Fabregas ana tatizo la msuli au "hamstring" ambalo limemfanya akae bench kwenye ziara ya Arsenal kule bara la Asia na hata nyumbani. Hata hivyo alianza kufanya mazoezi madogomadogo ili kumuweka kwenye hali ya kimchezo.
Sisi wapenzi wa Arsenal tunamshukuru kwa kutuwezesha kuwa na timu nzuri ambao yeye akiwa nahodha alitoa usaidizi mzuri kwenye timu. Tunamtakia kila la kheri akiwa Barcelona ingawa sidhani kama atacheza jumapili kwenye kombe la Super dhidi ya Real Madrid.
Kinachosubiriwa ni kuona kama Fabregas ataweza kupenya kwenye first 11 ya Pepe Guadiola ambao tayari ina Iniesta, Alcantara, Pedro, Xavier, Mascherano Busquests, Alves and alike.