kama wanaofanya kwenye industry hii na haya ndio maelezo yao basi watz bado tuna safari ndeeefu.Check-in cut off time wamesema 40min....ina maana natakiwa kuja muda wowote before cut off time, hata kama ni kasoro dakika moja.Tujifunze kufuata utaratibu...tatizo watu wa airlines wanauza nafasi kwa watu walio kwenye waiting list.......40 min zinamtosha abiria kutoka check in dest kwenda departure lounge. Kwa waendao nje muda unaongezeka kwa sababu ya taratibu za uhamiaji.
Remember! FASTJET - SMART TRAVEL
if ur not smart you won't travel by fastjet............!
Hizo sheria umezitoa wapi mkuu?
Naomba msaada ili nisije kufumaniwa.....
Hadi leo najua kuwa local flights in saa 1 kabla ya safari na international flights in 2-3hrs.
Hizo za kwako umezitoa wapi kaka?
Babu DC!!
Kaka acha kulinganisha international flight na local.. Mfundishe huyu Tiba ajue kwamba international wanasaidia wanaochelewa but local airline haiwezekani maana wanakodisha madirisha ya check in
Binafsi ni mteja mzuri sana wa fast jet na nitaendelea kuwa mteja wao kwa sababu nimeyakubali mapungufu yao.. Na ukilinganisha Fast jet na precision fast jet wana mapungufu machache kuliko precision.. Muhimu ni kuelewa terms and condition zao vizuri...
Terms za fast jet reporting time ni 3 hours before departure na ukichelewa sana watakusaidia lakini mwisho wa kufanya check in ni 40 minutes before departure.. So kwa kigezo hicho mtoa mada alichelewa check in..
Na wanafanya hivyo sababu Fast jet hawana dirisha la check in kama qatar au emirates. Wao wanachofanya wanaazima dirisha kwa ajili ya check in na ndio maana wanasema dakika 40 before safari hawawezi kusaidia wacherewaji sababu muda wa kukodisha dirisha unakuwa umeshaisha...
Binafsi nilishachelewa Qatar airways nakumbuka ilikuwa tarehe 24/6/2012 pale JNIA na tulifika saa sita kama na nusu hivi wakati ndege inaondoka saa 7 lakini kwa huruma walikuja wafanyakazi wao wakawasha computer za check in, wakatuprintia sticker za bags.. Tukachekiwa airport fasta na tukaingia kwenye ndege na kuondoka na hii iliwezekana sababu wao wana dirisha lao maalumu pale airport hawakodishi na wana haki ya kuwasha computer muda wowote tofauti na fast jet wanaotegemea Swissport..
Ukichelewa local airline imekula kwako lakini ukichelewa international airline unaweza ukaeleweka na kuwashiwa computer for check in maana wanajua wao wanatembea kwa Connections kwenye hubs zao so wakikuacha wanajua utateseka sana kwenye connection maana kuna miji mingine hazina connection flights za kila siku so lazima upandishwe ndege tu ili wakuokoe ukaiwahi connection yako
Ni uzoefu wa kutumia ndege za namna hiyo. Nilishashuhudia ndege ikiondoka dakika 15 kabla ya muda ulioandikwa na kisa walikuwa wanatakiwa kuipeleka ndege sehemu nyingine ikabebe abiria. Waliacha hadi watu waliokuwa wamecheck-In.
Ni ushauri tu wa kusema "za kuambiwa, changana na za kwako." Siyo lazima uufuate wangu. Wewe fuata waliouandika wao yaani dakika 40 kabla kama dada yetu hapo juu.
Pole sana kwa matukio na samahani kwa nitakayoyasema.
Nilishaona kwa macho yangu, desk check ya Turkish Air ikiwa imefungwa saa moja kabla. Ila alikuwepo Mbabe mmoja akapiga simu kwa mama mmoja ndani na wakafungua ingawa wafanyakazi wa Turkish Air walishasema kuwa hadi kesho.
Naona nyie mlikosa mtu kama huyo.
Ila nashindwa kuelewa kitu kimoja, ninavyofahamu mie ni kuwa kwa sasa kwa sheria za ulinzi zilivyo uwanja wa ndege, unatakiwa ufike masaa mawili kabla yaani dakika 120 kabla. Sasa wewe nani alikuambia unafika dakika 40 kabla? Dakika 40 kabla ni kuwa ndiyo mnajiandaa kwenda kuingia kwenye ndege tayari na si kwamba ndiyo unafanya Check-In.
Naona ukaja tena kuchelewa hata Bus la kwenda KIA. Yaani hata Bus likakuacha jamani? Nalo sijui utasingizia nini?
Pole sana kwa tukio ila kumbuka kuwa uwanja wa ndege unatakiwa kufika saa MBILI kabla popote pale duniani labda kama umesha Check-In online na huna mzigo, yaani unafika tu na kuingia ndani kusubiri kupanda ndege.
Mhhh kama hali zenyewe ndio hizi bora niendelee na box tu, at least life is predictable kwa maeneo flani huku duniani...... ntarudi huko badae sana kuja kula pensheni ya box
CC. Nyani Ngabu na wabeba box wooote popote walipo.
Whaaat! Kumbe na wewe unapiga boksi?
Mimi ndio najiandaa kuzamia pande za boxini, ila nishapewa orientation ya kazi yenyewe inavyofanyika(akili kidogo ukitoka hapo unapata hot shower unapata kapuchino au kinginecho, unakaa online unasoma blog zote za bongo weeee, unabishana blogini weeeeeee, unapiga umbea wote then unalaza ubavu kidogo box linaaza tena next day....mzunguko unajirudia hadi muda wa pensheni)...........vipi kuna la ziada uniongezee nondo?
Pole sana mkuu.....kumbe tulikuwa wote pale......ila mwenzio nilicheza ushapu nikaondoka na 5H-CCM.......
Hahahaha!!!Very high Risk traveling by buses! magari ya Arusha ni majeneza yanayotembea. Generally, usafiri wa mabasi ni majeneza yanayotembea! They are very rough!
Tik Tak ukiwa umevaa Msuli na hasa kama umesahau kale kanguo kadogo ni hatari
Pole Tiba hata mimi niliwahi kukutana na dhahama inayofananafanana ya kwako kutoka kwa hao FastJet. Ukweli ni kwamba sales officers wao hawako makini wanapowasiliana na wateja.Mimi nilisafiri nao kwa mara ya kwanza kutoka DAR kwenda KIA lakini yaliyonipata kabla ya ku check in niliapa sijku hiyo kuwa sitarudia tena kutumia usafiri huo.akwa kifupi nililipishwa nauli mara mbili kwa kosa lililotokana na uzembe wasales officer wao