Falling Again! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Falling Again!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ligogoma, Oct 16, 2011.

 1. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,133
  Likes Received: 849
  Trophy Points: 280
  Habari wana JF???

  Wewe ni baba umeoa mwanamke aitwaye Bahati (Jina ni Mfano tu) na umezaa nae mtoto aitwae Zawadi.

  Siku zote una gari yako na mkeo pia anayake ya kuendea ofisini kwake, siku ya siku gari yako ukapeleka gereji ikakulazimu uchukue ya mkeo coz yeye anatulia tu ofisini ila shuguli zako ni mizunguko mingi ila ulimuahidi utampeleka ofisini na utamfuata pia!!!

  Ulimpeleka asubuhi ukaondoka then jioni ukamfuata na ukamkuta hayupo tayari ikakulazimu umsubiri, ukajifungulia radio na kulaza siti ukajinyoosha humo kwenye gari ukimsubiri mkeo!!

  Ukiwa kwenye gari lilikuja kundi la wafanyakazi wenzie na mkeo pale kwenye parking ulipo ila wao wakiingia kwenye magari yao pia, mara baadhi yao walikuja karibu kabisa na gari uliyomo na mmoja akaanza kuongea; ` Sema babaa Bahati a.k.a. baba mdogo wa Zawadi tena inawezekana yule mtoto ni wa kwako mbona mmefanana makomo hivyo? naona umepozi karibu kabisa na gari ya mamaa, leo kakuachia uende nayo nini?? Jamaa yake anavyompenda mkewe akikikujua atakutenda mbaya, achana na wake za watu!!!

  Jamaa likajibu, `Acha kunizingua bana mie nimeanza nae mwaka jana mwanzoni wakati mtoto wake ana miaka minne sasa! Siwezi endesha gari aliyonunuliwa na mumewe, angenunua yake sawa. Aaaah!! Wapi simuachi aiseee!!! Lile zigo ukilikamatia ******** alooo siliachi!!!`

  Badae jamaa wakaondoka zao bila kuwa makini kama mule ndani ya gari kuna mtu, baada ya muda akaja mkeo mkaondoka!!

  The man is falling again, hana raha na anasema kabisa kuwa usingle unanukia!! Ia hajachukua hatua yoyote mpaka sasa!!

  SAsa wewe ndo huyo baba, utachukua maamuzi gani, na wewe mama utajiteteaje na huo msala??
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Oct 16, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mimi sio mbaba lakini ningemshauri achunguze zaidi kwani Bahati hayupo mmoja, na wala zawadi. Achunguze akipata jibu la uhakika ndipo afikirie hatua ya kuchukua.
   
 3. h

  hayaka JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  fatilia kwa makini kabla ya kuchukua hatua. Inawezekana ni utani wa ofisini!
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  duh...naomba urudie hapo kwenye lile zigo...********......nahisi uhondo uko hapo...

  halafu huyo baba mdogo na mume wake ni ndugu au?????
   
 5. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Nina assume huyo baba alisikia maneno hayo na kuwatambua kuwa wale ni wafanyakazi na mkewe...

  Kikubwa ni kumwambia wife' ili ajue nilisikia hizo habari.. Ni moyo wa wife' unajua ukweli na ni juu yake kuamua atachukua hatua gani either iwe kweli au si kweli..

  Kufuatilia zaidi mambo mengine ni kuongeza "stress" za maisha. Kama mmoja ana-cheat..kuna dalili na evidence nyingi za kusitisha zoezi linaloitwa "ndoa'
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...aiseee respect kwa jibu hili...sina la kuongeza.
   
 7. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,244
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimekusoma mimi kwanza naondoka naenda home kutengeneza taraka maana useng mtupu maana unataka ushahidi gani??mwambie mimi nawewe basi kama mnawatoto wadogo samehe jali watoto na mwambie jinsi alivyokukwaza nampe uhuru ajitetehe akubali kosa na aseme sirudii nina uhakika anaweza akawamwaga!
   
 8. AMINATA 9

  AMINATA 9 JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 2,132
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  unaakili sana ww mm penda sana veve loh!
   
 9. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  mi nina mspice islander....
   
 10. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,133
  Likes Received: 849
  Trophy Points: 280
  Siyo baba mdogo kama mdogo wa baba ila hapo alimaanisha kuwa baba halisi wa mtoto anayejulikana yupo, huyo ni baba mdogo kwa sababu anatembea na mama wa mtoto husika!!!

  Hiyo red hapo......hahahahahaaaaaa!!! Itapelekwa uvunguni!! Kuifuata kule kazi bana!!!
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...daaahhh, aisee slow down bana....sio kila unalolisikia lina maana sawa na 'unavyofikiria.'...usiache mke ungali bado unampenda.
   
 12. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Si walisema kabisa bahati ambae huyo bwana wake kapaki karibu ya gari alonunuliwa na mume wake, ambae ana mtoto wa miaka 4 etc, hapo taya ri umesha confirm wanaongelea mke wko. ila hakikisha hawakujua umo ndani ya gari coz sometimes mtu anaweza kujifanya kasema tu bila kujua upo, kumbe ana maana ya kufikisha ujumbe.
  Pia ongea na bahati mwenyewe.
   
Loading...