Fedha za upanuzi wa bandari zingetumika kujenga Cable car Mlima Kilimanjaro!

Wapi ameandika mbuga zijengwe lami?naona unarudiarudia neno lami.
Naona kaedit baada ya kujua alichoandika initially ni uharo but here's the original post
Screenshot_20170616-033840.png
 
Kwani ikiwekwa cable car, njia ya kupanda kwa miguu itafungwa? Atakayetaka kufanya adventure ya hiking atafanya asiye na nguvu Ila ana interest tu ya kufika kileleni atatumia cable car.
Bandari ni muhimu utalii pia muhimu so hapo kupanga vipaumbele.
Exactly priority huyu bwana bila aibu kasema tusiboreshe bandari na badala yake hizo pesa tujengee cable cars Kilimanjaro, hii ni pumba. Tunaweza kujenga hizo cable ila sio kipaumbele kwa sasa, bandari ni ya muhimu ina wateja wengi, wauhakika na wapo kila siku.
 
Upanuzi wa bandari kwa sasa hauna tija.
Hizo bilioni mia tatu zingetumika kujenga cable car ya kupandishia watalii mlima Kilimanjaro ndio mradi ambao ungekuwa na tija zaidi.
Tanzania inapata mapato mengi zaidi kwenye utalii kuliko hata kwenye bandari. So ingekuwa ni vyema zaidi tukaboresha sekta ya utalii...

Kwa sasa kwa kuwa mlima Kilimanjaro ndiyo habari ya mujini kwa watalii wengi na wengi wanaofika huishia kuuona kwa mbali kwa kuwa hawana nguvu na afya za kupanda mlima, ujenzi wa cable car ungesaidia watu wengi zaidi ikiwamo watalii wa nje na watalii wa ndani kupanda mlima kwa urahisi.
Kwa kuwa tuna watalii angalau milioni moja wanaotembelea nchi kwa mwaka, kila mmoja angelipa angalau laki moja kupanda mlima kwa kutumia cable car, tungeweza kugenerate mapato yasiyopungua bilioni mia moja kwa mwaka, na hiyo pesa ingeweza kurudhi ndani ya mda mfupi tu ikiwa ni pamoja na kukuza sekta!
113383.jpg

1200px-Funivia_Rote_Nase_alt.JPG

maxresdefault.jpg
Ni wazo zuri lakini sio sahihi kufikiri kwamba sababu ya utalii basi bandari haina tija. Long term bandari ina msaada mkubwa sana kwa uchumi kama ilivyo utalii
 
Bandari tuboreshe lakini sio kuchimba kina,ndio maana lilikuja wazo la bandari ya bagamoyo kwasababu kuna kina kirefu cha asili hii ya kuchimba baada ya muda kinajifukia yapo mambo ya kuboresha bandari ya muhimu kama vitendea kazi,matumizi ya teknolojia nk lakini sio kuchimba kina maana hata meli za kisasa zinatengenezwa kwa teknolojia ambayo haihitaji meli kuzama chini sana,teknolojia mpya inafanya meli kuelea juu juu ili kupunguza upinzani wa maji ambao unasababisha nguvu nyingi kutumika na chombo ambapo pia hutumia mafuta mengi.
 
Ni wazo zuri lakini sio sahihi kufikiri kwamba sababu ya utalii basi bandari haina tija. Long term bandari ina msaada mkubwa sana kwa uchumi kama ilivyo utalii
Bandari ina tija lakini mtoa mada kasemea hakuna tija kwenye kutoa bilioni mia tatu kuchima kina.
 
Bandari ina tija lakini mtoa mada kasemea hakuna tija kwenye kutoa bilioni mia tatu kuchima kina.
Sasa meli zinaongezeka ukubwa ili kupunguza gharama za uendeshaji. Sisi tuendelee kubaki vilevile itatusaidia nini?
 
Umesema kwa mwaka tuna watalii milion alafu unawaona ndio bora kuliko bandari? Huijui bandar mkuu
 
Watalii wapi ....wakati tunacharge 18% VAT.
Kwa umeme upi..huu wa mgao?
Itakuwa rahisi kujenga treni ndogo ya kitalii kuliko cable cars. Hii treni pia ingetumika kubeba walemavu + watakaoshindwa kufika au kurudi toka juu.
 
