Faini ya bodaboda ilistahili kuwa Shilingi 50,000; tutashuhudia mengi kwa wasiozingatia usalama

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
12,212
2,000
Binafsi sijafurahishwa na faini za bodaboda kushuka na kuwa 10,000/-kwani kwa jinsi ninavyowafahamu hawa ndugu zetu na rika lao,10,000/- itakuwa si chochote kwao na watadharau sana utaratibu wa barabara zetu hivyo huenda maafa yakawa makubwa zaidi kuliko vile itakavyofikiriwa.

Jambo lingine ambalo napingana nalo ni kuwa, bodaboda wengi kutokana na faini kuwa kubwa wanashindwa kukomboa pikipiki zao, sidhani kama hili lina mashiko maana nyingi ya pikipiki zinazoshikiliwa vituoni ni zile ambazo zinakuwa zimehusika na matukio mbalimbali yakiwamo ya wizi, ujambazi, aidha pikipiki hiyo kumilikiwa isivyo halali na anapotakiwa mwenyewe ajitokeze mhusika hukimbia mazima.

N.B: Sekta hii imeleta ajira nyingi Sana kwa vijana wetu na ujana ni maji ya moto na maafa yanayosababishwa na vyombo hivi hugharimu maisha ya wengi ambao ni abiria wa vyombo hivi, madereva wa vyombo hivi wanastahili mafuzo maalumu ya usalama barabarani kuliko hata madereva TAXI kama kweli tunawapenda usalama wao na abiria wao.
 

MUREFU

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,328
1,500
Siku zote Mjinga Muwekee urahisi ili Ule sana ndio serikali ilichokifanya. Kumbuka hilo ni kwakosa Moja ni 10,000/= sasa wao wanakuwaga na zaidi ya kosa moja.

Huoni Pesa inaingia Serikalini ngoja uje kusikia itakuwa inakusanya kiasi gani kwa Mwaka.

Ninakwambia itaizidi Tochi za barabarani.
 

kwenda21

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
2,789
2,000
Wewe hujui, Mimi ninapikipi police wetu wanakosea Sana, aliyefanya boda wawe Kama unavyowaona ni Police, boda akiwa njiani Hana Raha, anajua muda wowote anakamatwa, hasimami kwenye mataa anaogopa kukamatwa Tena ingewekwa Sheria kabisa marufuku kuwakamata wakiwa wako kwenye mataa, pita mjini uone zilivyojazwa vituoni, faini ikiwa ndogo mtu atalipa aondoke, siyo police wote Ila Kuna baadhi.
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,273
2,000
Mambo ya Faini ni kudangayana Hio 50K uwezo wa kulipa anao? Hata hio 30K uwezo anao? Cha maana ingekuwa mtu ukiwa na makosa points kwenye leseni zinashushwa zikishuka sana unalazimishwa kwenda VETA kwa kulipia kujifunza upya na ukikataa unahukumiwa au hata kama hauna ADA unalipia through Community Service
 

Dullah07

Senior Member
Apr 12, 2017
152
500
Hapo sirikali itapata stahiki zake maana zamani walikuwa wanakwambia faini 30000 haya jiongeze ww hapo lazima utatoa 10 au 20 kukwepa hiyo 30 sasa unakuta sirikali haipati pesa bali inaishia mifukoni mwa watu
 

vanus

Member
May 27, 2017
75
150
Mtoa mada kumbe unajua kiswahili, naona ulikuwa unajifanya hujui maana ya kwendraa.
 

ze-dudu

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
14,713
2,000
Siku zote Mjinga Muwekee urahisi ili Ule sana ndio serikali ilichokifanya. Kumbuka hilo ni kwakosa Moja ni 10,000/= sasa wao wanakuwaga na zaidi ya kosa moja.

Huoni Pesa inaingia Serikalini ngoja uje kusikia itakuwa inakusanya kiasi gani kwa Mwaka.

Ninakwambia itaizidi Tochi za barabarani.
Mwaka mbali ivyo wiki tu
 

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
12,212
2,000
Mambo ya Faini ni kudangayana Hio 50K uwezo wa kulipa anao? Hata hio 30K uwezo anao? Cha maana ingekuwa mtu ukiwa na makosa points kwenye leseni zinashushwa zikishuka sana unalazimishwa kwenda VETA kwa kulipia kujifunza upya au wakikataa kuhukumiwa au hata kama hawana ADA walipie through Community Service
Zipo faini zinazowekwa ili kumuogopesha dereva asifanye makosa na si lengo la kuongeza mapato ni kwa ajili ya usalama wake na abiria asiye na hatia.
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
17,690
2,000
Hapo naona jamaa wa kubrashi wataondoka na buku buku tu

Na faini ya risiti iwe 50,000 ubaya ubaya tu
 

simon2016

JF-Expert Member
Oct 19, 2020
298
1,000
Alie toa ushauri sio boda boda na wala hajui uchungu wa kubambikiwa kesi .

