Familia yaingilia ishu ya mwanaume shoga kumtaka mwanamuziki Jux

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,256
16,306

Familia ya staa wa Bongo Fleva, Juma Musa ‘Jux’ imeingilia kati ishu ya mwanaume ‘tata’, mkazi wa Dar, James Delicious aliyetangaza kumtaka kimapenzi msanii huyo ambaye ni mpenzi wa Mwanamuziki Vanessa Mdee ‘V-Money’.

Akizungumza na Wikienda kwa niaba ya familia, dada wa Jux, Fatu-ma Juma alisema kuwa hakuna kitu kinachowaudhi kama kijana huyo kutwa kutangaza kumpenda na kumtaka mdogo wao huyo wakati wote ni wanaume na ni kinyume cha maadili ya kidini (familia ya Kiislam), Kitanzania na Kiafrika kwa jumla.

“Kiukweli familia inachukizwa sana na tabia ya huyo kijana ambaye haoni aibu, tunamtaka kuacha mara moja kusumbua watu akitaka namba ya Jux la sivyo tutachukua hatua za kisheria kwani anatukera sana,” alisema Fatuma.

Hivi karibuni kijana huyo alitangaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa lazima ampindue Vanessa kwa Jux kwani anampenda jamaa huyo kupita kiasi.
 
Kwenda peponi imekuwa rahisi sana siku hizi kuliko ilivyozoeleka na mababu zetu.
 
Huyu fatuma naye anatafuta kick tu mbona mdogo jux katulia tuu.kwanza wakimstaki watamshtaki kwa kesi gani?
 
545015a02b592abf29ca2944b098c2c8.jpg
 
Mi nashangaa nchi hii wanadunda tu yaani hatujakubali ushoga lakini tunawaacha hawa wanatanua tu kwa uhuru wao.
 
Wallah huu mtihani mzito..yani hata enzi za marehemu akina aunt Reila na aunt Abuu hawajahi kuwa ng'ang'ania wanaume wenzao hadharani hivi.
 
Back
Top Bottom