Ni wazo zuri sana, tena sana, haya yote mawili yafanyike, tuwe na upanuzi wa bandari pia tujenge hiki kitu, wizara ya utalii fuatilieni mchakato mzima tujue gharama halisi ya kujenga hii kitu, pengine inaweza ikawa ni gharama ndogo ambayo serikali inaweza ikamudu, yaani hiyo kitu yenyewe kama yenyewe ni utalii tosha,watu wengi watapenda kwenda kubembea hadi kufika juu, naunga hoja.
 
The beauty of Mt Kilimanjaro ni kupanda kwa miguu na watalii wengi wanakuja kwa sababu ya kupanda kwa miguu.
What the point ya kupanda kwa kutumia cable car. Ukisha kileleni utasema umepanda mlima Kilimanjaro?

Hii itapunguza watalii wengi wa nje labda wa hapa nyumbani wanaotaka kulinda vitambi vyao.
Hajui purpose ya kupanda mlima kwa nguvu ya mtu mwenyewe.
Upanuzi wa Dar Port unaenda sambamba na ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha Standard gauge
 
Kupanda mlima ni life experience, adventure, achievement. Wengi wanapenda kuwa sehemu ya historia, Everest lina watalii wengi zaidi na hawana hizo cable cars
 
Ushajiuliza njia ya marangu ni nyepesi na ina miundombinu ya majengo(nyumba za vibanda)na ninafuu lkn wageni hawaipendi sana kulinganisha na nyingine??
 
The beauty of Mt Kilimanjaro ni kupanda kwa miguu na watalii wengi wanakuja kwa sababu ya kupanda kwa miguu.
What the point ya kupanda kwa kutumia cable car. Ukisha kileleni utasema umepanda mlima Kilimanjaro?

Hii itapunguza watalii wengi wa nje labda wa hapa nyumbani wanaotaka kulinda vitambi vyao.
Sasa kile cheti nilichopewa Kitakuwa na maana gani kama utafika Stella, Gilman na Uhuru peak kwa msaada wa umeme?
 
Wazo zuri sana sana.....watangaze tender wawekezaji waje wawekeze tugawane nao ujira......maana serikali kuendesha vitu vingi kama hivyo ni shida
 
Itabidi Utafiti ufanyika kuangalia kama kuna demand ya kutosha.isije ikawa hailipi. AU ikawa tunazungusha watalii walewale,yaani wanaacha kupanda kwa miguu wanahamia kwenye cable
Japo binafsi nadhani bandari italipa zaidi.Hilo wazo ni zuri kwa siku za mbeleni
 
Upanuzi wa bandari kwa sasa hauna tija.
Hizo bilioni mia tatu zingetumika kujenga cable car ya kupandishia watalii mlima Kilimanjaro ndio mradi ambao ungekuwa na tija zaidi.
Tanzania inapata mapato mengi zaidi kwenye utalii kuliko hata kwenye bandari. So ingekuwa ni vyema zaidi tukaboresha sekta ya utalii...

Kwa sasa kwa kuwa mlima Kilimanjaro ndiyo habari ya mujini kwa watalii wengi na wengi wanaofika huishia kuuona kwa mbali kwa kuwa hawana nguvu na afya za kupanda mlima, ujenzi wa cable car ungesaidia watu wengi zaidi ikiwamo watalii wa nje na watalii wa ndani kupanda mlima kwa urahisi.
Kwa kuwa tuna watalii angalau milioni moja wanaotembelea nchi kwa mwaka, kila mmoja angelipa angalau laki moja kupanda mlima kwa kutumia cable car, tungeweza kugenerate mapato yasiyopungua bilioni mia moja kwa mwaka, na hiyo pesa ingeweza kurudhi ndani ya mda mfupi tu ikiwa ni pamoja na kukuza sekta!
113383.jpg

1200px-Funivia_Rote_Nase_alt.JPG

maxresdefault.jpg

Wabongo bhana, Akili ndogo kweli, kweli!
 
Back
Top Bottom