Mimi kama bodaboda nawaomba abilia wangu humu mumpuuze.

Sisi ndio mnatutuma tuwaletee chips.
Sisi ndio tuna wawahisha kazini.
Sisi si ndio tunawaletea majiko ya gas halafu pesa mnatupa jioni na tunajua mmefulia.
Sisi tuna waheshimu mademu na michepuko yenu na nyinyi usiku mnatuamsha tuwabebe kuwapeleka mnapotaka bila kujali na sisi tunahitaji kukaa na familia


Mimi kama bodaboda nilie mkamata mkuu akiposha haki yetu nawaomba apuuzwe mara moja.

Nabeba abilia hapa badae.
 

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
12,212
2,000
Alie toa ushauri sio boda boda na wala hajui uchungu wa kubambikiwa kesi .

Mimi kama bodaboda nawaomba abilia wangu humu mumpuuze.

Sisi ndio mnatutuma tuwaletee chips.
Sisi ndio tuna wawahisha kazini.
Sisi si ndio tunawaletea majiko ya gas halafu pesa mnatupa jioni na tunajua mmefulia.
Sisi tuna waheshimu mademu na michepuko yenu na nyinyi usiku mnatuamsha tuwabebe kuwapeleka mnapotaka bila kujali na sisi tunahitaji kukaa na familia


Mimi kama bodaboda nilie mkamata mkuu akiposha haki yetu nawaomba apuuzwe mara moja.

Nabeba abilia hapa badae.
**Asante kwa wewe kuwa mstaarabu,na SIO mlevi kazini,simaanishi kwamba ni wote,ni vichwa ngumu hapana wapo bodaboda safi kabisa,lakini kiukweli wanaouthamini kazi hii 15/100.
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,273
2,000
Zipo faini zinazowekwa ili kumuogopesha dereva asifanye makosa na si lengo la kuongeza mapato ni kwa ajili ya usalama wake na abiria asiye na hatia.
Zinamuogopesha asifanye alafu hawezi kuzilipa akifanya then what ? Si ndio kutengeneza mianya ya Rushwa...
 

nanilii

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
302
500
kati ya vitu ambavyo wanasiasa mnakosea ila nyinyi hamujui ni suala la bodaboda,
yaani kwa kuwa wahanga wa matendo ya bodaboda hawana sehemu ya kukutania na kupaza sauti, basi nyinyi mnakomalia hapo hapo. ukweli ni kwamba watu wanachukizwa sana sana na mwenendo wa bodaboda na bajaji barabarni, lakini kwa kuwa wao wana vijiwe na ni rahisi kukusanyika na kupiga kelele mnadhani maumivu wanayo wao tu. sio siri kati ya vitu ambavyo sisi wananchi vinatuonyesha ubinafsi wa mwansiasa mbele ya kura, ni kutetea bodaboda na bajaji.

watu wanalia, watu wanakufa , watu wanpoteza viungo, watu wanharibiwa magari yao, lakini hawa watu hawana jukwaa la pamoja la kutoa vilio vyao. sasa nyinyi wanasiasa bila aibu mnadhani watu wanawafurahia kutetea bodaboda , kumbe watu rohoni wanumia sana , hasa wahanga.

sisi hatusemi zitungwe sheri mahsusi ya bodaboda pekee,, la hasha, sheria zipo , ziiipo !!! zisimamiwe tu !! tatizo ni nyinyi wansiasa, MAADHALI bodaboda wao wana vijiwe na wahanga wa bodaboda HAWANA VIJIWE, basi mnaegemea kwa bodaboda.

mkuu wa mkoa wa mbeya aligongwa na bajaji kweye kivuko cha waenda kwa miguu, yote haya hamuoni.
si jambo la kushangaza kuona bodaboda anatoka sehemu moja anakwenda sehemu nyingine mita 150, lakini spidi atakayokwenda nayo, akikutana na mtu anamuua, lakini hawajali.

kuna mfano alitoa mhe. Spika , kwamba huko ASIA , akari wamepewa viboko ili kudhibiti bodaboda , akapendekeza na hapa iwe hivyo, sijui iliishia wapi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom