Fedha za upanuzi wa bandari zingetumika kujenga Cable car Mlima Kilimanjaro!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,696
2,000
Upanuzi wa bandari kwa sasa hauna tija.
Hizo bilioni mia tatu zingetumika kujenga cable car ya kupandishia watalii mlima Kilimanjaro ndio mradi ambao ungekuwa na tija zaidi.
Tanzania inapata mapato mengi zaidi kwenye utalii kuliko hata kwenye bandari. So ingekuwa ni vyema zaidi tukaboresha sekta ya utalii...

Kwa sasa kwa kuwa mlima Kilimanjaro ndiyo habari ya mujini kwa watalii wengi na wengi wanaofika huishia kuuona kwa mbali kwa kuwa hawana nguvu na afya za kupanda mlima, ujenzi wa cable car ungesaidia watu wengi zaidi ikiwamo watalii wa nje na watalii wa ndani kupanda mlima kwa urahisi.
Kwa kuwa tuna watalii angalau milioni moja wanaotembelea nchi kwa mwaka, kila mmoja angelipa angalau laki moja kupanda mlima kwa kutumia cable car, tungeweza kugenerate mapato yasiyopungua bilioni mia moja kwa mwaka, na hiyo pesa ingeweza kurudhi ndani ya mda mfupi tu ikiwa ni pamoja na kukuza sekta!

Wamabere

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
790
500
Upanuzi wa bandari kwa sasa hauna tija.
Hizo bilioni mia tatu zingetumika kujenga cable car ya kupandishia watalii mlima Kilimanjaro ndio mradi ambao ungekuwa na tija zaidi.
Tanzania inapata mapato mengi zaidi kwenye utalii kuliko hata kwenye bandari. So ingekuwa ni vyema zaidi tukaboresha sekta ya utalii ikiwa ni pamoja na kujenga bara bara za lami kwenye mbuga za wanyama ili ziweze kupitika mda wote (I hope environmentalist wataafiki hili).

Tizama ndugu sijui kama unaufahamu mzuri wa kupanda mlima na kupanda cable car. Kupanda mlima ni utalii kwani njiani utaona vitu vingi na kuchukua picha zake za kumbu kumbu sasa ukienda kilele cha mlima utakuwa hujapanda mlima. Hizi picha unazolweha hapa labda tuweke cable car milima ya usambara ambapo hakuna mtu anayepanda huko na tunaweza kuwekeza restaurants na casinos vinginevyo utafuta maana ya kupanda mlima
 
karanga mbichi

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
269
250
Upanuzi wa bandari kwa sasa hauna tija.
Hizo bilioni mia tatu zingetumika kujenga cable car ya kupandishia watalii mlima Kilimanjaro ndio mradi ambao ungekuwa na tija zaidi.
Tanzania inapata mapato mengi zaidi kwenye utalii kuliko hata kwenye bandari. So ingekuwa ni vyema zaidi tukaboresha sekta ya utalii ikiwa ni pamoja na kujenga bara bara za lami kwenye mbuga za wanyama ili ziweze kupitika mda wote (I hope environmentalist wataafiki hili).

Kwa sasa kwa kuwa mlima Kilimanjaro ndiyo habari ya mujini kwa watalii wengi na wengi wanaofika huishia kuuona kwa mbali kwa kuwa hawana nguvu na afya za kupanda mlima, ujenzi wa cable car ungesaidia watu wengi zaidi ikiwamo watalii wa nje na watalii wa ndani kupanda mlima kwa urahisi.
Kwa kuwa tuna watalii angalau milioni moja wanaotembelea nchi kwa mwaka, kila mmoja angelipa angalau laki moja kupanda mlima kwa kutumia cable car, tungeweza kugenerate mapato yasiyopungua bilioni mia moja kwa mwaka, na hiyo pesa ingeweza kurudhi ndani ya mda mfupi tu ikiwa ni pamoja na kukuza sekta!

Hakuna kinachoingiza mapato makubwa kuliko bandari mkuu acha kudanganya
 
Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,696
2,000
. Hizi picha unazolweha hapa labda tuweke cable car milima ya usambara ambapo hakuna mtu anayepanda huko na tunaweza kuwekeza restaurants na casinos vinginevyo utafuta maana ya kupanda mlima
Ndio maana nchi za kiafrika zimeendelea kubaki nyuma kwa kuwa na viongozi wenye fikra mgando kama za kwako! :oops::oops::oops:
 
Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
5,680
2,000
Hii ni pumba first class; cable car Kilimanjaro, lami mbugani, bandari isiboreshwe, umesomea ulichooandika kweli?

Milima ya kitalii ni kwaajili ya hiking sio kutumia cable unless huo mlima upo katikati ya mji. Nchi gani wameweka cable car kwenye mlima wa utalii Everest, Himalayas au mt Kenya au wapi huko? Utalii unachangiwa na vivutio vyote nchini sio Kilimanjaro tu ndiyo maana Pato la utalii ni kubwa. Bandari ikiboreshwa na kusimamiwa vizuri ina wateja wengi na wauhakika kila siku. Lami mbugani wakati hata mijini hazijaisha, nchi gani wameweka lami mbugani kila Kona? We jamaa umeenda shule kusomea ujinga
 
ILAN RAMON

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
7,131
2,000
Hapana kumbuka wengine wazer au wasio na nguvu ya kupanda kwa miguu wewe unawasrmea wenye ubavu ambao ni adventures...haws watapanda tu.kwa miguu hata cabke ikiwekwa
QUOTE="Wamabere, post: 21646146, member: 376486"]Tizama ndugu sijui kama unaufahamu mzuri wa kupanda mlima na kupanda cable car. Kupanda mlima ni utalii kwani njiani utaona vitu vingi na kuchukua picha zake za kumbu kumbu sasa ukienda kilele cha mlima utakuwa hujapanda mlima. Hizi picha unazolweha hapa labda tuweke cable car milima ya usambara ambapo hakuna mtu anayepanda huko na tunaweza kuwekeza restaurants na casinos vinginevyo utafuta maana ya kupanda mlima[/QUOTE]
Hapana
 
Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,696
2,000
Hii ni pumba first class; cable car Kilimanjaro, lami mbugani, bandari isiboreshwe, umesomea ulichooandika kweli?
Wapinga kila kitu huwa wapo! Jana nilikuwa nasoma kitabu cha Saikoloji ili nipate kuwaelewa watu kama wewe!
Ona picha ulizoweka ni picha za cable cars za milima iliyo katikati ya miji sio milima ya utalii. Jifunze maana ya hiking kwanza kabla ya kuandika pumba za cable cars kisa tu umeona picha. Unajua nchi ngapi zinategemea bandari yetu? Mbuga gani yenye lami Duniani? Umeandika pumba za kiwango cha shahada ya uzamivu
 
babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,474
2,000
The beauty of Mt Kilimanjaro ni kupanda kwa miguu na watalii wengi wanakuja kwa sababu ya kupanda kwa miguu.
What the point ya kupanda kwa kutumia cable car. Ukisha kileleni utasema umepanda mlima Kilimanjaro?

Hii itapunguza watalii wengi wa nje labda wa hapa nyumbani wanaotaka kulinda vitambi vyao.
 
Wewe unasema hivyo kwa kuwa waafrika tumeshazoea shida. Wazungu wangekuwa wanapenda shida kama wewe, wasingegundua vitu vyote hivi vilivyopo Duniani ambavyo vinarahisisha maisha ya mwanadamu!
 
bwii

JF-Expert Member
May 24, 2014
1,209
2,000
Hakuna kitu kizur na cha fahar km kupanda mlima kwa miguu ndio maana wanaoshindwa kufika kilelen wanashikwa na uchungu na kuahidi kurudia kupanda siku zingine, halafu pia ukiweka cable car utakuwa umeongeza tatizo la.ajira kwan vijana weng wakaz wa moshi na arusha hutegemea zaid utalii hivyo maendeleo ya hiyo miji itarudi nyuma kutokana na mzunguko wa pesa kuwa mdogo hivyohivyo ajira ambazo zingetokana na bandari kuanzia matengenezo hadi operations kuanza hazitakuepo.
 
Jun 14, 2017
74
125
Upanuzi wa bandari kwa sasa hauna tija.
Hizo bilioni mia tatu zingetumika kujenga cable car ya kupandishia watalii mlima Kilimanjaro ndio mradi ambao ungekuwa na tija zaidi.
Tanzania inapata mapato mengi zaidi kwenye utalii kuliko hata kwenye bandari. So ingekuwa ni vyema zaidi tukaboresha sekta ya utalii ikiwa ni pamoja na kujenga bara bara za lami kwenye mbuga za wanyama ili ziweze kupitika mda wote (I hope environmentalist wataafiki hili).

Kwa sasa kwa kuwa mlima Kilimanjaro ndiyo habari ya mujini kwa watalii wengi na wengi wanaofika huishia kuuona kwa mbali kwa kuwa hawana nguvu na afya za kupanda mlima, ujenzi wa cable car ungesaidia watu wengi zaidi ikiwamo watalii wa nje na watalii wa ndani kupanda mlima kwa urahisi.
Kwa kuwa tuna watalii angalau milioni moja wanaotembelea nchi kwa mwaka, kila mmoja angelipa angalau laki moja kupanda mlima kwa kutumia cable car, tungeweza kugenerate mapato yasiyopungua bilioni mia moja kwa mwaka, na hiyo pesa ingeweza kurudhi ndani ya mda mfupi tu ikiwa ni pamoja na kukuza sekta!

Huu ni upuuzi No 1 , huwezi jenga Barabara tena ukaweka rami mbugani au kwenye hifadhi , hii ZERO Brain .
 
Jomy

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
425
250
Mkuu cable care ni nzuri ila mi naona kama BANDARI inachangia zaidi pato La taifa kuliko huo mlima.Hasa upanuzi ukikamilika mapato yataongezeka zaid kwa kupokea meli kubwa zaidi
Nusu ya pato la Taifa ni bandari japo wazo lake ni zuri
 
Raphello

Senior Member
Mar 20, 2017
162
250
Huko ni kusafiri kuelekea kilele cha mlima na sio kupanda mlima,,ila ziwepo njia zote mtu atachagua mwenyewe.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom