Fanya jaribio hili usiku, nakuhakikishia utaona vitu visivyo vya kawaida angani

magwiji Rakim, Mshana Jr et al mara nyingi wamekuwa wanajitolea hapa jf kuelimisha kuhusu hisia ya sita.

kwa kupitia topic hii napata hisia kwamba inawezekana wtz wengi hawajui kuitumia hisia hiyo au wengi hawajaliwa kipawa cha kutumia hisia hiyo.yaani wapo wapo tu.
Wakija watasema uliona maruweru ila naamini dunia hii ina vingi binadamu hatuvijui kwa macho ya kawaida, ila kwenye mlango mwingine
 
Mimi ni madadisi sana, hupenda sana kudadisi vitu visivyo vya kawaida.

Katika udadisi wangu situmii mbinu yoyote ya kisayansi bali hupenda kutumia macho, pua, masikio na zaidi hisia.

Kuna siku mida ya saa saba za usiku umeme wa tanesco ulikuwa umekatika, sikuweza kustahimili joto la ndani ya nyumba maana AC/feni bila umeme haiwezi kufanyakazi.

Basi nikaamua nitoke zangu nje ya nyumba kupunga upepo.

Kwa kuwa umeme ulikuwa umekatika, nje ya nyumba kulikuwa kimya sana huku anga likiwa na utulivu usio wa kawaida.

Hali ya kukatika kwa umeme ukafanya eneo lile liwe na kiza sana na kufanya nyota za angani zionekane kwa uzuri bila tashwishi.

Hapohapo likanijia wazo la kutazama angani kwa utulivu ili nishangae nyota.

Basi nikavuta pumzi na hisia ya juu sana nikiwa nimetazama angani nikilitafakari anga, nyota na uwezo usio wa kawaida wa aliyeviumba.

Nililitazama anga kwa takribani kama dakika kumi au kumi na tano bila kutikisika nikiwa katika tafakari au hisia ya juu sana(sijui wenyewe ndio mnaita hisia ya sita).

Basi ghafla nikaanza kuona vitu visivyo vya kawaida vikitembea angani, niliona mamia ya nyota zikisogea kwa kupishana taratibu kutoka point moja kwenda point nyingine.

Vitu vingine nilivyoviona siwezi kuvielezea kwa uzuri, mpaka leo bado navitafakari.

Nakusihi na wewe fanya jaribio hili, unaweza kuona maajabu zaidi ya niliyoyaona mimi.

Kwa hakika anga lina maajabu sana na limetunza siri nyingi.
Huu mchezo niliufanya nulipokuwa mtoto. Maajabu ni kuwa, unachokiona wewe jirani yako Anaweza asikione, Badala yake anaweza akakiona kitu kingine cha tofauti
 
Mtu akivuta sigara kali au akilewa pombe, ni jambo la kawaida kuona maajabu kama hayo anapotazama angani.
 
Mkuu naona taratibu unaanza kuingia kwenye zile anga za Mzee wa upako na yule mwezie nani hiii...Mwingira.;)
 
kilichokufanya uwe mdadisi ni kwasababu umeme ulikatika tu, ungekuwa mdadisi ungekuwa unaangalia anga kila siku hivyo ungekuwa unadadisi vitu vingi tu......mfano mm najua ni sayari gani zinaonekane kwa ukaribu leo, ISS iko position ipi ya dunia, chombo gani kinategemewa kurushwa angani na makitu mengi tu siyo hayo maruweruwe yako uliyoona......ukitaka kujua ni maruweruwe fumba macho kwa dakika kumi halafu fungua uone.......
Mkuu uzi wako ungeweza fupisha kwenye sentensi mbili tu
Hongera mkuu kumbe unamiliki AC
ulikua unaona maruerue mkuu
Ulivuta bangi kidogo?
Mi nilijua labda kuona wachawi wakiwa uchi ni wachungulie
Nimechekaaaaaa mpaka Nimesakamirwaaa.
Mtu akivuta sigara kali au akilewa pombe, ni jambo la kawaida kuona maajabu kama hayo anapotazama angani.
hakuna half time??
....
 
Mkuu unanikumbusha miaka ile ya kweusi; basi Tanesco wakifanya yao; tunatoka nje kuhesabu nyota mpaka ukirudi ndio unarudi ndani kulala.
 
Vitu vingine ulivyoviona visivyo vya kawaida na hauwezi kuvisimulia, ndiyo nini!
Kauli yako hiyo kwamba hauwezi kusimulia mambo uliyoyaona yasiyokuwa ya kawaida, kunaifanya thread yako nzima iwe ni ya kusadikika.
 
Mimi ni madadisi sana, hupenda sana kudadisi vitu visivyo vya kawaida.

Katika udadisi wangu situmii mbinu yoyote ya kisayansi bali hupenda kutumia macho, pua, masikio na zaidi hisia.

Kuna siku mida ya saa saba za usiku umeme wa tanesco ulikuwa umekatika, sikuweza kustahimili joto la ndani ya nyumba maana AC/feni bila umeme haiwezi kufanyakazi.

Basi nikaamua nitoke zangu nje ya nyumba kupunga upepo.

Kwa kuwa umeme ulikuwa umekatika, nje ya nyumba kulikuwa kimya sana huku anga likiwa na utulivu usio wa kawaida.

Hali ya kukatika kwa umeme ukafanya eneo lile liwe na kiza sana na kufanya nyota za angani zionekane kwa uzuri bila tashwishi.

Hapohapo likanijia wazo la kutazama angani kwa utulivu ili nishangae nyota.

Basi nikavuta pumzi na hisia ya juu sana nikiwa nimetazama angani nikilitafakari anga, nyota na uwezo usio wa kawaida wa aliyeviumba.

Nililitazama anga kwa takribani kama dakika kumi au kumi na tano bila kutikisika nikiwa katika tafakari au hisia ya juu sana(sijui wenyewe ndio mnaita hisia ya sita).

Basi ghafla nikaanza kuona vitu visivyo vya kawaida vikitembea angani, niliona mamia ya nyota zikisogea kwa kupishana taratibu kutoka point moja kwenda point nyingine.

Vitu vingine nilivyoviona siwezi kuvielezea kwa uzuri, mpaka leo bado navitafakari.

Nakusihi na wewe fanya jaribio hili, unaweza kuona maajabu zaidi ya niliyoyaona mimi.

Kwa hakika anga lina maajabu sana na limetunza siri nyingi.
Aliyekuambia Nyota zinapishana taratibu ni nani huyo Mualimu tumchape!
 
Hicho ulichoona si chochote bali kinaitwa kitaalam "OPTICAL ILLUSION " na mara nyingi hutokea baada ya mtu kukodolea kitu kimoja kwa muda mrefu kama jinsi ulivyofanya.
 
Back
Top Bottom