FEED-BACK ina maana gani kwa kiswahili??

Naamini mtoa hoja alitaka tafsiri na hii ya ''mrejesho imekaa vizuri labda waikatae BAKITA".
Hizi nyingine zimekaa kimaelezo zaidi kuliko tafsiri

kweli nimejua kuna watu wanajua lugha...hii tafsiri imekaa fresh!
 
Hata mimi mnanchangana. Hebu jarbu hii: Mtiriko wa taarifa kuhusiana na shughuli au kazi iliyopangwa kwa ajili ya maamuzi au muendelezo. Kismahili . . . haswa tafsiri inapoanzi kwenye lugha asili!
 
:nono:Muuliza swali nimemsoma katikati ya mstali. Anachokihitaji ni tafsiri wala si maana kwa sababu MAANA pia yaweza kuwa ya kisemantiki au ya kipragmatiki na hivo sidhani kama wanajamvi watakuwa na muda kujiingiza kiundani katika tafsiri hizo. Ninaamini kabisa muuliza swali ameuliza kwa muktadha wa kimawasiliano. Na kama hivo ndivyo, basi mimi niseme tu kwamba "mlisho nyuma" ni mchakato unaopitia kuanzia kwenye WAZO/UJUMBE (Message) linalopitia kwenye NJIA fulani (channel) na msikilizaji kusimba (ENCODE) wazo hilo kabla ya kulipatia fasiri mahsusi (DECODE) kisha kutenda kadri ya matakwa ya ujumbe husika (FEED BACK). Kwa maelezo kuntu ni kwamba huo ni mchakato unaokamilisha mkufu wa mawasiliano. Upo hapo, mtu wangu??????:frusty:
 
Back
Top Bottom