Ushuhudi wa alichokisema Messi kwa board ya Barcelona upo na bado unaendelea :Kama kuku aliekatwa shingo
Another saga ya kuchanganyikiwa board ya Barcelona wamemuuza semedo so hatuna natural RB
Yaani mchezaji anakubali kuondoka team kubwa kama Barcelona anaenda Wolves -team ndogo ya wa portuguese kwa sababu anaona kabisa Barcelona hakuna bright future
Enyi watu nawaambia tuanze kuzoea ,Messi Barcelona huu ni msimu wake wa mwisho
Hata Kama Suarez kachoka huwezi kufanya replacement yake eti awe Depay ,unamkosea heshima El Pisterero (top 5 goal scorers wa Barca ame make history no matter what),na laana yake haitakosa kututafuna ,hivi niwaulizeni Paco Alcacer na Depay nani ni mzuri?au umeshawahi kujiuuliza kwanini wanahangaika usiku na mchana ili aletwe muholanzi Depay ,kwani Griezman aliletwa kwa kazi gani?hawamuamini tena?mbona waliunguza fedha nyingi sana kuletwa pale hadi ,financial status ya team ikakosa nafasi ya kumrudisha Neymar?The board is confused ,nani anajua sababu aliuzwa sub ya Suarez Paco Alcacer akaenda aka perform sana Borrusia Dortmond hadi alipokimbizwa na Halaand na kuamua kurudi zake Villarreal na kuacha kumbukumbu kule mwaka juzi?
Acha hilo mwezi uliopita wamefanya kituko kingine wamemuuza kijana wa miaka 23 kutoka America ya kusini team ya Gremio straight to Barcelona alikuja msimu wa 2018, Arthur Mello na wakamchukua Pjanic Milarem ambaye ana miaka 32 ,muda huo huo wakilalamika kua midfileder za Barcelona umri umekwenda (Sergio Busquets ,Ivan Rakitic ,Artulo Vidal),Hivi mnakumbuka ujio wa Paulinho 2017?msinichekeshe
Hivi mnakumbuka Barca mwezi February walimnunua striker Martin Braithwaite kwa pound mil 24 tena kutoka leganes ya Spain ambae alitetwa kwa mkopo kutoka Middlesbroug ya Germany??kulikua na sababu gani ya kumuuza Carlez Perez kwenda AC Roma(natural striker wa lamasia ambaye alikaririwa nchini Italy baada ya kuuzwa akisema pale Barcelona watoto wachanga board haina uvumilivu na sisi wa Lamasia )?
Je Messi anaposema Barcelona hamna project yoyote ,wala mpango wa kuitumia Lamasia kujenga team, wanafukia tu kashimo anakua amekosea?actions za board ya Barcelona speaks more than their promises
Tumeona kwa watoto waliopotezewa ramani na dira ya kuchezea team yao ya ndoto hii ni baadhi tu ya mifano Carlez Arena ,Riqui Puig huyo ametiwa depression recently ,tumeona kwa akina Miranda ,Dennis Suarez ,Munir El hadaad ,Deleofeu ,Sergi Samper ,Fundi Marc Cucurella eti unamuuza then unamnunua Junior Firpo eti ndio replacement ya Jordi Alba?
Hivi mnajua Thiago Alcantara bado mdogo wake Rafinha Alcantara yuko bado Barcelona anakopeshwa tu kila mwaka mara Inter Milan ,mara Celta Virgo ,kaka aliji offer tena kwa Barcelona sio chini ya mara tatu kuanzia 2016 baada ya kuuzwa kwa bei ya kutupwa mwaka 2015 akaelekea Buyern?Yeye wakati anakua pale Lamasia Cantera watoto wenzake walikua Wana brand na kumuita Kama the next Andrew Iniesta ,usishangae yeye kuongoza kupiga key passes na pass acuuracy ya 95% plus kwa sababu alikulia hivyo Lamasia na Barcelona ndio home hadi mzee wake Mazinho Alcantara ana card ya trusted legend wa Barcelona ,je unajua board walisema nini ?eti bora tumchukue Wijnaldum wa Liverpool
Hapo sitaki kupigilia msumari wa deal la usajili wa Dembele na Coutinho,wala saga la Neymar alivyoenda PSG na kutamani kwake mara moja kurudi Barcelona jinsi walivyolishughulikia
Nina wasiwasi Ansu Fatti ,chini ya menager wake mpenda fedha Mendez, team itakayo muhitaji ikifikia tu dau la kutosha ,Barcelona hawatajishauri mara mbili watamuuza na kumuacha Dembele

,kwani si tumeona kwa mtoto mdogo Xavi Simons (the next Xavi ) alivyouzwa PSG mwaka 2018?
Hatuna future pale ,let's begin from the scratch ,namtabiria mabaya sana huyu mzee wa kiholanzi