyo hiyo. Hakuna hata muda wa kujadili.

Hata kama kila instrument imepigwa vizuri, lyrics nzuri, uimbaji mzuri, bila arrangement wimbo unaboa.
Mkuu tofauti ya huku na huko ni kwamba,
Mziki huko una shule, Producer kaenda shule ya mziki, mameneja wa wanamuziki wana shule ya mziki, hata wasanii nasikia hupewa kozi ya mziki, kupangilia ala, vina, instruments, wapi kupanda, kushuka, kuweka hisia.

Tatizo huku bongo tuna amini kila kitu ni kipaji, mashairi ya hovyohovyoo.

Shule ndo tatizoooo
 
Juzi nilikuwa nasikiliza kipindi cha sanaa BBC World Service. Walikuwa wanaongelea sinema za kihindi na zilivyo diverse si Bollywood tu. Kuna dada alikuwa anahojiwa akasema amesomea filamu Massachusetts USA.

Lupita Nyongo Mkenya anatingisha dunia, anesomea drama Yale University.

Sisi tunapasua kwa vipaji tu.

Hata ile kusoma vitabu mwenyewe tu tabu.
 
Huu wimbo ili kutoboa unahitaji promo kubwa sana la Clouds kama lile walilomfanyia Saida, lasivyo utapigwa kapuni haraka!
 
Mziki umekua kama elimu.

Zamani ilikua ukiingia studio tu, umetoka. Ukitaka uendelee kusikika lazima ukubali mabadiliko ya teknolojia.

Usipokua mbumifu hata uwe na kipaji vipi, utaishia kulalamika.

Sijamuona ferooz wa enzi za boss na starehe hapa. Ameimba kama wale watoto wanaimba singeli mtaani
 
ferooz angejiingiza kwenye kitengo cha wapambanaji wa ukimwi, Pengine saivi angekua balozi wa kupambana na ukimwi Africa. mziki umebadilika sasa, watu hawahitaji mafunzo, wanataka mziki mnene tu
Na hii ndo inawaangusha wanaHipHop wengi mkuu
 
Kaza roho km jina la nyimbo yako inavyoitwa,najua marafiki wengi wamekukimbia ,mapromota wamekutenga ila sisi mashabiki wako tuko pamoja,nyimbo ni nzuri ila kwakuwa baadhi ya watu hawakupendi haitahit,kaza roho bro,we love u so much,ni mapito tu ya dunia
 
Inasikitisha sana ,jamaa kaimba ukweli mtupu,inauma sana aisee
 
Back
Top Bottom