Fedha za upanuzi wa bandari zingetumika kujenga Cable car Mlima Kilimanjaro!

Hii ni pumba first class; cable car Kilimanjaro, lami mbugani, bandari isiboreshwe, umesomea ulichooandika kweli?

Milima ya kitalii ni kwaajili ya hiking sio kutumia cable unless huo mlima upo katikati ya mji. Nchi gani wameweka cable car kwenye mlima wa utalii Everest, Himalayas au mt Kenya au wapi huko? Utalii unachangiwa na vivutio vyote nchini sio Kilimanjaro tu ndiyo maana Pato la utalii ni kubwa. Bandari ikiboreshwa na kusimamiwa vizuri ina wateja wengi na wauhakika kila siku. Lami mbugani wakati hata mijini hazijaisha, nchi gani wameweka lami mbugani kila Kona? We jamaa umeenda shule kusomea ujinga
Mpagazi nini mbona umeongea kwa Key note za juu sana mkuu?
 
Wewe unasema hivyo kwa kuwa waafrika tumeshazoea shida. Wazungu wangekuwa wanapenda shida kama wewe, wasingegundua vitu vyote hivi vilivyopo Duniani ambavyo vinarahisisha maisha ya mwanadamu!
Sijui umeingizaje shida hapa lakini kama nimekusoma sidhani kama wazunguka wanalipa na kupanda ndege kama wangekuwa wanai consider ni "shida"!
 
[QUOTE="
Hiyo cable car inaweza ikajengwa huko huko Marangu, swala hapa ni kukuza utalii nchini...[/QUOTE]
sasa Cable car ya nini kuupanda Mlima Kilimanjaro?
ina maana wapelekwe na kushushwa kam wagonjwa tu
kukwea miti, majabali milima nk ni kitu kingibe kabisa na kumpeleka au kumshusha mgonjwa
 
raha ya milima uupande uone vegetation tofaut na uzuri wa uumbaji wa mungu,,,hujui raha ya kulala camp wewe
 
nalo ni wazo zuri sana ukizingatia kuna wengine hawana nguvu ya kupanda, lakini bandari ipanuliwe kwanza hiyo ifanyike wakati mwingine
 
Hata Abramovich atakuja tena maana alipokuja mwanzo alishindwa kufika kileleni akashuka na kusepa
 
Nchi hii bado tunayo mengi ya kufanya zaidi ya hizo cable. Hospitali zenyewe kila mikoa zimewashinda, shuleni bado hakueleweki watoto wanakaa chini. Maziwa yetu yanahitaji meli za uhakika kwa usafiri na kubebea mizigo bado unafikiria cable leo.

Bado hatujaweza kuifanya bandari yetu kuwa walau ya pili kwa ukanda wa bahari hindi kask-kus. Ungeniuliza mie ningekwambia hii cable ijengwe 2050. Hata wenzetu ambao naamini hizi picha ulikozitoa hawakufikia hapo kama unavyofikiri, walianza na mengi yaliyo madogo. Hatuwezi kuiga kila kitu pasipo kuwaza kwa undani hari zetu kwanza.
 
toka nimeanza kusoma jf wewe ndo umeongea point.ingawa itapunguza ajira ila ni nzur sn
 
Hii ni pumba first class; cable car Kilimanjaro, lami mbugani, bandari isiboreshwe, umesomea ulichooandika kweli?

Milima ya kitalii ni kwaajili ya hiking sio kutumia cable unless huo mlima upo katikati ya mji. Nchi gani wameweka cable car kwenye mlima wa utalii Everest, Himalayas au mt Kenya au wapi huko? Utalii unachangiwa na vivutio vyote nchini sio Kilimanjaro tu ndiyo maana Pato la utalii ni kubwa. Bandari ikiboreshwa na kusimamiwa vizuri ina wateja wengi na wauhakika kila siku. Lami mbugani wakati hata mijini hazijaisha, nchi gani wameweka lami mbugani kila Kona? We jamaa umeenda shule kusomea ujinga
Atakuwa ametawaliwa na uzungu hata kufikiri na si ajabu hata sura yake inaelekea kuwa ya kizungu hivi. Colonized mind always pathetic!
 
