ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
ALBUM YA PROFESOR JAY "MACHOZI ,JASHO NA DAMU
View: https://www.facebook.com/100064569174258/posts/pfbid0Eksw2k3qTSg3kzXd5H6BtXzEYYNiNtGTXA6K24WvMf2U6zETpBsMxgtCTF6L1u2yl/?app=fbl
"Machozi Jasho na Damu..
ni jina la kutaja albamu ya kwanza kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Kitanzania, Professor Jay. Albamu imetoka mwaka 2001, mwaka mmoja tangu kutolewa albamu aliyofanya na kundi zima la Hard Blasters Crew, Funga Kazi (2000).
Professor Jay anarudi tena kama msanii wa kujitegemea, lakini safari hii anaamua kutoa na albamu kabisa badala ya kufanya moja-moja. Kabla ya albamu na kujiunga HBC, Jay (wakati huo Nigga Jay) alifanya wimbo na Taff B. (Fascinating Rhymes) na amepita makundi mengi tu kabla kufika HBC halafu baadaye kurudi kama msanii wa kujigetemea. Albamu imetazama nyanja nyingi, kuanzia siasa, maisha, historia na hoja nzito kuhusu vijana na wazee.
Jay ameenda mbali zaidi katika albamu hii kwa kuenzi muziki wa hip hop wa Tanzania kwa kuelezea mengi tangu muziki huu unaanza katika miaka ya 1980 na 1990 mwanzoni. Katika "Tathmini" anaelezea jinsi walivyopata tabu katika kuanzishwa kwa muziki huu katika Tanganyika ya Kijamaa.
Halkadhalika ame-enzi kazi ya mwanzilishi halisi wa rap ya Kiswahili nchini Tanzania bwana Edward Mtui (maarufu kama Fresh XE) kwa kuchukua kiitikio chake cha "Piga Makofi" ambacho kilimpelekea ashinde tuzo ya Yo Rap Bonanza katika miaka ya 1980, lakini hakutoa nyimbo
Professor Jay anatungia wimbo kiitikio hicho na ndani yake anataja wale wote walioifikisha hip hop ya Tanzania hapa kwa kuwataja.
Katika wimbo wa Piga Makofi, kamtaja, Cool Moe Cee, Fresh XE, Ibony Moalim (yeye na Kim ndio hasa waliokuwa waratibu wakuu kabisa wa Yo Rap Bonanza), Rankim Ramadhani, Big Rawy, JD, Uncle Jay, Masoud Masoud, Master T (Taji Liundi), Saleh Jabri na wengine wengi.
Mtindo huu wa kuthamini muziki ulipotoka katika albamu hii umekuwa kitu cha kawaida huku utunzi na namna ya kuenzi hali halisi ya hip hop ya Tanzania katika nyimbo umekuwa wa kipekee sana.
Jay amerudia tena kuwataja waasisi wa muziki wa aina mbalimbali (Ugly Faces, KU Crew, Mr. 2, Taff B., Mack D, John Dillinger], Tough B) nchini Tanzania katika wimbo wa "Yataka Moyo
". Katika wimbo huo, Jay anajaribu kutazama kazi ya sanaa na kipato wanachokipata wasanii katika kazi hiyo. Halkadhalika anataja wasanii walioisukuma gemu ya muziki wa Tanzania katika kiwango cha sasa.
Vilevile anawataja wadau mbalimbali wa sanaa mbalimbali ambao nao walihangaikia kusukuma sanaa na wasanii wa Bongo katika ramani iliyoisimama. Mwaka ambao albamu hii inatoka, kulitoka pia albamu nyingine kibao, albamu kama vile Nini Chanzo, Ni Saa Ya Kufa Kwangu, Bwege Mtozeni, Poa Tu - Volume 1, Tuko Pamoja?... Vol. 1 na nyinginezo kibao. Huu ulikuwa mwaka wa mapinduzi hasa ya muziki wa kizazi kipya. Ilikuwa lazima kila albam ikitoka ifanyiwe uzinduzi.
Sikiliza ujumbe huu kutoka kwa msanii "Lb" katika wimbo unaitwa " Na bado" moja kati ya ngoma kali zinazopatikana katika Album hii ya " Machozi ,jasho & Damu.
💥💥💥💥💥💥💥💥💥💥💥💥💥💥🗯🗯🗯🗯💥💥💥💥💥🗯🗯🗯🗯🗯🗯💢💢
Natumia nafasi hi kudhibitisha kipaji changu/ nikiwa ni mkakati wa kuinua jina langu/ na huu sio mkwala tu ni msisitizo wenye nia/ kama kipaji kipo sioni wa kuziba njia/ nadhibitisha mc umahili kimiundombinu/ na jay na lb kwenye mpango ndani ya kino/ nipo fresh na bado nitazindi kuthibisha/ kadri siku zinavyokwenda ndivyo ndavyo tisha/ thamani ya kipaji changu ni zaidi ya uhai wa mtu/ kinauwezo kuelimisha na kubadirisha mtu/ na anzisha vita baridi aje mpinzani wa jadi/ kama osama na bush rap izushe jihadi/ jino kwa jino tu sambamba jukwaani/ hata aje ngwiji sihofii kutoa ushindani/ na amini kwamba uwezo huo ninao na ninazua mtafaruku wabishane wao kwa wao/ fani uwanja wa vita na ndani nisha vaa kwanda/ nakoleza ushambulizi na siogopi kupondwa/ Tungo zangu silaha na kipaji ndio Ngao/ ole wao vichwa pumba Kazi kwao na Bado....
(👆👆👆👆👆 Verse ya msanii LB GENIUS)
#funguka
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202