Ajiua na kumtaka bosi wake akamzike Musoma badala ya Moshi

Munch wa annabelletz47

JF-Expert Member
Aug 13, 2019
963
1,346
Kijana Kepteni Warioba (23) amejiua kwa kujikata na mashine ya kupasua mbao leo Juni 16, 2023, Moshi mkoani Kilimanjaro, huku akiacha ujumbe wa kumtaka bosi wake aende kumzika mkoani Mara na asipofanya hivyo atakuwa anamuona na kumsumbua mara kwa mara.

Tukio hilo limetokea leo Juni 16, 2023, katika mtaa wa Kalkacha, ambapo mashuhuda wamesema kuwa marehemu alikuwa mfanyakazi wa karakana ya kupasua mbao ya tajiri anayefahamika kwa jina la Erasto, ambaye anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.

---
Moshi. Mwita Warioba (35), mkazi wa mtaa wa Kiusa wilayanihapa, amejiua kwa kujikata shingo na mashine ya kuchana mbao.

Tukio hilo limetokea siku moja baada ya kusimamishwa kazi kutokana na upotevu wa fedha katika kiwanda alikokuwa akifanya kazi, huku akiacha ujumbe kwa mwajiri wake.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Yahya Mdogo amethibitisha taarifa za tukio hilo lililotokea Juni 16 mwaka huu, katika mtaa wa Rau, kwenye kiwanda cha kuchana mbao.

Alisema mwili wa Warioba umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini, KCMC kwa uchunguzi zaidi.

Warioba, fundi seremala na mwenyeji wa Mkoa wa Mara alifikia uamuzi huo baada ya mwajiri wake kupanga kufanya ukaguzi wa hesabu kiwandani.

Inaelezwa Warioba aliwahi asubuhi kiwandani alikowasha mashine inayotumia umeme na kuamua kujitoa uhai.

Ujumbe ulioachwa

Katika ujumbe wa maandishi aliouacha ambao Mwananchi umeuona, alitaka mwili wake usafirishwe kwenda Musoma mkoani Mara na asizikwe Moshi.

Alieleza endapo atazikwa Moshi atasumbua familia ya mwajiri wake (jina tunalifadhi) kizazi hadi kizazi.

Alielekeza mali zake, vikiwamo vyombo akabidhiwe dada aliyemtaja (jina tunalihifadhi) na kwamba, alimpenda sana na alitaka kumuoa. Dada huyo ni jirani yake eneo la Line

Barua iliyoanza kwa kutaja jina la mwajiri ilieleza "...naomba unisafirishe hadi nyumbani, sitaki nizikwe huku Moshi, usipofanya hivyo na ukibisha mimi nitaendelea kukusumbua kizazi hadi kizazi, mimi nataka nikazikwe nyumbani.

"…mimi Mwita Warioba, nakataa kuzikwa Moshi, endapo ukikaidi utakiona cha moto, nitakusumbua hadi unirudishe nyumbani, naomba nipelekwe nyumbani, naomba vile vyombo vyangu mkampe dada wa saloon yuko pale ninapoishi Line Polisi anaitwa… nilimpenda sana, nilimuahidi kwamba namuoa lakini imekuwa hivyo, Mungu ametoa, Mungu ametwaa..."

Kaimu Kamanda Mdogo alisema Warioba alisimamishwa kazi kwa tuhuma za wizi wa fedha za mapato ya karakana hiyo na kutakiwa kutoa maelezo.

Mwenyekiti wa mtaa wa Kalikacha kilipo kiwanda hicho, Sweetfredy Maleo alisema wakati wa tukio hilo watu walikuwa wamelala na walishangazwa kusikia ngurumo ya mashine alfajiri.

Alisema alifuatwa nyumbani na kuelezwa kwamba kuna tukio hilo, ambalo limewafedhehesha.

“Nashauri vijana wanapokumbwa na matatizo wajaribu kutushirikisha au wapate ushauri kwa waliowazidi umri," alisema.

CREDIT: MWANANCHI
 
#HABARI Kijana Kepteni Warioba (23) amejiua kwa kujikata na mashine ya kupasua mbao leo Juni 16, 2023, Moshi mkoani Kilimanjaro, huku akiacha ujumbe wa kumtaka bosi wake aende kumzika mkoani Mara na asipofanya hivyo atakuwa anamuona na kumsumbua mara kwa mara.

Tukio hilo limetokea leo Juni 16, 2023, katika mtaa wa Kalkacha, ambapo mashuhuda wamesema kuwa marehemu alikuwa mfanyakazi wa karakana ya kupasua mbao ya tajiri anayefahamika kwa jina la Erasto, ambaye anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.
View attachment 2659754

#EastAfricaTV
It seems to be a DECOYING TECHNIQUE in order to conceal the real motive/cause of the death.
Extremely poor and bad if not a worse cover story.
 
#HABARI Kijana Kepteni Warioba (23) amejiua kwa kujikata na mashine ya kupasua mbao leo Juni 16, 2023, Moshi mkoani Kilimanjaro, huku akiacha ujumbe wa kumtaka bosi wake aende kumzika mkoani Mara na asipofanya hivyo atakuwa anamuona na kumsumbua mara kwa mara.

Tukio hilo limetokea leo Juni 16, 2023, katika mtaa wa Kalkacha, ambapo mashuhuda wamesema kuwa marehemu alikuwa mfanyakazi wa karakana ya kupasua mbao ya tajiri anayefahamika kwa jina la Erasto, ambaye anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.
View attachment 2659754

#EastAfricaTV
Amejikataje na hiyo mashine, ameweka kichwa au imekuwaje?
Au wame muondoa alafu wakamsaidia kuandika ujumbe.
 
Kijana Kepteni Warioba (23) amejiua kwa kujikata na mashine ya kupasua mbao leo Juni 16, 2023, Moshi mkoani Kilimanjaro, huku akiacha ujumbe wa kumtaka bosi wake aende kumzika mkoani Mara na asipofanya hivyo atakuwa anamuona na kumsumbua mara kwa mara.

Tukio hilo limetokea leo Juni 16, 2023, katika mtaa wa Kalkacha, ambapo mashuhuda wamesema kuwa marehemu alikuwa mfanyakazi wa karakana ya kupasua mbao ya tajiri anayefahamika kwa jina la Erasto, ambaye anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.

View attachment 2659754

#EastAfricaTV
akienda tarime atarudi moshi kwenye jeneza!!
 
Back
Top Bottom