kadoda11
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 21,453
- 20,712
Mimi ni madadisi sana, hupenda sana kudadisi vitu visivyo vya kawaida.
Katika udadisi wangu situmii mbinu yoyote ya kisayansi bali hupenda kutumia macho, pua, masikio na zaidi hisia.
Kuna siku mida ya saa saba za usiku umeme wa tanesco ulikuwa umekatika, sikuweza kustahimili joto la ndani ya nyumba maana AC/feni bila umeme haiwezi kufanyakazi.
Basi nikaamua nitoke zangu nje ya nyumba kupunga upepo.
Kwa kuwa umeme ulikuwa umekatika, nje ya nyumba kulikuwa kimya sana huku anga likiwa na utulivu usio wa kawaida.
Hali ya kukatika kwa umeme ukafanya eneo lile liwe na kiza sana na kufanya nyota za angani zionekane kwa uzuri bila tashwishi.
Hapohapo likanijia wazo la kutazama angani kwa utulivu ili nishangae nyota.
Basi nikavuta pumzi na hisia ya juu sana nikiwa nimetazama angani nikilitafakari anga, nyota na uwezo usio wa kawaida wa aliyeviumba.
Nililitazama anga kwa takribani kama dakika kumi au kumi na tano bila kutikisika nikiwa katika tafakari au hisia ya juu sana(sijui wenyewe ndio mnaita hisia ya sita).
Basi ghafla nikaanza kuona vitu visivyo vya kawaida vikitembea angani, niliona mamia ya nyota zikisogea kwa kupishana taratibu kutoka point moja kwenda point nyingine.
Vitu vingine nilivyoviona siwezi kuvielezea kwa uzuri, mpaka leo bado navitafakari.
Nakusihi na wewe fanya jaribio hili, unaweza kuona maajabu zaidi ya niliyoyaona mimi.
Kwa hakika anga lina maajabu sana na limetunza siri nyingi.