Fatuma Karume: Zanzibar inaidai Tanzania bara 4.6 trillion

View attachment 1768230

Hivi Nyerere na Karume walivyochanganya ule udongo wa bara na visiwani kwenye kile chungu waliweka agano gani?

Na baada ya kuuchanganya waliupeleka wapi?

Atakayejua kile chungu kilipo na udongo wake na yale maneno anaweza vunja Muungano.... na sasa sababu hauvunjiki tuunde Serikali moja malalamiko yaishe
Hahahha na huu Muungano umedumu kwa sababu hiyo hiyo ya kutokua na formula inayoeleweka. Udongo ulichanganywa wa nchi mbili ili kupata nchi moja. Lakini Zanzibar imebaki kama nchi katika mambo flani na haina mamlaka kama nchi katika mambo flani ambayo Jamhuri ya Muungano ndio itatambulika kama nchi na kuyasimamia. Huku Tanganyika yenyewe ikiwa imepotea kwenye ramani.

Nadhani Nyerere alitaka hiki kizanzibari kiwe kimkoa ila alichemka ndio maana walikubaliana katika mambo flani na mambo flani ambayo Karume hakuyakubali wakapewa mamlaka yao full. Leo hii wazanzibari wanaona kama kuna kitu wanakikosa kumbe yale wanayoyakosa ndio yalikuwa makubaliano ya Nyerere na Karume yawe mambo yanayosimamiwa na serikali ya Jamhuri.
 
Halafu wakarudije nyuma? Hivi Comoro si ni visiwa?

Kwa bidhaa za magendo?

Ukumbuke hata ardhi ya kuwatosha wenyewe hawana, watatoka kwetu wataenda kwa wengine kuwa sehemu ya nchi na mshirika wa muungano.

Kilwa ilikuwa na umeme na sarafu, ikiwa yakwanza kwa huku bara giza kama nilisikia vizuri.
Comoro ni visiwa na watu wake kitamaduni wanafanana na wananzibar na maendeleo ya comoro ni yakawaida sana
 
Kuna msemo unasema Picha ni zaidi ya maneno. Hii ni dhahiri inatoa picha halisi juu ya muungano. Nyerere kabeba vikopo vyote vya mchanga akilazimisha muungano. Ilitakiwa wawili wachanganye mchanga kuashiria hiari ya kuunganisha.

Ukisoma machapisho mengi utaona bado wengi wanafikiri kama vile Zanzibar ni mali ya Tanganyika. Hivyo wanaweza tena kulazimisha na kuifuta serekali ya visiwa hivyo. Nataka niwapeni pole sana visiwa vile kunaishi binadaamu kama ilivyo sehemu nyengine ya dunia. Hakuishi wanyama pori kule ukafikiria ukiamka leo asubuhi unasema serekali moja!

Tukio la baada ya hiyo picha ndio kuleee Karume alikopeleka udongo
 
Unanijumuisha mimi na hao waliotumia nguvu?

Mimi sipo Tanzania miaka zaidi ya 20, sina chama cha siasa na sijaishabikia serikali ya Tanzania kuhusu Zanzibar.

Ukianzisha chama cha Zanzibr kujitenga naweza kukusaidia mchango.

Mtuondolee kelele zenu za kijinga.
Unaposema kuwa nakujumuisha wewe na waliotumia nguvu, na kwamba hupo Tanzania na hushabikii serikali kisha unasema tukuondolee kelele zetu nashindwa kukuelewa. Kelele zetu zinakukerea nini na ya Tanzania hayakuhusu? kiherehere tu kinakusumbua
 
Wee ngumbaru jifune kusoma kwa ufahamu kwanza kabla hujanikaribia.

Unanipa kazi ya kukufundisha kusoma na mimi sina muda huo.
 
Fatuma Karume amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaidai Serikali ya Jamhuri ya Muungano kiasi cha pesa cha trilioni 4.6 kutokana na kupokonywa kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo

Fatuma Karume ambaye mara kwa mara hujimwambafai kukulia Ikulu ya Zanzibar na hivyo kuwa anafahamu siri nyingi ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Serikali ya Muungano imekuwa na kasumba ya kuipora pesa Zanzibar ambazo zipo Kikatiba na Kisheria juu ya Muungano

My take : Hawa Wazanzibar hawaridhiki kila siku wanaibuka na kero mpya ifike pahali tuunde Serikali moja including Zanzibar iwe kimkoa tu tutumie nguvu tu

USSRView attachment 1768148
Hii ndiyo hasara ya muungano ambao hauna usawa. Kipande cha ardhi kisicholingana na hata wilaya ya Bara kinapewa hadhi kisichostahili na tunadanganya kuwa tuko sawa. Kama mnaona mnanyonywa nendeni zenu kwa mabwana zenu wa kiarabu muone kama uamuzi wenu ni wa busara.
 
Hahahha na huu Muungano umedumu kwa sababu hiyo hiyo ya kutokua na formula inayoeleweka. Udongo ulichanganywa wa nchi mbili ili kupata nchi moja. Lakini Zanzibar imebaki kama nchi katika mambo flani na haina mamlaka kama nchi katika mambo flani ambayo Jamhuri ya Muungano ndio itatambulika kama nchi na kuyasimamia. Huku Tanganyika yenyewe ikiwa imepotea kwenye ramani.

Nadhani Nyerere alitaka hiki kizanzibari kiwe kimkoa ila alichemka ndio maana walikubaliana katika mambo flani na mambo flani ambayo Karume hakuyakubali wakapewa mamlaka yao full. Leo hii wazanzibari wanaona kama kuna kitu wanakikosa kumbe yale wanayoyakosa ndio yalikuwa makubaliano ya Nyerere na Karume yawe mambo yanayosimamiwa na serikali ya Jamhuri.
Endelea kujifunza.
 
Kinachonisikitisha mimi ni Huu Uzanzibar ambao sasa umefikia hata Mzanzibara yaani alozaliwa bara hata kama wazazi wake wote walizaliwa Zanizbar sii MzanIbar na hawezi kugombea Uongozi wa Zanzibar. Yametokea haya baada ya baadhi ya Wazanzibar kudai kwamba rais wa Zanzibar ndugu Hussein Ally Mwinyi kazaliwa Bara hivyo hana sifa za kuongoza Zanzibar!

Mawazo haya, mwl. Nyerere aliyapiga vita na kutuasa tusiyape nafasi lakini sasa inaonekana wazi kabisa kuna nguvu kubwa inatumika kutugawa Watanzania. Tuweni makini sana na watu hawa na nadhani isike mahala tuseme SASA BASI.. Hivi sasa naandika nipo katika maansalizi ya kuandika makala yangu inayohusu Ubaguzi huu nikianza kwa kuuliza MZANZIBAR NI NANI?
 
Huyu dada anapitia "midlife crisis", aidha mume hafanyi kazi yake kisawasawa, mpuuzeni na mumsamehe, hakajuwi kasemalo wala vitendo..
 
Back
Top Bottom