alishindwa kura za maoni, na chama hakina ulaji kama ccm... angefanya nini na yeye anahitaji mlo?
Mkuu Acid !,
Simtetei Mama Maghimbi,Lakini Mimi kama walivyo wengi hapa nimeshangazwa sana na Mama huyu kuondoka CUF na kurudi CCM.Kati ya Viongozi wa vyama vya Upinzani niliokuwa nawaamini kutokana na michango yao Bungeni na kwenye Majimbo yao ni pamoja na Mwanamama huyu ambaye kwa Taaluma ni mwanasheria.
Mama Fatma Mussa Maghimbi (64) alikuwa ni Mwanzilishi wa Chama cha CUF,na ana uhusiano wa karibu na Katibu Mkuu wa Chama hicho Seif Sharif Hamad.Mama huyo ambaye ameolewa Bara,na Mmoja wa Waanzilishi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro Mzee Mussa Y.Maghimbi aliingia CUF mwaka 1992 na amekuwa Mbunge wa Chake chake (Mkoa wa Pemba Kusini) toka mwaka 1995.Kabla ya hapo Mama huyo alikuwa mfanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam toka mwaka 1971.
Pamoja na mambo mengine Mama Maghimbi amekuwa mshiriki wa moja kwa moja wa siasa za Pemba na haswa CUF pamoja na kwamba muda wake mwingi anautumia Dar-es-salaam anakoishi na familia yake,yeye pamoja na Prof.Haroub Othman (RIP) na Mzee Hassan Said ni waanzilishi wa Zanzibar Legal Services Centre (ZLSC),Taasisi inayotoa ushauri na huduma za kisheria bure kwa watu wasio na uwezo,katika vipindi tofauti Mama Maghimbi amekuwa kiongozi wa Upinzani Bungeni na pia amekuwa Waziri Kivuli wa Mambo ya Katiba na Sheria.
katika kura za Maoni za CUF zilizofanyika mwezi Mei Mama Maghimbi pamoja na Wabunge wengine 11 walishindwa katika kura za maoni.Inawezekana kuwa Mama Maghimbi kahama CUF kwa sababu za kutofautiana na sura mpya za sasa zilizopo CUF,ambako kumejaa vijana wengi wenye damu ya mabadiliko ya haraka.
Mama Maghimbi amesoma sheria Chuo Kikuu cha D'salaam mwaka 1989 na baadaye kusoma shahada ya pili ya sheria Warwick, England mwaka 1994.Mama Maghimbi ana watoto 3.