smarte_r
JF-Expert Member
- Nov 8, 2013
- 4,537
- 11,869
Nipo masikani kwangu usiku huu kwenye kitongoji fulani hapa Dar.
Umeme wa TANESCO umekatika kutokana na mgao. nje ya nyumba yangu kuna upepo mzuri wa asili na ukimya mwingi, yaani hata zile kelele za mziki kutoka bar na grocery za jirani hazisikiki.
Nikiwa hapa nje kulishangaa anga kutokana na maajabu yake ya kiuumbaji, ghafla nimeona nyota tatu angani mashariki mwa Dar zikitembea kwa kasi sana kuelekea magharibi mwa nchi.
Nimetafakari sana. sasa sijui ndio dalili ya mwana wa adamu kurudi duniani kwa mujibu wa maandiko ya dini?, Au labda anga letu limetembelewa na viumbe kutoka sayari za mbali(aliens )?.
Vipi wenzangu hamjaona chochote huko angani?