Atakuwa ametawaliwa na uzungu hata kufikiri na si ajabu hata sura yake inaelekea kuwa ya kizungu hivi. Colonized mind always pathetic!
Yani kachukua picha za mijini anataka ndo ifanyike Kilimanjaro sijui mlima gani wa utalii unahizo cable, sijui mbuga gani Duniani ina lami. Huyu jamaa kasomea ujinga
 
Mkuu cable care ni nzuri ila mi naona kama BANDARI inachangia zaidi pato La taifa kuliko huo mlima.Hasa upanuzi ukikamilika mapato yataongezeka zaid kwa kupokea meli kubwa zaidi
Hakuna tija yoyote kuongeza kina halafu sio mara ya kwanza kuongeza kina na baada ya muda kinajifukia tena,meli zilizopo sasa tunashindwa kuzihudumia hatuna miundombinu mizuri tunataka tu ziongezeke?ukiangalia barabara ya kuingilia bandarini ambapo mizigo yote ndio inapotokea imeoza haifai kabisa barabara ina mashimo kama mahandaki halafu tunataka ufanisi wa bandari!
 
Sijui waota nini
Ule mlima watu wanaufaidi kwa kupanda kwa miguu
 
Tizama ndugu sijui kama unaufahamu mzuri wa kupanda mlima na kupanda cable car. Kupanda mlima ni utalii kwani njiani utaona vitu vingi na kuchukua picha zake za kumbu kumbu sasa ukienda kilele cha mlima utakuwa hujapanda mlima. Hizi picha unazolweha hapa labda tuweke cable car milima ya usambara ambapo hakuna mtu anayepanda huko na tunaweza kuwekeza restaurants na casinos vinginevyo utafuta maana ya kupanda mlima
Kuwe na optioni zote mbili,maana sio wote wanaweza kupanda kwa kutembea,hata vijana wenye afya zao nzuri wanashindwaga kupanda kwa kutembea halafu kumbuka watalii wengi wana umri mkubwa.
 
Ona picha ulizoweka ni picha za cable cars za milima iliyo katikati ya miji sio milima ya utalii. Jifunze maana ya hiking kwanza kabla ya kuandika pumba za cable cars kisa tu umeona picha. Unajua nchi ngapi zinategemea bandari yetu? Mbuga gani yenye lami Duniani? Umeandika pumba za kiwango cha shahada ya uzamivu
Wapi ameandika mbuga zijengwe lami?naona unarudiarudia neno lami.
 
Wachaga mna roho mbaya za kutaka maendeleo yawafikie nyie tu..
Unaongea kabisa bila uoga utalii una mapato kuzidi bandari?!!

Ungesema wasipanue bandari wakaweke madawa hospitali,kuna mikoa lami wanaiona kwny TV..eti nyiny mzidi kuneemeshwaa..milima yenyewe wanapanda wazunguu..bora wangepanda waTz wenzio
 
Hii ni pumba first class; cable car Kilimanjaro, lami mbugani, bandari isiboreshwe, umesomea ulichooandika kweli?

Milima ya kitalii ni kwaajili ya hiking sio kutumia cable unless huo mlima upo katikati ya mji. Nchi gani wameweka cable car kwenye mlima wa utalii Everest, Himalayas au mt Kenya au wapi huko? Utalii unachangiwa na vivutio vyote nchini sio Kilimanjaro tu ndiyo maana Pato la utalii ni kubwa. Bandari ikiboreshwa na kusimamiwa vizuri ina wateja wengi na wauhakika kila siku. Lami mbugani wakati hata mijini hazijaisha, nchi gani wameweka lami mbugani kila Kona? We jamaa umeenda shule kusomea ujinga
Kwani ikiwekwa cable car, njia ya kupanda kwa miguu itafungwa? Atakayetaka kufanya adventure ya hiking atafanya asiye na nguvu Ila ana interest tu ya kufika kileleni atatumia cable car.
Bandari ni muhimu utalii pia muhimu so hapo kupanga vipaumbele.
 
The beauty of Mt Kilimanjaro ni kupanda kwa miguu na watalii wengi wanakuja kwa sababu ya kupanda kwa miguu.
What the point ya kupanda kwa kutumia cable car. Ukisha kileleni utasema umepanda mlima Kilimanjaro?

Hii itapunguza watalii wengi wa nje labda wa hapa nyumbani wanaotaka kulinda vitambi vyao.
Sio wote wanaweza kupanda kwa miguu,kuupanda mlima kilimanjaro kwa miguu sio shughuli ndogo.na kumbuka watalii wengi umri ni mkubwa kwahiyo hawawezi kuupanda kwa miguu.
 
Back
Top Bottom