Fanya jaribio hili usiku, nakuhakikishia utaona vitu visivyo vya kawaida angani

Hizo dalili za uoga.
Vitu vingine ulivyoviona visivyo vya kawaida na hauwezi kuvisimulia, ndiyo nini!
Kauli yako hiyo kwamba hauwezi kusimulia mambo uliyoyaona yasiyokuwa ya kawaida, kunaifanya thread yako nzima iwe ni ya kusadikika.
Msimpuuze Jamani.
Mm nimemwelewa
Aliyekuambia Nyota zinapishana taratibu ni nani huyo Mualimu tumchape!
Hicho ulichoona si chochote bali kinaitwa kitaalam "OPTICAL ILLUSION " na mara nyingi hutokea baada ya mtu kukodolea kitu kimoja kwa muda mrefu kama jinsi ulivyofanya.
..
 
hahahaha...kiukweli niliingiwa na uoga wa kuendelea na huo udadisi, sikutaka kuendelea.

mpaka hii leo sijajaribu tena kwa hofu ya kuona vitu vingi zaidi ambavyo wanadamu hatupaswi kuviona au kuvijua.

wanadamu tumewekewa ukomo wa kujua baadhi ya siri. wenyewe wanakwambia kuna siri ukishazijua tu hupaswi kuendelea kuishi,lazima ulipie gharama ya kifo.
True .....na ndio maana ukifa hurudi! Kuja kutuletea letea umbea na mengine kuongeza chumvi, yaan Sir God alijua!
 
Mimi ni madadisi sana, hupenda sana kudadisi vitu visivyo vya kawaida.

Katika udadisi wangu situmii mbinu yoyote ya kisayansi bali hupenda kutumia macho, pua, masikio na zaidi hisia.

Kuna siku mida ya saa saba za usiku umeme wa tanesco ulikuwa umekatika, sikuweza kustahimili joto la ndani ya nyumba maana AC/feni bila umeme haiwezi kufanyakazi.

Basi nikaamua nitoke zangu nje ya nyumba kupunga upepo.

Kwa kuwa umeme ulikuwa umekatika, nje ya nyumba kulikuwa kimya sana huku anga likiwa na utulivu usio wa kawaida.

Hali ya kukatika kwa umeme ukafanya eneo lile liwe na kiza sana na kufanya nyota za angani zionekane kwa uzuri bila tashwishi.

Hapohapo likanijia wazo la kutazama angani kwa utulivu ili nishangae nyota.

Basi nikavuta pumzi na hisia ya juu sana nikiwa nimetazama angani nikilitafakari anga, nyota na uwezo usio wa kawaida wa aliyeviumba.

Nililitazama anga kwa takribani kama dakika kumi au kumi na tano bila kutikisika nikiwa katika tafakari au hisia ya juu sana(sijui wenyewe ndio mnaita hisia ya sita).

Basi ghafla nikaanza kuona vitu visivyo vya kawaida vikitembea angani, niliona mamia ya nyota zikisogea kwa kupishana taratibu kutoka point moja kwenda point nyingine.

Vitu vingine nilivyoviona siwezi kuvielezea kwa uzuri, mpaka leo bado navitafakari.

Nakusihi na wewe fanya jaribio hili, unaweza kuona maajabu zaidi ya niliyoyaona mimi.

Kwa hakika anga lina maajabu sana na limetunza siri nyingi.
mmmh! saa hizo nje kuna mbu wengi sana! sijui ulimudu vipi kutulia bila kujikuna kwa dakika 15 mfululizo. au uko wapi?

Huko juu kuna satellites nyingi sana zimerushwa, hivyo sio ajabu kuziona angani gizani, wachilia mbali vimondo
 
kwa kuwa uliangalia muda mrefu kwa kunyanyua shingo misuli ya fahamu ilichoka ikakuletea vitu vya ajabu na nyota kupishana inawezekana uliona satellite zikitembea
 
True .....na ndio maana ukifa hurudi! Kuja kutuletea letea umbea na mengine kuongeza chumvi, yaan Sir God alijua!
mmmh! saa hizo nje kuna mbu wengi sana! sijui ulimudu vipi kutulia bila kujikuna kwa dakika 15 mfululizo. au uko wapi?

Huko juu kuna satellites nyingi sana zimerushwa, hivyo sio ajabu kuziona angani gizani, wachilia mbali vimondo
kwani ulikunywa ngapi ?
kwa kuwa uliangalia muda mrefu kwa kunyanyua shingo misuli ya fahamu ilichoka ikakuletea vitu vya ajabu na nyota kupishana inawezekana uliona satellite zikitembea
..
 
Nililitazama anga kwa takribani kama dakika kumi au kumi na tano bila kutikisika nikiwa katika tafakari au hisia ya juu sana(sijui wenyewe ndio mnaita hisia ya sita). Basi ghafla nikaanza kuona vitu visivyo vya kawaida vikitembea angani, niliona mamia ya nyota zikisogea kwa kupishana taratibu kutoka point moja kwenda point nyingine. Vitu vingine nilivyoviona siwezi kuvielezea kwa uzuri, mpaka leo bado navitafakari.

Ahaa, hiyo hali inaitwa kusinzia na kuota Mkuu. Inawapata wengi tu wakiwa wametulia wakikaza fikra juu ya kitu kimoja. Ndoto ya kwazna ni kile kitu ulichokuwa umekazia fikra kabla hujasinzia.
 
Mleta thread kweli Chenga, nimekuja mbio nikidhani majaribio yako umeyafanyia maabara,

ulikuwa unasumbuliwa na usingizi hujaona kitu chochote..
 
Ahaa, hiyo hali inaitwa kusinzia na kuota Mkuu. Inawapata wengi tu wakiwa wametulia wakikaza fikra juu ya kitu kimoja. Ndoto ya kwazna ni kile kitu ulichokuwa umekazia fikra kabla hujasinzia.

Imagination.

Mleta thread kweli Chenga, nimekuja mbio nikidhani majaribio yako umeyafanyia maabara,

ulikuwa unasumbuliwa na usingizi hujaona kitu chochote..

..
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom